Showing posts with label BUSINESS. Show all posts
Showing posts with label BUSINESS. Show all posts

Mikoko ya Vodacom kukuza uchumi kwa washindi!!


Baadhi ya washindi wa magari ya Hyundai i10 yanayotolewa na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kupitia promosheni yake ya ‘Shinda Mkoko’ wamesema zawadi hiyo itawasaidia kukuza uchumi wao kwani itarahisisha usafiri katika shughuli zao.


Akizungumza kwa njia ya mahojiano kutokea Dodoma baada ya kuibuka mmoja wa washindi wa promosheni hiyo, Tolino Pechaga ambaye ni fundi umeme wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) alisema anatumaini gari hilo litakamilisha ndoto yake ya kimaisha katika kujiletea maendeleo.


Akifafanua alisema, ingawa alikuwa akitumia magari ya wafanyakazi kutoka Maili mbili anakoishi hadi Udom, ujio wa Hyundai i10 utamaliza muda wa kukimbizana na basi hilo na kumpa nafasi ya kufanya kazi zake binafsi baada ya muda wa kazi kwa mwajiri wake.


“Unajua mimi ni mwajiriwa wa chuo, lakini nafanya pia kazi zangu binafsi. Usafiri ulikuwa kikwazo namba moja kufikia malengo yangu, lakini sasa kila kitu kitaenda sawa kwani tayari nitakuwa na usafiri wangu binafsi utakaorahisisha maendeleo yangu,” alisema Pechaga.


Kwa upande wake Benard Asenga wa Keko Magurumbasi jijini ambaye ni mfanyabiashara wa duka la bidhaa ndogondogo na vyakula alisema alikuwa akitumia muda mwingi na baiskeli kufuata bidhaa sokoni Kariakoo, lakini gari hilo litamuwezesha kuboresha utoaji huduma kwa wateja wake.



Aidha Asenga alifafanua kwamba mara baada ya kukabidhiwa Hundai i10 aliyojishindia atabadilisha mtindo wa biashara anaoufanya na anafikiria kuwa mjasiriamali wa kati (SME’s) na kumiliki duka la bidhaa za jumla na rejareja.


“Sasa sitatumia tena baiskeli kufuata bidhaa mjini, nafikiria kukuza biashara yangu kutoka hatua moja kwenda nyingine jambo litakaloniwezesha kukuza hali yangu kiuchumi,” alisema mfanyabiashara huyo.


Naye Simon Kihuru ambaye ni dereva wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songea alisema zawadi hiyo iliyotolewa na Vodacom Tanzania itampunguzia gharama za usafiri kwa ajili kuwapeleka na kuwarudisha watoto wake shule kwani wataweza kutumia gari hiyo kwa matumizi ya binafsi.



“Kama nilivyosoma kwenye magazeti mbalimbali kwamba gari hiyo haitumii gharama kubwa kuihudumia, kwa kuwa mimi ni dereva itaniwezesha kutunza fedha zangu baada ya kukwepa huduma za daladala ambazo sio salama sana hususani kwa watoto,” alisema Kihuru.



Akizungumza hivi karibuni kwenye hafla ya uzinduzi wa promosheni ya ‘Shinda Mkoko’ iliyopanga kuwazawadia wateja wake gari moja aina ya Hyundai i10 kila siku Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru alisema shindano hilo litawahusisha wateja wote wa kampuni hiyo nchini na kwamba ndani ya siku 100 kila siku mtu atakuwa anajipatia gari moja.

Precision Air yaleta ndege mpya!!


Na Mwandishi Wetu


SHIRIKA la Ndege la Precision linalotoa huduma bora Tanzania, limetangaza kuleta ndege yake mpya ya sita aina ya ATR42-500 itakayowasili Agosti 26 mwaka huu kutoka Toulouse, Ufaransa, ikiwa ni sehemu ya kutekeleza programu ya kutoa huduma za kisasa zaidi. Mkurugenzi Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Precision Air, Alfonse Kioko, aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa, ndege hiyo mpya itakayopachikwa jina la Bukoba, itafuatiwa na nyingine ya saba itakayoingia Septemba 15 mwaka huu.



Mwaka 2006, Precision na ATR ya Ufaransa walisaini mkataba wa dola za Marekani milioni 129 ili kutoa ndege saba mpya. Ndege ya kwanza kati ya hizo iliwasili Machi 2008. Tangu wakati huo, Precision imepokea ndege tano aina ya ATR 72-500 na kufanya iwe na ndege tano mpya mpaka sasa. Pia ina ndege nyingine tatu za zamani. Kioko alisema baada ya ndege hiyo yenye namba 5H-PWF kuwasili, wataizindua Dar es Salaam Agosti 27.




Alisema ina vifaa vya kisasa vya burudani kwa ajili ya wasafiri kuangalia sinema na kusikiliza muziki wakiwa safarini. Ndege hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 70. Mkurugenzi huyo pia alitangaza kwamba tangu kuanza mwaka mpya wa fedha, idadi ya abiria wapya imeongezeka kwa asilimia 12 kulinganisha na mwaka jana. Pia mizigo ya biashara imeongezeka licha ya kudorora kwa uchumi duniani.




Akizungumza katika mkutano huo, Meneja Masoko wa Precision, Emillian Rwejuna alisema kampuni hiyo inatarajia kupata ndege ya Boeing 737, kati ya Oktoba na Novemba mwaka huu. Rwejuna alisema kupatikana kwa ndege hiyo kutapanua wigo wa huduma za safari.




Ndege hiyo ya tatu aina ya Boeing 737 itaboresha safari za Johannesburg, Afrika Kusini, na pia katika miji ya Kinshasa na Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Precision Air hivi sasa inafanya safari katika miji ya Dar es Salaam, Mwanza, Tabora, Musoma, Shinyanga, Kigoma, Kilimanjaro, Zanzibar, Mtwara na Arusha. Pia ina safari za Nairobi na Mombasa, Kenya na Entebbe, Uganda.

Ushirikiano kati ya Tanzania na China katika Uchapishaji

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu wa Bunge) Phillip Marmo (kulia) akikabidhi zawadi ya mkoba wa ngozi leo jijini kwa Naibu Wazir i, Utawala wa Habari na Uchapishaji kutoka Jamhuri ya Serikali ya watu wa China LI DONGDONG(kushoto) Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera ,Uratibu wa Bunge)Phillip Marmo (kulia) leo katika Ukumbi wa Mikutano katika ofisi ya Waziri Mkuu, amemkabidhi zawadi ya ngozi ya Pundamilia kwa Naibu Waziri,Utawala wa Habari na Uchapishaji wa kutoka Jamhuri ya Serikali ya watu wa China LI DONGDONG baada ya mazungumzo ya kiserikali yanayohusu mambo ya Uchapishaji. Mazungumzo hayo yamewahusisha watendaji wakuu wenyedhamana katika Wizara ya Habari pamoja na Uchapishaji kutoka Tanzania Bara na Visiwani wakishirikiana na Ujumbe kutoka China.Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO.

Hapa wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano huo leo.

Tanzania yakopeshwa bilioni 173.8 na Korea


Habari na picha Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salam.



Jamhuri ya Korea imetiliana saini na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya kuikopesha shilingi bilioni 173.8 ( Dola la Kimarekani milioni 124) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mitatu ya maendeleo hapa nchini.




Sherehe hizo zilifanyika jana jijini Dar es salaam na kuwakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhan Khijjah kwa niaba ya Tanzania na Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Mheshimiwa Young-hoon Kim. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Khijjah, fedha hizo zitasaidia ujenzi wa upanuzi wa Chuo Kikuu cha Tiba na Afya Muhimbili(MUHAS) katika eneo la Mloganzila, usambazaji wa umeme katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro na usambazaji wa maji katika Manispaa ya Dodoma.





Alisema kuwa katika mradi wa maji katika Manispaa ya Dodoma utagharimu shilingi bilioni 69.5 na utahusisha ujenzi wa vyanzo vya maji , ukarabati wa matenki ya kuhifadhia maji na ujenzi wa matenki mapya. Khijjah alisema kuwa kwa upande wa upanuzi wa MUHAS jumla ya shilingi bilioni 69.3 zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa kufundishia na eneo la kutolewa matibabu.




Pia mkataba huo unalenga kusaidia kuboresha huduma ya umeme katika baadhi ya eneo la mkoa wa Kilimanjaro na Arusha ambapo mradi huo utagharmu shilingi bilioni 35.




Aliongeza kuwa Dola milioni 18 zitasaidia vituo vya ufundi stadi katika katika mikoa ya Dar es aalaam , Pwani, Lindi na Manyara na Dola milioni 25 zitasaidia ujenzi wa daraja la Maragarasi.

HYUNDAI YAKABIDHI RASMI MAGARI YA "SHINDA MKOKO" KWA VODACOM TANZANIA

Mwenyekiti wa Kampuni ya magari ya Hyundai East Africa Ltd, Gulam Hussein Karmali (kulia) akimkabidhi rasmi mfano wa funguo wa magari 100 kwa ajili ya wateja wa Vodacom kujishindia a katika Promosheni ya "SHINDA MKOKO" Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa Mahusiano ya Wateja(Executive Customer Relationship Management)wa Vodacom Tanzania Aika Makindara Matiku,katikati Mkurugenzi mtendaji wa Hyundai East Africa Ltd,Mohamed Karmali.
Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa Mahusiano ya Wateja(Executive Customer Relationship Management)wa Vodacom Tanzania Aika Makindara Matiku akiongea na waandishi wa habari wakati wa kukabidhiawa rasmi magari 100 kwa ajili ya wateja wa Vodacom kujishindia katika Promosheni ya "SHINDA MKOKO"(kulia) Mwenyekiti wa Kampuni ya magari ya Hyundai East Africa Ltd, Gulam Hussein Karmali.
Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa Mahusiano ya Wateja(Executive Customer Relationship Management)wa Vodacom Tanzania Aika Makindara Matiku akilijaribu moja kati ya magari 100 aliyokabidhiwa rasmi leo kwa ajili ya wateja wa Vodacom kujishindia katika Promosheni ya "SHINDA MKOKO ".


Serengeti kutoa kinywaji bure watu wa kwanza ndani ya fiesta jipanguse 2010

Kampuni ya bia ya Serengeti imetamka rasmi leo asubuhi kupitia kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa na Clouds FM 88.4, kuwa itatoa vinywaji vyake bure kwa watu wa kwanza watakowahi kuingia kwenye tamasha la Fiesta Jipanguse 2010,linalofanyika ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijin Dar .


Meneja Mkuu wa Uhusiano, mawasiliano na Jamii wa kampuni ya Bia ya Serengeti ,Teddy Mapunda (pichani kushoto) ameweka hilo bayana ndani ya kipindi hicho leo asubuhi kuwa ,watu watakaofika ndani ya tamasha hilo kabla ya saa 12 jioni watapewa bia moja ya bure,na watakaofaidika zaidi ni wale wenye umri zaidi ya 18.

Teddy amesema kuwa kutokana na Familia ya kampuni yhiyo kuwa kubwa,washabiki na wapenzi wake watakuwa na uhuru wa kuchagua bia waitakayo,kwani zitatolewa bia za aina tatu,yaani bia ya Uhuru,Tusker pamoja na Serengeti a.k.a Mfalme wa raha kamili.


Kampuni ya bia ya Serengeti ndio mdhamini mkuu wa tamasha la Fiesta Jipanguse 2010 ,ambapo mpaka sasa tamasha hilo limekwishafanyika mikoa ipatayo nane na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa,mikoa hiyo ni kama vile Morogoro,Arusha,Moshi,Dodoma,Tanga,Zanzibar,Musoma pamoja na Mwanza,na sasa ni zamu ya wakazi wa jiji la Dar ambao siku ya jumamosi watajipangusa vilivyo kwa burudani mbalimbali zitakazotolewa na wasanii wa hapa nyumbani na wa Kimataifa.

Kampuni ya Gold Star yachezesha droo!!


Benjamin Sawe Maelezo Dar es Salaam.


Kampuni ya Gold Star leo imetangaza washindi 35 walioshindana katika bahati nasibu ya jipatie mapesa na Gold Star iliyoanza miezi miwili iliyopita wakati wa kipindi cha mashindano ya soka ya kombe la dunia.


Akiongea na wanahabari jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bwana Kulathu Srinivasan amesema lengo la mashindano hayo ni kuhamasisha wananchi wapende michezo kwa ujumla..


Katika shindano hilo ambapo washindi walitambulika kwa namba, washindi 5 wa kwanza walipata kitita cha shilingi milioni 1 kila mmoja na washindi 10 walipata kitita cha shilingi laki 5 ambapo washindi 20 waliobakia walipata shilingi laki mbili na nusu kila mmoja. Alitaja lengo lingine ni pamoja na kuhamasisha watumiaji wa bidhaa za kampuni ya Gold Star kupenda michezo kwa kuangalia Kombe la dunia na kulipa moyo bara la Afrika kwa kuandaa michuano ya kombe la dunia.


“Tumefanya bahati nasibu hii ili kuwaweka pamoja wateja wetu wanaotumia rangi ya bidhaa zetu za kampuni ya Gold Star na kulipongeza Bara la Afrika kwa kupata nafasi ya kipekee ya kuandaa Kombe la dunia”.Alisema Bwana Srinivan.



Shindano hilo lilishirikisha jumla ya washiriki 35 lilianza wakati wa kipindi cha mashindano ya dunia ya mpira wa miguu na lilikuwa na lengo la kuhamasisha watanzania kuwa na utamaduni wa kupenda michezo.

VODACOM TANZANIA YAZINDUA PROMOSHENI YA "SHINDA MKOKO" KWA KUTOA MAGARI 100

Mkurugenzi wa masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru akiongea na wageni mbalimbali wakati wa uzinduzi wa promosheni ya "Shinda Mkoko" ambapo Vodacom imetoa magari 100 aina ya Hyundai i10 ambayo yatashindaniwa na wateja wa vodacom huku mshindi akipatikana kila siku kwa siku 100. kwa kutuma msg iliyoandikwa Mkoko kwenda namba 15544 na kujibu maswali utakayoulizwa, kila meseji itachajiwa shilingi 550 hafla hiyo imefanyika leo kwenye viwanja vya Mlimani City jijini Dar es salaam.
Katika picha kutoka kushoto ni Dylan Lennox Mkugenzi wa Tekinolojia Mpya ya Vodacom Tanzania wa pili Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Francois Swart na kulia ni Aika Makindara Matiku Mkuu wa Mawasiliano kwa wateja.
Kaimu Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Francois Swart na Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald wakizindua rasmi magari yaliyotolewa na Kampuni hiyo kwa ajili ya Promosheni ya Shinda Mkoko kwa wateja wake, jumla ya magari 100 yatashindaniwa kwa siku miao moja huku kila siku mshindi wa gari moja akipatikana kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacoma Tanzania Ephraim Mafuru na kulia ni Aika Makindara Matiku Mkuu wa Mawasiliano kwa wateja.

Viongozi mbalimbali wa kampuni hiyo katika picha na magari hayo kwenye viwanja vya maegesha mlimani City leo

Wakuu wa Vodacom Tanzania wakiwa aktika picha ya pamoja tayari kwa kuzindua promosheni ya Shinda Mkoko leo katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar es salaam.