Na Anna Nkinda – Maelezo
16/12/2008 Kikao cha siku mbili cha Kamati ya ushirikiano baina ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la kujenga Uchumi (JKU) kwa upande wa Zanzibar kinatarajia kuanza leo (kesho) makao makuu ya JKT Mlalakuwa jijini Dar es Salaam.
Kikao hicho cha siku mbili kinatarajiwa kufunguliwa na Kaimu Mkuu wa JKT Brigedia Jenerali Samweli Kitundu.
Pamoja na mambo mengine kikao hicho kinatarajia kuzungumzia jinsi ya kuimarisha ushirikiano wa jadi uliopo kati ya majeshi hayo, kutafuta nyanja mpya za ushirikiano zitakazoharakisha kukua na kuimarika kwa ushirikiano baina ya pande mbili na kuangalia maeneo ambayo kila upande utaweza kunufaika hasa upande wa kilimo na ufugaji.
Majeshi hayo yanaushirikiano wa muda mrefu tangu mwaka 1975 pale rais wa awamu ya pili wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Aboud Jumbe alipofanya ziara ndani ya JKT na kuvutiwa na majukumu ya Jeshi hilo katika malezi ya vijana ambapo alitoa msukumo wa kuanzishwa kwa kamati maalum ya ushirikiano baina ya pande mbili za Muungano.
0 comments:
Post a Comment