MAPOKEZI YA TAIFA STARS YAFUNIKA!!

Nurdin Bakari muuaji wa goli la Pili la Taifa Stars lililoteketeza kabisa ndoto za Timu ya Sudan kusonga mbele katika fainali za CHAN zitakazofanyika nchini Ivory Coast mwakani akiwa ametulia na kujifunika kitambaa kikubwa chenye rangi ya kijani katika viwanja vya kilimanjaro Kempiski.
Marcio Maximo akipokewa kwa Furaha na wafanyakazi wa Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski.

Kocha mkuu wa Taifa Stars Marcio Maximo kushoto akiwaamuru wachezaji wake kuvaa fulana zao tayari kwa kuingi katika chumba cha mkutano mara baada ya kuwasili katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski

Haruna Moshi (Boban) kulia katikati na Athuman Idd (Chuji) kushoto katikati na wachezaji wengine wakiimba kwa furaha walipowasili katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski
Wachezaji wa timu ya Taifa wakiwasili katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski katika basi dogo aina ya Toyota Hiace huku wakiwa kifua wazi na wakiwa wenye furaha kubwa.

Rais wa TFF Roadger Tenga akipongezana na makamu wake wa kwanza aliyemaliza muda wake Crescentus Magori walipokutana katika Hoteli ya kilimanjaro Kempiski ambako Taifa Stars ilikula chakula cha mchana mara baada ya kuwasili ikitokea Sudan leo.

Mwenyekiti wa kamati ya operesheni ushindi ya Taifa Stars Mbunge wa Singida Mjini Mh. Mhamed Dewaji kulia akiongea na Naibu waziri wa Nishati na Madini Adam Malima, Dewji aliongoza msafara wa kamati yake na kufanikiwa kupata ushindi ulioipeleka Taifa Stars Ivory Coast katika Fainali za (CHAN) zitakazofanyika mwakani.

Mh. Naibu waziri wa wizara ya Nishati na Madini Adam Malima kulia akitaniana na mjumbe wa kamati ya ushindi ya Taifa Stars Dr. Ramadha Dau, kati ni Makamu wa pili wa Rais TFF Ramadhan Nassib wakati wakisubiri kuipokea Taifa Stars ilipowasili ikitokea Sudan ambako ilipata ushindi mnono wa Goli 2-1 dhidi ya Sudan


Viongozi mbalimbali wa TFF wakiwa katika Hoteli ya Kilimnjaro Kempiski wakisubiri kuipokea timu ya Taifa TYaifa Stars ilipokwenda kupata chakula cha mchana leo katika hoteli hiyo kuanzia kulia niCrescentius Magori makamu wa kwanz wa Rais aliyemaliza muda wake,Muhsin Balhabou mjumbe wa kamati ya utendaji, Fredrick Mwakalebela katibu mkuu, Ramadhan Nassib makamu wa pili wa Rais na Sikazwe mjumbe kamati ya utendaji

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

1 comments:

  1. Kuanzia kushoto ndio magori

Post a Comment