BLIND SOUND WAJA KISOMI KAMA P. SQUARE!!!

Vijana wa BLIND SOUND Abubakary Maiko a.k.a (majegea) na Jamaldin Athuman a.k.a (Wakuziba na kuzibua)




Abubakary Maiko Kulia kati Mrs Kitima na Jamaldin Athuman.



Kuanzia kulia ni mkurugenzi wa Dida Fashion Tanzania Jordan Kitima, msanii Jamaldin Athuman (wakuziba na kuzibua) mkurugezi wa Dida Fashion Uingereza Mrs Kitima, msanii Abubakary Maiko (Majegeka) na mlezi wao Daud Saleh katika picha ya pamoja mara baada ya kuongea na FULLSHANGWE.


Wasanii chipukizi kutoka kundi la Blind Sound wamekuja kwa kishindo kikubwa baada ya kuipua single yao moja inayokwenda kwa jina la (I wanna Know) waliyoiimba katika lugha ya kingereza na kiswahili na kuingiza sauti zenye mvuto wa ajabu.

Vijana hao ambao wote ni Vipofu Jamaldin Athuman aka (wakuziba na kuzibua) na Abubakary Maiko aka (Majegeka) wanavyo vipaji ambavyo mimi mwenyewe nilipowasikiliza sikuamini kwani waliniimbia akapela za wanamuziki mbalimbali kama vile Koffi Ololmide Werrason, Jb Mpiana na wengine wengi kutoka nchi za Amerika.

Nilidhani labda uwezo wao ni kuiga tu, lakini walinitolea mpya pale waliponiimbia wimbo wenye lugha ya kimakonde na kutia vionjo vya kabila hilo, kwakweli ilinivutia kuongea nao kwa muda ili niweze kujua mengi zaidi juu ya kazi yao ya muziki, wameanza lini na wametokea wapi?.

Vijana hao ambao ukiwaona unaweza kufikiri labda ni ombaomba si kwa mavazi ila kutokana na kwamba hawawezi kujiongoza wenyewe lazima waongozwe na watu wengine kazi ambayo inafanywa kwa umakini na promota wao kutoka kampuni ya Dida Fashion yenye makao makuu yake Uingereza kwani kila mmoja hushikwa mkono na kuelekezwa wapi apite na wapi akae.

Abubakary anasema walianza kwa kuimba sehemu mbalimbali katika kumbi za starehe na mabaa na walikuwa wakichangiwa labda kiasi cha shilingi mia tano hivi ndipo wanaanza kuimba, anaongeza kuwa wamenyanyaswa sana na watu mbalimbali na waliwafuata watu wengi wenye uwezo ili wawasaidie kuingia Studio lakini hawakufanikiwa kitu ambacho kiliwaumiza lakini hawakukata tamaa.

Anaongeza kuwa ndipo alipotokea mlezi wao wanayekaa nae hapa jijini Bw. Daud Saleh ambaye aliwachukua na kuishi nao nyumbani kwake "tunamshukuru kaka yetu kwani baada ya hapo tulikutana na Msanii H. Baba ambaye alitusaidia tukakutana na huyu dada yetu wa Kampuni ya Dida Fashion iliyotuona na kuamua kutupeleka Studio za Big Time Production zilizo chini ya Producer Said Comorien".

kwakweli hii Single yetu ya I wanna Know tumekamua ukitusikiliza huwezi kutofautisha na P, Square ya Nigeria tumejituma na kufanya ufundi wa hali ya juu ili kuwaonyesha mashabiki wa muziki kuwa tunakuja kwa moto mkubwa na hatutapenda uzimike na sisi sio vilema tunajua mungu atatuwezesha tutaonyesha maajabu katika muziki.

Abubakary ameongeza kuwa tayari wana nyimbo zingine Tisa ili kukamilisha Albam yao itakayokuwa na nyimbo kumi na kila wiki wanarekodi nyimbo moja, amezitaja nyimbo hizo kuwa ni Nikikumbuka,Kumukoo, kiwewe,Litana hii ni ya kimakonde,Fedha,sisi wasanii,Forever,Uvumilivu na Pigo la moyo, katika Albam hii pia watamshirikisha mwanamuziki H. Baba,Amemalizia na kusema kuwa Albam yao itakuwa na mahadhi mchanganyiko ikiwa ni Rhumba, Zouk Dansall HipHop laini.

Naye mkurugenzi wa Dida Fashion Mrs Kitima amesema tunajisikia vyema na sifa kubwa kwenye kampuni yetu ya Dida Fashion kwa kuwa na vijana wenye vipaji kama hawa unajua mtu anapokuwa na uwezo katika kitu chochote unachomsaidia hata kama gharama itakuwa kubwa wewe unajisikia furaha tu, kwani lengo ni mafanikio na lengo letu ni kuwafikisha mbali sana hawa wasanii wetu



You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment