Showing posts with label FASHION. Show all posts
Showing posts with label FASHION. Show all posts

VODACOM MISS TANZANIA KUPIGA KAMBI AGOSTI 16th…!!!


MKURUGENZI wa Kampuni ya Lino International Agency , ambaye pia ni Mratibu wa shindano la Vodacom Miss Tanzania Hashim Lundenga leo ametangaza majina ya warembo 31 watakaoingia kambini Agosti 16 mwaka huu.




Lundenga ilitaja majina ya washiriki na maeneo wanayowakilisha katika mabano ni hawa wafuatao Ester Dennis na Gloria (UDSM),Shadia Mohammed, Furaha David na Mary Kagali (Nyanda za Juu Kusini).




Wengine ni Bahati Chando, Salma Mwakalukwa na Consolata Lukosi (Kanda ya Kati),Flora Florence, Mary Adam na Angelina Ndege (Kanda ya Mashariki), Alice Lushiku, Irene Hezron na Amisuu Malick (Kanda ya Kinondoni), Genevive Emmanuel, Anna Daudi na Britney Urassa (Kanda ya Temeke), Glory Mwanga, Prisca Mkonyi na Jally Murei (Kanda ya Kaskazini).
Wengine ni Gloria Mosha na Christine Justine (Kanda ya Chuo Kikuu Huria), Flora Martin, RachelSindbad na PendoSam (Kanda ya Elimu ya Juu), Fatma Ibrahim, Buduri Ibrahim na Margareth Godson (Kanda ya Ziwa).




Taarifa hiyo ilisema kuwa warembo wote wanatakiwa kuripoti Agosti 16 saa tatu asubuhi katika ofisi za Kamati ya Miss Tanzania zilizopo mtaa wa Samora na Mkwepu baadaye watapelekwa katika hoteli ya Giraffe iliyopo Jangwani beach ambako ndipo itakuwa kambi yao.





Aidha washiriki wote wametakiwa kufika katika muda uliopangwa na si vinginevyo, mshiriki atakayechelewa kufika bila ya kutoa taarifa atakuwa amejitoa katika fainali hizo.
Wakiwa kambini washiriki hao watapata mafunzo mbalimbali kutoka kwa wakufunzi walioandaliwa pamoja na wataalamu wa nyanja tofautitofauti.

Fatma Ibrahim ndiye Vodacom Miss lake Zone 2010!!

Vodacom Miss lake Zone 2010 Fatma Ibrahim kutoka Mara akitabasamu baada ya kutawazwa kuwa malkia wa taji hilo, kushoto ni mshindi wa pili Buduli Ibrahim kutoka Shinyanga, Kulia ni Margreth Godson mshindi wa tatu kutoka Shinyanga. Shindano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Natiro Annex Capripoint jijini Mwanza.

BINTI AFRICA YATIA FORA MAONYESHO YA MAVAZI YA TINGATINGA MAKUMBUSHO!!


Mmiliki wa kampuni mpya ya mavazi Binti Africa iliyopo Kionondoni B na mbunifu wa mavazi ya kiafrika akiwa katika picha ya pamoja na wanamitindo wake mara baada ya kupita na mavazi yake aliyoyabuni ambayo aliyaonyesha katika uzinduzi wa onyesho la mavazi ya kiafrika ya TINGATINGA katika onyesho lililofanyika mwishoni mwa wiki kwenye kijiji cha Makubusho jijini Dar es salaam na kushirikisha wabunifu mbalimbali, kulia ni mwanamitindo Zawadi na kushoto ni mwanamitindo Eva.


Watu waliohudhuria walipata fursa ya kujionea ubunifu wa mavazi tofauti ya Afrika pamoja na sanaa ya uchoraji katika nguo ya TINGATINGA kwenye onyesho hilo lililoandaliwa na kampuni ya Sophy Entarteinment ya jijini huku burudani ikitolewa na bendi ya FM Academia ya jijini Dar es salaam katika onyesho hilo.

Mwanamitindo Eva na Kivazi ha kutokea.
Gauni refu lililochorwa maua mbele na nyuma.
Kivazi kingine cha kutokea.

Mwanamitindo Mouddy akionyesha vazi safi linalofaa kwa nyakati mbalimbali


Mwanamitindo Zawadi akipita na vazi murua la kutokea jioni.

REDDS YAWAPONGEZA WAREMBO WATAKAOINGIA KAMBI YA VODACOM MISS TANZANIA 2010!!

Hawa ni vimwana kutoka kanda ya Temeke ambayo mwaka huu inaonekana kutishia kanda zingine katika shindano la Vodacom Miss Tanzania kutokana na warembo wake kuwa katika viwango vinavyostahili katika mashindano hayo ya Vodacom Miss Tanzania hapa wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kupita mbele ya wageni waalikwa kwenye hafla ya kuwapongeza warembo waliofanikiwa kutinga kwenye kambi ya Vodacom Miss Tanzania ambayo itaaza hini karibuni jijini Dar es salaam.
Hafla hiyo ya kuwapongeza warembo hao iliandaliwa na kampuni ya bia ya Tanzania TBL kupitia kinywaji chake cha Redds ambao ni wadhamini wakuu wa kanda tatu za Temeke, Ilala na Kinondoni, hafla hiyo imefanyika usiku wa kuamkia leo kwenye hoteli ya Movenpick jijini Dar es salaam ikikutanisha wadau mbalimbali wa urembo nchini.
Afisa uhusiano wa Kamati ya Miss Tanzania Aidan Rico amesema kwa njia ya simu kwamba kamati hiyo inatarajia kutangaza mbele ya wanahabari kuhusu kuanza kwam kambi hiyo siku ya jumanne ambapo kila kitu kitawekwa waazi kuhusu maandalizi ya Vodacom Miss Tanzania mwaka huu.
Hawa ni Vimwana kutoka Miss Kinondoni wakipozi kwa picha mara baada ya kupita mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo iliyoandaliwa ka wadhamini wa kuu wa kanda hizo Redds Premium Cold.
Mdau Edwin Temba wa pili kutoka kushoto na maiwaifu wake wa mwisho kushoto wakijadili jambo kuhusu zawadi katika hafla hiyo, ambapo mrembo mwenye nidhamu kutoka Miss Ilala alipewa zawadi ya Luninga nchi 18 zawadi iliyotolewa na wakuu wa kamati ya Miss Ilala.
Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa CM.CM. LTD Charles Mtawali, Mkurugenzi wa Fabac Fashion Aisa Idarous na Muddy Mass wakijadiliana jambo katika hafla hiyo.

Kutoka kulia ni Charels Mtawali Mkurugenzi wa Kampuni ya kuuza magari ya CM CM. LTD "Rais wa Magari" akipozi kwa picha na mfanayabiashara Muddy Mass pamoja na Gabriel Baluawa Team Freght Limited.
Vimwana wa Miss Temeke wakiwa katika hafla hiyo hapa wakipiga picha na mratibu wa Miss Chang'ombe Tom Chilala.
Tume Makani na Ronald Shelukindo wakizungumza mawili matatu katika hfla hiyo iliyofanyika kweye hoteli ya Movenpick.
Elsi Mgimba kulia na Amanda wakila stori katika hafla ya kuwapongeza warembo wanaoingia kambini kujiandaa na shindano la Vodacom Miss Tanzania kwenye hoteli ya Movenpick usiku wa kuamkia leo.

Twiga Stars beat The Northwest Nationals FC 2-0!!

Tonight Tanzania's National Women's Football team, the Twiga Stars, took on the Northwest National Reds U-18 in a friendly match at the Starfire Sports Complex south of Seattle, Washington, USA.


Despite having traveled for almost two full days, spending 28 hours on planes and arriving only the night before, the Twiga Stars beat their American opponents 2-0, with goals by Eto Mlenzi and Esther "Lunyamila" Chabruma.


The Northwest Nationals are one of the top youth soccer clubs in Washington State, and many of their players each season go on to earn soccer scholarships at top universities.
The Twiga Stars are currently on their USA training trip sponsored by Ms. Rahma Al-Kharoosi, president of RBP Oil & Industrial Technology Ltd.


While in the USA, the Twiga Stars will be playing a number of matches, including a special showcase match on August 7 against the Seattle Sounders Women's Team, who play in the USL W-League, the second tier of USA women's soccer. The aim of the trip is to gain experience before the African Women's Championship to be held in South Africa this October.


The Twiga Stars qualified for the continental finals by beating Ethiopia 4-2 on aggregate, then beating Eritrea 11-3 on aggregate.
http://www.twigastars.com/




MISS TANZANIA WAFANYA HAFLA YA KUWATAMBULISHA MUZASHA TOURS AND SAFARIS KAMA WADHAMINI WAPYA!!

Mkurugenzi wa Muzasha Tours and Safaris Bw. Muzamil Issa Katunzi wa pili kutoka kushoto akiwa na marafiki zake katika hafla ya kutambulisha hiyo kama wadhamini wenza wa Vodacom Miss Tanzania ambayo imedhamini mashindano hayo kwa shilingi milioni 61.
Katika picha kutoka kulia ni Benedict Mulokozi Mkurugenzi, Bw. Charles Mtawali Mkurugenzi wa CM. CO. LTD na mwisho kushoto ni Kulwa Katuzi, Hafla hiyo inayoendelea sasa hivi inafanyika kwenye hoteli ya Regency Park Mikocheni jijini Dar es salaam, FULLSHANGWE tunawapongeza Muzasha kwa kudhamini Vodacom Miss Tanzania kwani kwa nafasi hii mtaweza kusaidia katika kukuza utalii wa ndani jambo ambalo limekuwa likipigiwa mbiu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Bodi ya ke ya Utalii TTB.
Wadau mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo na kuburudika vya kutosha.
Mama Elsi Mgimba katikati akiwa na marafiki zake Miss Domestic Tourism Sia Ndeskoi kulia na Amanda Chale wakiwa katika hafla hiyo.

Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga kulia akifurahia jambo na maafisa wa kamati hiyo katika hafla ya kuwatambulisha wadhamini wapya wa Vodacom Miss Tanzania Kampuni ya Muzasha Tours and Safaris ya jijini kwenye hoteli ya Regency Park jijini Dar es salaam inayoendelea usiku huu, wanaofuatia katika picha ni Mkuu wa Itifaki Albert Makoye, Afisa Uhusiano Hidan Ricco na Miss Domestic Tourism Sia Ndaskoi.

Mdau Cesilia kutoka Radio Uhuru akichati na wadau mbalimbali katika hafla hiyo kulia ni Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude.