BREAKING NEWSSSSS NASMA KHAMIS KIDOGO AMEFARIKI DUNIA!!

Marehemu Nasma Khamis Kidogo kushoto akiwa na Mwimbaji wa TOT Khadija Omar Kopa katika moja ya shughuli za Muziki wa Taarab enzi za uhai wake

Mwimbaji wa siku nyingi wa muziki wa Taarab aliyewahi kutamba na kundi la muungano lililokuwa likiongozwa na Mchezea nyoka maarufu Norbert Chenga Nasma Khamis "Kidogo" amefariki dunia leo kwenye Hospitali ya Temeke alikokuwa amelazwa kutokana na kuugua Maralia
Baba mdogo wa Marehemu ambaye amejitambulisha kwa jina la Mzee Kaniki akizungumza na vyombo vya habari nyumbani kwake Kinondoni Sharif Shamba ambako ndiko msiba uliko amesema Marehemu alikuwa na matatizo ya shinikizo la damu tatizo lililokuwa likimsumbua mara nyingi, hata hivyo siku za hivi karibuni alishikwa na maralia na kupelekwa katika Hospitali ya Temeke ambako alilazwa na kukaa hapo kwa siku nne mpaka mauti yalipompata usiku wa kuamkia leo
Nasma Khamins atakumbukwa kwa nyimbo zake nyingi nzuri zilizokuwa zikipendwa na mashabiki wengi wa muziki kama vile "Naona mambo iko huku" wimbo uliovuma sana wakati huo akiwa na kundi la muungano kundi hilo likiwa hasimu mkubwa wa kundi lingine la la muziki wa Taarab TOT, ambapo mwimbaji mshindani wa Nasma alikuwa alikuwa Khadija Kopa Mungu ailiaze mahali pema peponi Roho ya Marehemu Nasma Khamis Kidogo Amin

MWANARIADHA FABIAN JOSEPH AWATESA WENZAKE VODACOM DAR MARATHON!!

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Joel Bendera wa pili kushoto akishiriki mbio za Vodacom Dar Marathon 5km Fun Run, kushoto Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru, Mbunge wa zamani Jimbo la Kilolo Venance Mwamoto na mwisho Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Vodacom Tanzania Peter Kisumo.
Mshindi wa kwanza wa Vodacom Dar Marathon kilometa 21 Fabian Joseph akimalizia mbio hizo kwenye uwanja wa Uhuru , mbio hizo zilianzia katika uwanja huo ambapo amekimbia na kumaliza mbio hizo kwa muda mfupi kuliko wote kwa kutumia 1:3:43

Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa shirika la utangazaji la kimataifa BBC Abdalah Majura (kushoto) akibadilishana mawazo na Afisa Habari wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu wakati wa mbio za Vodacom Dares Salaam Marathon zilizoanzia kwenye uwanja wa Uhuru na kumalizikia hapo.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Joel Bendera kushoto akishuhudia wakati Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Ephraim Mafuru akimpongeza mshindi wa pili wanaume wa mbio za Vodacom Dar marathon kilometa 21 Martin Sulle mara baada ya kupokea zawadi yake ya shilingi 600.000, anayefuata ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Evance Balama na mwisho ni mkuu wa Udhamini na Mawasiliano Vodacom Tanzania George Rwehumbiza.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Joel Bendera kushoto akizungumza jambo na Kaimu mkuu wa mkoa wa Dar es alaam na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Evance Balama pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru leo kabla ya kutolewa zawadi kwa washindi wa Vodacom Dar Marathon kwenye uwanja wa Uhuru.

Wafanyakazi wa Benki ya KCB wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa shindano la Vodacom Dar Marathon ambapo Benki hiyo ilikuwa ni mdhamini mwenza wa Vodacom Tanzania.

Mmoja wa washiriki wa mbio hizo ambaye jina lake halikupatikana mara moja inadhaniwa alipata matatizo ya kurukwa na akili na kuanza kusema hovyo huku akivamia watu hovyo, katika purukushani hizo alimvamia mmoja wa wapiga picha wa magazeti ya serikali Habari Leo na Daily News Yusuph Badi ambaye hata hivyo alisaidiwa na watu waliokuwa karibu na Tukio hilo kama unavyomuona akiwa ameshikiliwa na wafanyakazi wa Msalaba Mwekundu.

Mwanariadha Fabian Joseph aliyeshinda mbio za Vodacom Dar Marathon kilomita 21 akipongezwa na mke wake Josephine na mtoto wake Olympia kama unavyowaona katika picha ya pamoja kwenye uwanja wa Uhuru leo.

Mshindi wa kwanza wa mbio za Vodacom Dar Marathon kilomita 21 kwa wanawake mwanariadha Sara Ramadhan akihojiwa na wanahabari baada ya kushinda mara baada ya kumaliza mbio hizo akiwa mwanamke wa kwanza.

Mshindi wa tatu mbio za Vodacom Dar Marathon kilomita 21 mwanariadha Dickson Marwa akihojiwa na waandishi wa habari mbalimbali mara baada ya kumaliza mbio hizo zilizonzia kwenye uwanja wa uhuru na kumalizikia hapo leo asubuhi.

Hawa ni wasiriki wa shindano la Vodacom Dar Marathon kilomita 21 wakipepea kwa uwezo wao wote kushindania dau la shilingi milioni moja na zawadi zingine lukuki hapa wakoa maeneo ya shimo la udogo Highway Kurasini katika barabara ya Mandela.

Washiriki wa mbio za Vodacom Dar Marathon kilomita 21 wakianza mbio hizo kwenye uwanja wa Uhuru leo asubuhi, mbio hizo ziliishia hapo.

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Joel Bendela akifungua rasmi mbio za Vodacom Dar es alaam Marathon 5km Fun Run zilizofanyika leo kuanzia uwanja wa Uhuru na kumalizikia hapo ambapo katik mbio hizo pia Naibu Waziri huyo alishiriki. kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Vodacom Peter Kisumo na wa nne ni mkurugenzi wa masoko kampuni ya Vodacom Ephraim Mafuru

M-NET LAUNCHES HOT NEW KENYAN DRAMA SERIES!!


June 2009
Can a marriage survive when the powerful ambitions of two busy career professionals collide explosively with their tense personal lives? Can a husband’s weaknesses destroy his wife’s hopes? Can two people, with everything to lose, find a love that lasts?

Welcome to M-Net’s sizzling new drama series CHANGES which debuts on DStv on Tuesday June 23 at 19:00 CAT! A contemporary drama uncovering the secrets behind the closed doors and apparent domestic bliss of 3 couples living in the upmarket Makao Close apartments in Nairobi, CHANGES promises must-watch viewing for anyone wondering...can love survive life?

At the heart of the series are 3 very different couples, each with their own challenges, fears, aspirations and triumphs. First up is quintessential career woman, Ugandan born Namata Gitau and her lawyer husband Alfred. Both are career driven but their differing opinions on when to start a family is creating conflict. As Namata pursues a pregnancy and tries to balance work and family, the eloquent and debonair Alfred is focussed on getting a promotion and being made a partner in his law firm.

Meanwhile their downstairs neighbours Jabali and Lupita Otieno face troubles of their own when their comfortable marriage of several years begins to slowly disintegrate. With two daughters depending on them, they must now try to resolve their issues or risk destroying their family forever. Lupita, stressed out homemaker and working mom, is driven to self-destructive behaviour by her charming, womanising husband, Jabali.

Couple no. 3 is gorgeous, glamourous Cindy Kamau and her older Tanzanian boyfriend Minja Kabwe who live in the most expensive flat at Makao Close. Enigmatic, chess playing Minja is wealthy, mysterious and will go to extraordinary lengths for family and for love. Generous but ruthless he keeps his family’s mining success a closely guarded secret. Meanwhile Cindy is learning how to make it on her own using her brains, not her body until the day when her past returns to haunt her…

Produced by Big Ideas Entertainment and based on an original story by Serah Mwihaki, CHANGES combines humour and drama, delving deep into the lives of these three couples as they work through domestic struggles and family life, with all its joys, desires, frustrations, tensions, and secrets.

Commenting on CHANGES, M-Net Africa Director Biola Adekanbi joins M-Net East Africa Program Manager Wangeci Murage in commending the series.
“To create any series is a real challenge and it’s one that M-Net is familiar with. There are no guarantees that a series will work because ultimately it relies heavily on timing, to get the mix just right, to get the episodes scripted, rehearsed, filmed, edited and onto screen. You have to start with a very strong story and then there’s that intangible element...that magic that makes it work, that makes it appealing to audiences.”

Adekanbi goes on to say, “Given that CHANGES accomplishes all this, M-Net is proud of its cast, crew and producers who’ve worked so hard to finish this 13-part series. It’s now done and ready for audiences to enjoy. So sit back, relax and enter a world where love is under the spotlight and ‘forever’ is put to the test.”

Audiences tuning in for the series, which was filmed on location in Kenya, will find a cast that also includes Ugandan and Tanzanian television personalities.
In starring roles are Kenyans Ian Mbugua (Alfred), Pierra Makena (Cindy), Godfrey Odhiambo (Jabali) and Renne Sewe (Lupita) with Tanzania’s Adam Juma (Minja) and Uganda’s Susan Nalwoga (Namata). In a key supporting role is Uganda’s Cleopatra Koheirwe as Nanziri.

For more information on CHANGES, to find out who’s who and what happens next, log on to http://www.mnetafrica.com/.

MISS SINZA 2009 APATIKANA!!

Miss Sinza 2009 Lulu Ibrahim katikati akipunga mkono mara baada ya kutangazwa mshindi katika shindano lililofanyika kwenye ukumbi wa Vatcan Sinza usiku wa kuamkia jana kushoto ni mshindi wa pili Rahma Faiz na kulia ni mshindi wa tatu Evastansia Temba katika shindano hilo burudani ilitolewa na watoto wa mujini Fm Academia na Kundi la The Chocolate linaloongozwa na mfalme Saboka.
Tano bora ya Miss Sinza 2009 kuanzia kushoto ni Lulu Ibrahim, Evastansia Temba,Liliani, Lane Wilson na Rahma Faiz mara baada ya jaji mkuu Boy George kutangaza tano bora.

Dada Jack Mbando kulia na mdogo wake Joyce Mbando wakifuatilia kwa makini wakati shindano la Miss Sinza 2009 lilipokuwa likiendelea kwenye ukumbi wa Vatcan Sinza usiku wakuamkia leo ambapo Lulu Ibrahim ameibuka mshindi katika shindano hilo .


TAMASHA LA NCHI ZA JAHAZI KUANZA JUNI 24 - JULAI 4 - 2009!!

Ofisa Mtendaji mkuu wa Tamasha la nchi za Jahazi ZIFF Prof. Martin Mhando akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika katika kituo cha utamaduni cha Ufaransa Alliance Francaise juu ya maandalizi ya tamasha hilo, linalotarajiwa kuanza juni 24 mpaka julai 4 mjini Zanzibar likishirikisha wanamuziki na wasanii kutoka nchi mbalimbali, ambapo kutakuwa na maonyesho mbalimbali ukiwemo muziki, Filamu, semina mbalimbali juu ya mapambano ya Ukimwi, Ngoma za Asili na mambo mengine mengi, huku mgeni rasmi wa Tamasha hilo akiwa mwigizaji filamu maarufu kutoka Hollwood nchini Marekani anayejulikana kama Danny Glover, wengine katika picha ni Hassan Mitawi katikati mwenyekiti wa ZIFF na mwisho kushoto ni Murugenzi wa kituo cha utamaduni cha Ufaransa Alliance Francaise Didier Martin.

Mwandishi wa habari kutoka shirika la utangazaji Tanzania TBC Evance Mhando aliyeshika kipaza sauti akiuliza swali wakati wa mkutano na waandaaji wa Tamasha la nchi za Jahazi ZIFF katika mkutano na wanahabari uliofanyika kwenye kituo cha utamaduni cha ufaransa Alliance Francaise leo.

Mwanamuziki Mwasiti kutoka THT akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo juu ya ushiriki wake katika tamasha la nchi za Jahazi ZIFF.

Mtangazajiwa Star Televisheni Saida Mwilima akimhoji msanii Kassim Mganga aliyeimba wimbo wa (Anewa) ambaye ni miongoni mwa wasanii watakaofanya onyesho katika Tamasha la nchi za jahazi ZIFF linalotarajiwa kuanza Juni 27 mpaka julai 4 mwaka huu mjini Zanzibar kulia ni mwandishi wa Star Televisheni Agness Baharia.

MSTAAFU UHAMIAJI AUKWAA UMILIONEA KUTOKA VODACOM!!

Vodacom Miss Tanzania Nasreem Karim(kushoto) akibonyeza kitufe kwa ajili ya kumpata mshindi wa Tuzo Milionea wa Milioni 100,ambapo Mzee Renatus Mkinga (59) mkazi wa Gongolamboto jijini Dares Salaam alijinyakulia kitita hicho.(kulia)Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania Mrisho Mlao kushoto ni meneja matukio wa vodacom Rukia Mtingwa.
Baaada ya kumpata Mshindi wa Tuzo Milionea.

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom kupitia promosheni yake ya ‘Tuzo Milionea’ jana usiku ilimpata mshindi wa jumla wa shindano hilo Renatus Mkinga (59) ambaye alijinyakulia kiasi cha milioni 100/- baada ya kushinda katika mchezo uliorushwa moja kwa moja na kituo cha TBC
Kupatikana kwa mshindi huyo kulifuatia mchakato mkali wa kumalizika kwa ungwe ya pili ya promosheni ya tuzo milionea ya kampuni hiyo ambayo iliwazawadia washindi 59 muda wa maongezi wa 100,000/- kutokana na droo zilizokuwa zikiendeshwa kila siku chini ya usimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha.
Akizungumza na mlinda mlango anayeaminika kuwa ni nambari moja nchini, Juma Kaseja kwa njia ya simu, Mkinga mkazi wa Gongolamboto jijini Dar es Salaam ambaye ni mstaafu wa idara ya uhamiaji makao makuu alisema amefarijika baada ya kushinda nafasi hiyo.
“Kwa kweli mimi ni mstaafu wa idara ya uhamiaji ambaye maisha yangu ni kama nilikuwa najikongoja kuyaendesha, lakini kwa umilionea huu kutoka vodacom ni matarajio yangu sasa ni kukamilisha ndoto zangu kadhaa za kimaisha kama kuanzisha miradi na vitega uchumi mbalimbali,” alisema Mkinga.
Ni kama Mkinga alikuwa na bahati ya kipekee kwani kabla ya kuchaguliwa kuwa mshindi washiriki kadhaa waliotangulia licha ya namba zao kujitokeza kwenye luninga zilipopigwa hazikupatikana ama kuwa hewani jambo lililopingana na kanuni na taratibu za michezo ya kubahatisha.
“Taratibu ni kwamba anayeshiriki hana budi kupigiwa simu, apokee na kuzungumza ili kuthibitisha ushiriki wake...hivyo kwa yule asiyepokea mara tatu ama akakataa kuongea atakuwa amejikosesha ushindi,” alisema Mrisho Milao kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha.
Akizungumzia kumalizika kwa mchakato wa kumpata mshindi wa promosheni ya pili iliyoanza Aprili, 2009, Meneja matukio na promosheni wa Vodacom, Rukia Mtingwa aliwashukuru Watanzania wote kwa waliokuwa bega kwa bega na kampuni hiyo wakati wa shindano hilo.
“Kwa niaba ya Vodacom nawashukuru wateja wetu wote walioshiriki katika promosheni hii na kwamba kumalizika kwa programu hii ni mwanzo wa mchezo mwingine utakaotangazwa baadaye,” alisema.
Mbali ya Kaseja na Milao wengine waliokuwepo kushuhudia kupatikana kwa milionea huyo wa Vodacom ni mwanariadha Dickson Marwa na Vodacom Miss Tanzania anayetarajia kukabidhi taji hivi karibuni Nasreem Karim.

Serikali ya Japan itatoa shilingi bilioni 14,216,000,000 kugharimia mradi wa maji kanda ya ziwa!!

Makamu wa Rais Dk Ally Muhamed Shein akiongea na Balozi wa Japan nchini Hiroshi Nagawa wakati alipomtembelea kwa mazungumzo ofisini kwake leo.

Clarence Nanyaro, Ofisi ya Makamu wa Rais
Serikali ya Japan itatoa shilingi bilioni 14,216,000,000 kugharamia mradi wa maji safi na salama kwa mikoa ya Mwanza na Mara ambao utatekelezwa kwa awamu tatu kuanzia septemba 2009 hadi 2011.
Akizungumza na Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein Jijini Dar es salaam leo, Balozi wa Japan hapa nchini Hiroshi Nagawa amesema kuwa serikali ya Japan inafurahishwa na mipango ya serikali ya Tanzania kuwapatia wananchi huduma za kijamii na nchi hiyo itaendelea kutoa misaada na kuimarisha ushirikiano uliopo.
Mradi huo wa maji safi na salama ambao utatekelzwa katika mikoa hiyo unategemewa kunufaisha vijiji 44 na kuongeza idadi ya watu watakaopata maji safi na salama kutoka 9,400 hadi 55,000.
Balozi Nagawa amesema kuwa kuwa samabamba na kugharamia mradi huo,pia serikali ya Japan itakamilisha ujenzi wa barabara ya Kilwa na kufanya upanuzi wa barabra hiyo hadi katika ya jiji la Dar Es salaam.
Balaozi Nagawa ameongeza kuwa,ili kuimarisha hali ya usafiri jiji Dar Es salaam, Japan itafanya upanuzi wa barabara ya Bagamoyo kuanzi eneo la Moroco hadi Tegeta kati ya Julai na Desemba mwaka huu.
Serikali ya Japan pia inafadhili ujenzi wa barabra ya kutoka Arusha kupitia Namnaga hadi Athi nchini Kenya.
Sambamba na balozi wa Japan,Dk Shein pia alionana na Mabalozi wa Denmark na Misri hapa nchini. Akizungumza na Makamu wa Rais, Balozi wa Denmark Bjarne Sorensen ambaye aliwasilisha ripoti ya kamisheni ya Afrika kuhusu kuongeza ajira kwa vijana ,aliitaka serikali kuendelea kuzifanyia barabara matengenezo badala ya kuziacha zikachakaa na kujenga upya ili kupunguza gharama.
Serikali ya Denmark ndiyo inagharamia upanuzi wa barabara kutoka Chalinze hadi Segera ambapo itakapo kamilika itakuwa na uwezo wa kupitisha magari mawili upande mmoja.Uzinduzi wa upanuzi wa barabara hiyo ulifanyika mwezi Mei mwaka huu katika eneo la Lugoba.
Aidha ,kuhusiana na ripoti ya kamisheni ya Afrika balozi Sorensen amesema kwa sasa wanandaa jinsi ya kuinadi ripoti hiyo katika Taasisi za kimataifa ili iwe ajenda ya kudumu na kuweza kuondoa tatizo la ajira linalowakabili Vijana wengi kwa sasa. Mkutano wa Kujadili matatizo ya ajira kwa vijana ulifanyika mwezi machi mwaka huu nchini Tanzania.
Kwa upande wake, balozi Wael Adel Nasr wa Misri, amesema kuwa kuanza tene kwa safari za shirika la ndege la Misri kutainifaisha Tanzania kutokana na kuleta watalii wengi.
Pia Misri imefuangua ofisi za kanda za shirika lake la ndege hapa Tanzania ili waweze kuhudumia wasafiri kutoka katika nchi nyingi zinzoizunguka Tanzania.
Serikali ya Misri pia inafadhili uchimbaji wa visima 30 katika Wilaya ya Same kwa lengo la kuwapatia wanachi maji na mradi huo unatagemea kuzinduliwa mwezi ujao mwanzoni.

BENKI YA EXIM YATOA MSAADA WA VITABU KWA SEKONDARI YA TAI (W) RORYA!!

Meneja Masoko na uhusiano wa Exim Benki Christina Manyenye wa kwanza kutoka kulia, Meneja wa Fedha wa Benki hiyo Lydia Kokugonza wa pili, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Tai iliyopo Wilaya ya Rorya mkoa wa Mara, Richard Okore (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Mikopo ya Elimu ya Juu George Nyatega wakiangalia vitabu vyenye thamani ya Shilingi Milioni Tatu vilivyokabidhiwa na benki hiyo kwa walimu hao, Dar es Salaam jana.
Meneja Masoko na uhusiano wa Exim Benki Christina Manyenye wa pili kutoka kulia, Meneja wa Fedha wa Benki hiyo Lydia Kokugonza (kulia), Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Tai iliyopo Wilaya ya Rorya mkoa wa Mara, Richard Okore (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Mikopo ya Elimu ya Juu George Nyatega wakiangalia vitabu vyenye thamani ya Shilingi Milioni Tatu vilivyokabidhiwa na benki hiyo kwa walimu hao, Dar es Salaam jana.

The last seven days at Emirates Stadium!!

Latest news… 24-year-old goalkeeper Lukasz Fabianski committed his future to the Gunners by signing a new long-term contract with the Club. Elsewhere Cesc Fabregas bagged Spain's fourth goal in their classy Confederations Cup victory over New Zealand. Also in international action were Theo Walcott and Kieran Gibbs who both started for England Under-21s as they beat Finland in their European Championship opener. Elsewhere Bacary Sagna dismissed rumours linking him with a move to Real Madrid.
The DRAFT Barclays Premier League fixtures 09/10
The DRAFT fixture list for next season has now been announced. Arsenal have been handed an away trip to Everton on the opening day of the season and will entertain Portsmouth in the first home Premier League clash of the campaign on August 22. However the Gunners' season will end on home soil as Fulham visit Emirates Stadium on the final day of 2009/10. you can see the full DRAFT fixture list on Arsenal.com. … MORE >>
Bergkamp and Henry lead the charge
We're now down to No 35 in our Top 50 countdown and, unsurprisingly, two Gunners legends are hogging the headlines. Of the 15 goals revealed so far, Thierry Henry has three while Dennis Bergkamp has four. You can visit the GGG50 homepage to see which other players have made the list. Do you agree with the selections so far? Let us know by visiting www.arsenal.com/studio … MORE >>
Your Chance to Star in an Arsenal O2 Advert… Calling all gunners. As sponsors of Arsenal, O2 like to give fans a bit extra. As part of next seasons campaign, O2 are giving you the chance to star in their new Arsenal O2 ad. You will be the face of Arsenal fans and appear throughout the season at Emirates Stadium. Click here for the chance to win a place and represent the loyal Arsenal fans. … MORE >>
Season Review 2008/09 DVD… Re-Live all the key moments of the Season 08/09 with highlights from every game and every goal scored in the Uefa Champions League,Barclays Premier League,FA Cup and the Carling Cup. This DVD is the definitive record of Arsenal's 08/09 season … MORE >>

The NEW Arsenal away kit - Wear yours first!… Arsenal Football Club has revealed its new away kit for the 2009/2010 season. The kit goes on sale from Thursday 25th June. Click here to pre-order yours now! … MORE >>
Visit Arsenal.com >

GIRRAFE OCEAN VIEW HOTEL YADHAMINI MISS VYUO VIKUU!!


Hoteli ya kitalii ya Girrafe Ocean View iliyoko ufukweni mwa bahari ya hindi maeneo ya Mbezi Beach imeingia katika kudhamini shindano la Miss Vyuo vikuu linalotarajiwa kufanyika mwezi ujao, Hoteli hiyo imetoa Malazi na chakula kwa muda wa wiki moja kwa warembo 15 wanaoshiriki shindano hilo wakati watakapopiga kambi ya wiki moja kabla ya shindano julai 3 mwaka huu kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es alaam.

Warembo watakuwa wakifanya wakilala na kufanya mazoezi hotelini hapo huku usafiri ukitolewa na wadhamini wengine Aurora Security kwa muda wote watakapokuwa kambini kwa ajili ya kujiandaa na kinyang'anyiro hicho kinachotarajiwa kuwa kikali kutokana na viwango vya warembo kutoka vyuo mbalimbali nchini wanaoshiriki shindano hilo mwaka huu linaloandaliwa na Manka Mushi Promotion

Kanda ya Vyuo vikuu mwaka jana ilitoa mshindi wa tatu kwenye shindano la Miss Tanzania Hivyo Manka Mushi Promotion imejiandaa kuhakikisha heshima hiyo inaongezeka kwa kutoa Miss Vodacom Tanzania Mwaka huu na hilo linawezekana kutokana na kazi kubwa ya kutafuta warembo wenye viwango iliyofanywa na mkurugenzi Manka Mushi

Warembo kutoka vyuo 8 ambavyo ni UD, TSJ, IFM,SOCIAL WORK, CBE na JK Kigamboni. ni veronica Mick, Ester Gao, Francisca Mansilo, Magreth Beatus, Mary Thomas, Subira Wahure, Doris Deonatus, Selestine Will Elimina majina ya warembo wengine yatatajwa baadae kwani wanaendelea kumalizia mitihani yao kwa muda mfupi uliobaki.

Mazoezi yalianza Juni 15 katika ukumbi wa Billcanas. Warembo wako chini ya mwalimu wao Miss Tanzania namba 3, ambaye pia alikua Miss Higherlearning mwaka jana, Pendo Laizer Bendi maarufu ya African Stars Twanga Pepeta itaporomosha burudani la kukata na shoka siku hiyo kwa mtindo wao wa kusugua kisigino,
Onyesho hilo linadhaminiwa na makampuni ya
Vodacom,TDL – Overmeer, Ben Expedition Tours, Air Tanzania, Ndege Insurance Co, Tesco Furniture, Clouds FM kupitia leo tena, Perfect Solutions, Global Publishers, Billcanas, Rozella Saloon, Fullshanwe.blogspot.com, City Stars Boutique, Dollwood,Varley Spring, Hattman Production, Zizzou Fashion,Aurora Security na kampuni ya kubuni mavazi ya Carpuany Design



Mustafa Hassanali Collection At ARISE AFRICA FASHION WEEK





Mustafa Hassanali launched his Prêt a Porter Spring/Summer 2009/10 Collection “Mduara” on 14 June at the Arise Africa Fashion Week.
The collection has been inspired by the sacred, savoury, significance, Sensual, soulful, synergetic Rhythms of our Swahili nation

Mustafa Believes “The Vibrancy of our Music, Culture, myths and Believes form an integral part of our being hence “Mduara” The Local Dance Rhythms which has Inspired this ready to wear Women Collection which is An eclectic mix of Tradition meeting Modernity and Vice versa”

WAFANAKAZI WA VODACOM KITENGO CHA CORPORATE SOLUTIONS WALA MSOSI NA WATOTO YATIMA!!

Wafanyakazi wa mbalimbali wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kitengo cha Corporate solutions wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wa kituo cha kulelea watoto yatima Chakuwama kilichoko Sinza jijin Dar es alaam jana katika kusherekea siku ya mtoto wa Africa wafanyakzi hao pamoja na watoto walikula cha mchakula kwa pamoja na kubadilishana mawazo mbalimbali na watoto hao.
Watoto wakila chakula cha mchana kilichoandaliwa na wafanyakazi wa Vodacom kitengo cha Corporate Solutions jana katika kituo cha kulelea watoto yatima Chakuwama katika kusherekea siku ya mtoto wa Afrika.

Mdau wa blog ya Mactemba.blogspot.com Edwin Mac Temba ambaye pia ni mfanyakazi wa Vodacom akiwa na watoto wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Chakuwama kilichopo Sinza jana hii ilikuwa ni kusherekea siku ya mtoto wa Africa.

WATOTO YATIMA WA TANZANIA MITINDO HAUSE WASHEREKEA SIKU YA MTOTO WA AFRICA!!

Mkurugenzio wa kituo cha kulelea watoto yatima na wenye mazingira magumu Tanzania Mitindo House ambaye pia ni mbunifu maarufu wa mavazi hapa nchini Khadija Mwanamboka akiwa na watoto hao pamoja na wageni kutoka Canada Katie na Kleey waliohudhuria sherehe hizo kituoni hapo jana kwa ajili ya kushiiriki na watoto katika kituo hicho.
Watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Tanzania Mitindo House wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Africa kwenye kituo hicho jana siku hii huadhimishwa kila mwaka juni 16.

Mwanamuziki mwalikwa Buti Jiwe alikuwapo jukwaani katika onyesho la masala Festival!!

Mr.Buti Jiwe mwenye kitambaa kichwani na Christian Bakotessa aka Chris-B.Mcharaza solo machachari.
Mr.Buti Jiwe aka Galinoma Jr,
Mwana Muziki wa Kizazi kipya cha mziki wa dansi,alikuwa msanii mwalikwa wa Ngoma Africa katika Onyesho la Masala Festival,kama unavyomuona jukwaani akienda sambamba na ndugu zake Ngoma Africa! Onyesho hilo lilifunikwa na mzuka wa muziki wa dansi wa Tanzania!
Bendi ya Ngoma Africa ilikuwa na lengo moja tu kuwadatisha washabiki wake! na kuhakikisha kuwa muziki wa bongo unachukua nafasi ya mwanzo bila ya kuwa na mpinzani katika anga za kimataifa.
Buti Jiwe anafanyia shughuli zake nchini Uholanzi anapatikana
butijiwe@yahoo.com

MISS SINZA KUPATIKANA JUNI 19 VATCAN SINZA!!


Hawa ndiyo warembo watakaoshiriki kwenye shindano la kumsaka mrembo wa kitongoji cha Sinza linalotarajiwa kuafanyika juni 19 kwenye ukumbi wa Vatcan Sinza Burudani ikiletwa kenu na kundi zima la Fm Academia watoto wa mujini na kundi la mfalme Siboka Chocolate .
mshindi wa shindano hilo atanyakua kitia cha shilingi 500.000 wa pili 300.000 watatu200.000 na washindi wa nne na wa tano watajipatia shilingi 150.00 kila mmoja huku wengine wakiondoka na kifutajasho cha 100.000 kila mmoja.
Warembo wanaoshiriki katika shindano hilo ni Lilian Komba, Salma Said, Beatrice Shayo, Rahma Faiz, Beatrice Shirima, Lulu Ibrahim, Aminatha Omar, Evastansia Temba, Dedensia Dawsony, Jane Wilson na Nazia Gabriel na kiingilio kitakuwa shilingi 15.000 na 5000.
Wadhamini wa shindano hilo ni Vodacom, Redds ,Vuvuzel. Old Kent Pub, Vanne Fashion, Sonda Communications, Break Point Bar, Habari Cooparations Zizzou Fashions na Clouds Fm

Ngoma Africa wawasha moto mkali! Masala Festival Hannover!!

The Ngoma Africa wakiwasha moto Jijini Hannover Ujerumani hivi karibuni.

Hannover palikuwa hapatoshi! Ras makunja Na kikosi chake cha kutuliza ghasia Ngoma Africa band a.k.a FFU a.k.a wazee wa kukaanga mbuyu! siku ya jumapili 14-06-2009 jioni mzimu wa muziki wao wa dansi la bongo, ulifanikiwa kuziteka nyoyo za mashabiki katika maonyesho makubwa ya muziki ya kimataifa Masala World Beat Festival,mjini Hannover,Ujerumani.

Majira ya saa 12 jioni Ras Makunja a.k.a "Bw.Kichwa Ngumu" alikiongoza jukwaani Kikosi cha The Ngoma Africa band, kilichokuwa kimesheheni wanamziki washambuliaji akiwamo yule mchawi wa solo Christian Bakotessa a.k.a Chris-B, Pia kulikuwa na mwanamziki mgeni mwalikwa Mr.Buti Jiwe ambaye alikuwa (Guest Artist),wengine alikuwapo yule mwadada anayekwenda sambamba na wanamuziki wa kiume katika kushambulia jukwaa Dada Severn Onkomo aka Sevasha.
Kiongozi wa bendi hiyo Ebrahim Makunja a.k.a ras makunja alikiamrisha kikosi chake nacho bila kurembaremba kilijibu mashambulizi kwa kuporomosha muziki mkali ambao midundo yao ya bongo dansi aliwazidi nguvu mashabiki na dakika chache wakaanza kudatishwa kama si kudata ! na kujikuta wapo katika Kindumbwe Ndumbwe cha Kuitikia kwa sauti kila walipoamrishwa na Ras Makunja!
Wataalamu wa mziki na maporomota walikuwa roho juu kila mmoja akiwa anataka kufanya kazi na bendi hiyo ambayo imetajwa kuwa ni moja ya bendi za Africa Mahiri sana kwa sasa katika nchi za Ulaya, watayarishaji wa onyesho hilo wamesema haijawihi kutokea katika historia ya maonyesho hayo kwa "Mziki wa dansi wa kiafrika" kuwadatisha mashabiki kwa kiwango kubwa kiasi kile! wamesema muziki wa The Ngoma Africa Band una nguvu isiyo ya kawaida! labda kutokana na midundo yake na jinsi wanamuziki wanavyojua kushambulia jukwaa kupanga vyema sauti, vyombo na jinsi wanavyocheza na kuwafanya mashabiki wasiweze kulala!
Bendi hiyo maarufu kwa tabia za kuwatia kiwewe washabiki wake huko ulaya kwa kutumia muziki wa dansi wa Tanzania,
Bendi hiyo imejikuta ina nafasi ya pekee katika ushindani wa muziki wa kimataifa.
Kwa sasa The Ngoma Africa inachukuliwa kama Klabu inayowaunganisha maelfu ya mashabiki kimataifa, kiongozi wa bendi hiyo Ras Makunja alikaliliwa akisema kuwa misheni na mtazamo wa Ngoma Africa band,kwa sasa si kuutangaza muziki wa dansi wa bongo tu,bali pia kuhakikisha wanamuziki wa bongo dansi wanapata nafasi ya kimataifa kwa kupitia bendi ya The Ngoma Africa,kamanda huyo wa The Ngoma Africa band.
Bendi hiyo ipo katika medani ya dansi kwa muda wa miaka 16, na imefanikiwa kulitangaza dansi la bongo na kujinyakulia nafasi ya pekee kimataifa.
wasikilize hapa www.myspace.com/thengomaafrica pia ukiwataka wasiliana nao kwa: http://de.mc588.mail.yahoo.com/mc/compose?to=ngoma4u@ngomaafrica