VIJANA JAZZ YATUNGA WIMBO WA KUPINGA MAUAJI YA MAALBINO NCHINI!!



Mwenyekiti wa chama cha maalbino nchini Bw. Ernest Kimaya akionyesha picha ya mtoto Albino wa miezi saba anayedaiwa kuuwawa huko mkoani mwanza, Bendi ya Vijana Jazz imetunga wimbo maalum wa kuhamasisha watu wote kupambana na mauaji ya Maalbino kwa imani za kishirikina uanoitwa mauaji ya Albino picha hiyo ilionyeshwa kwa waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya habari maelezo jijini.




Katibu mkuu wa Bendi ya Vijana Jazz Kulwa Millonge akizungumza mbele ya waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Habari maelezo wakati akielezea kuhusu wimbo waliotunga kwa ajili ya kuhamasisha jamii kuachana na tabia ya kuua Maalbino kwa imani za kishirikina katikati ni Joseph Torner mratibu wa maandamano dhidi ya mauaji ya maalbino yanayotarajiwa kufanyika 19/10/2008 na mgeni rasmi atakuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Jakaya M. Kikwete na anayefuatia ni Ernest Kimaya.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment