Mukubwa Deo Mwanambilimbi na Mamaa Debora Nyange hivi ni miongoni mwa vichwa vya kutegemewa katika Bendi ya Kalunde Band Mtu mzima Kasaloo Kyanga hayupo pichani lakini kamera ya FULLSHANGWE itamsaka mpaka impate na wenzake
Deo kati kushoto Mwakichui na kulia Said
Kuanzia kushoto Makichui, Said na Deo katika poozi
Bendi maarufu kwa sasa inayojulikana kama Kalunde Band iko mbioni kukamilisha Video yake inayokwenda kwa jina Naomba uniambie, akizungumza na FULLSHANGWE mkurugenzi wa bendi hiyo Bw. Deo Mwanambilimbi kwenye Club ya Rainbow Mbezi Beach ambapo bendi hiyo hufanya maonyesho yake amesema itakuwa ni Video ya kufungia mwaka.
Deo ameongeza kwamba kazi kubwa inafanyika hivi sasa kati ya wanamuziki wa bendi hiyo na Producer wa Big Time Studio Said Comorien ili kuhakikisha kazi hiyo inakuwa ya kiamataifa na wapenzi wetu wanaikubali ndani na nje ya Tazania.
Kama unavyojua mzee wa FULLSHANGWE Kalunde Band ilianza na moto na inataka kuuendeleza moto huo ili kuonyesha mashabiki wake kuwa muziki ni kazi kubwa na yenye heshima lakini kama unafanya muziki mzuri na wenye kuvutia wapenzi wako.
Ameongeza kuwa sambamba na kurekodi video hiyo pia wanakamilisha albam yao itakayokuwa na nyimbo sita kama vile Itumba Ngwewe ,Nataka nizae na wewe, Umenigusa nimekugusa, Naomba uniambie, Balaa na nyinginezo.
Amesema wanatarajia kuzindua albam yao mwezi ujao na huenda ikawa wakati wa sikukuu za X-Mass na maandalizi kwa ajili ya uzinduzi huo yanaendelea vizuri.
Deo amesifu kikosi cha Bendi hiyo kikiongozwa na yeye mwenyewe, mamaa Debora Nyange ambaye pi katibu wa bendi hiyo , mwakichui mtu mzima Kasaloo Kyanga aliyewahi kutamba na Bendi ya Tancut Almas ya mkoani Iringa enzi hizo na wana muziki wengine wakali walioko katika bendi hiyo, anongeza kuwa kikosi kimekamilika na kiko tayari kwa kuwapa Shangwe mashabiki kwa kwenda mbele.
0 comments:
Post a Comment