Habari zilizoifikia Tovuti ya FULLSHANGWE leo jioni na kutangazwa pia na vituo mbalimbali vya Radio zinasema wale wanamuziki maarufu Boyz 2 men kutoka Marekani waliokuwa watumbuize leo katika Viwanja Vya Leaders jijini Pamoja na mkali wa muziki mwingine kutoka nchini humo Joe Thomas hawatakuja tena kwakuwa mmoja wa wanamuziki hao anaumwa.
Habari kutoka kwa mmoja wa waratibu wa ziara hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina alisema Boyz 2 Men hawatakuja kwakuwa mmoja wao anaumwa lakini onyesho litafanyika kama lilivyopangwa ambapo sasa Joe Thomas atashirikiana na wanamuziki wawili kutoka Jamaica Tante Metro na Devonte Whos'.
Boyz 2 Men wanajulikana kwa shughuli yao pevu jukwaani na mashabiki wengi walilipania sana onyesho hilo lakini, pia mashabiki wengi waliokuwa hawaamini habari hizo walipata uhakika wa kutowasili kwa wanamuziki hao baada ya vituo vya Radio karibu vyote kutangaza kuwa wanamuiziki hao hawatakuja tena nchini.
wakati huohuo mwanamuziki Joe Thomas aliyeyuka na kutotokea katika hafla iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili ya kukutana na wageni waalikwa mbalimbali katika klabu ya usiku (Maisha Pub) Oysterbay jana usiku ambapo waalikwa mbalimbali wakiwemo vimwana walijimwaga ili angalau kupata picha na kuonana kwa karibu na mwanamuziki Joe Thomas.
Hafla ilikuwa ianze saa tatu kamili lakini mpaka saa tano na nusu hakuna mwanamuziki aliyekuwa amefika wala waratibu wa ziara hiyo ilipofika saa sita kasoro robo ndipo wanamuziki Tante Metro na Devonte Whos' walipoingia ukumbini hapo hata hivyo waalikwa karibu wengi walikuwa wameshaanza kuondoka kuelekea viwanja vingine huku wakilalamikia kitendo hicho.





3 comments:
Mercy galabawa i miss u ma dear, sijamuona huyu mrembo long time ila sasa mhhh mbona kama kawa mweupe??au ndo mambo ya macosmetic??
pamoja na hayo yote lakini i hate uvaaji wa fide, sorry kwa hii touch arrogant yangu but thats it!
jamani wewe mwenye bog mbona unaharibu majina ya watu? Messe ndio kitu gani? Frola ni nini? ah hebu jaribu kuwa mwangalifu uwavutie watu!
mmmh hizo eyeshadow za dollar store nini?
mdau U.S.A
Post a Comment