WANIGERIA WA SIMBA WAREJEA KUITUMIKIA TIMU YAO!!

Mshambuliaji wa timu ya Simba Eme Ezechukwualiyerejea leo kutoka mapumzikoni Nigeria habari zaidi shuka chini.

Eme Ezechukwu kulia akiwa na mmoja wa wajumbe wa kundi la marafiki wa simba Mulamu Ng'ambi (Friends of Simba).

Wachezaji wa kimataifa kutoka Nigeria Eme Ezechukwu na Orji Obina wanaoichezea Klabu ya Simba jijini Dar es alaam wamerejea nchini kwa ndege tofauti jana na leo ambapo Obina aliwasili jana asubuhi na Eme Ezechukwu amewasili leo mchana ili kuendelea na kibarua chao katika timu hiyo yenye makao makuu mtaa wa msimbazi.

Akiongea na tovuti ya FULLSHANGWE mchezaji Eme amesema wamerejea kuitumikia klabu yao na kwamba anatarajia kuwa timu yao itacheza vizuri zaidi katika mashindano ya kombe la Tusker na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom ambayo inatarajiwa kuendelea mwanzoni mwa mwaka ujao.
Awali wakati wachezaji hao wakiondoka hapa nchini kurejea kwao kwa mapumziko kulikuwa na uvumi mwingi kuwa huenda wachezaji hao wasingerejea tena nchini baada ya mmoja wa wachezaji hao Orji Obina kukwaruzana na kocha Mburgaria Krasmir Benziski aliyekuwa akikifundisha kikosi hicho.
Eme ameongeza kuwa wachezaji wote tunahitaji kushirikiana na kuwa kitu kimoja ili kuiletea mafanikio timu yetu katika mashindano yaliyopo mbele yetu.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment