Showing posts with label entertainment. Show all posts
Showing posts with label entertainment. Show all posts

EUROPEAN THRILLER – BAYERN VS REAL - LIVE ON SUPERSPORT!!


Two of the traditional giants of European football clash in a mouth-watering pre-season friendly as Bayern Munich host Real Madrid at the Allianz Arena on Friday, live on your World of Champions.



Bayern were double winners in Germany last season and got their new campaign off to the perfect start with a comfortable 2-0 success over Schalke in the DFB Supercup at the weekend. They are the team to beat in Germany this year, but coach Louis van Gaal will have some personal reasons to want a win in this one too.




He has previously had two spells in charge of Real’s archrivals Barcelona, and nothing would please him more than to sow the seeds of doubt in the Madrid team’s pre-season plans. Real coach Jose Mourinho has been working hard at putting his personal stamp on the Spanish side he joined in June from European champions Inter Milan.




Mourinho plotted the downfall of Bayern in the UEFA Champions League title-decider in May, and now has a quick return fixture against the side. Pre-season friendlies count for little in the greater scheme of things, but nobody wants to lose a high-profile fixture such as this one.




Pride is everything in European football and there will be no shortage of it out there at the Allianz Arena when these giants go toe-to-toe in Munich. DStv viewers can tune in for live coverage of the match on Friday August 13 (2155) on SS3, SS3A, SS3N and Maximo.

CLOUDS TV WAUNGANA NA MTV BASE

Usiku wa kuamkia leo, ndani ya ukumbi wa Much More uliopo katika jengo la Club Billicanas, umefanyika uzinduzi rasmi wa ushirikiano kati ya Clouds TV na televisheni ya Kimarekani MTV Base. katika ushirikiano huo, Clouds TV itakuwa ikirusha baadhi ya vipindi vya MTV Base kwa saa kadhaa kila siku jioni kuanzia saa 12. Pichani ni Mkurugenzi wa Clouds Entertainment Jose Kusaga (kulia) akitoa shukrani zake kwa MTV Base kupitia mwakilishi wao Mr. Paul

M-Net's Big Brother ALL STARS: Images from day 21 (Sunday August 8, 2010)

It’s day 21 on M-Net’s Big Brother All Stars --- and Lerato is evicted from the Big Brother All Stars into the Barn, to join Hannington and Sammi. Last night’s show also featured Malawian rising star Young Kay. Stay tuned to M-Net’s BIG BROTHER ALL STARS with 24/7 coverage on DStv channel 198 plus daily edited shows on M-Net and AfricaMagic. For more information on the series, log on to www.mnetafrica.com/bigbrother.

BIG BROTHER ALL STARS MUNYA OR TATIANA – AFRICA MUST DECIDE!


Zimbabwe’s Munya and Angola’s Tatiana are up for eviction this week after Monday night’s (9 August) nominations on M-Net’s Big Brother All Stars. Munya finds himself up for eviction for the second week in a row after Sheila saved herself and put him up for eviction in her place.




Head of House Sheila found herself up for eviction after receiving the bulk of nominations from her housemates, based on the fact that she could save herself. · Code nominated Yacob, because as he says "I can't trust him and I can't place him yet". His second nomination went to Sheila. ·



Jennifer nominated Uti and Meryl because she feels they have formed an alliance, which concerns her.



· Kaone nominated Sheila and Meryl – the former because she could save herself. · Meryl nominated Kaone because he "gets on my last nerve” and also because she feels he is judgmental. She also nominated Tatiana because she considers her to be strong competition but pointed out that "it has nothing to do with Lerato, I just don't want her around for too long".





· Munya kept his nominations going along the same lines he has stuck to every week – “strictly business”. He nominated Uti and Yacob, explaining "I'm starting from the top of Africa and moving down”. ·



Paloma nominated Sheila because she could save herself and Uti because she felt his jokes had gone overboard and he is hurting people “and this is getting out of hand”.




· Mwisho nominated Tatiana because he thought everyone would be thinking along the same lines after both her Head of House decisions had seen the people she replaced herself, with evicted from the house. He also named Kaone because "the game has shifted” - he feels he needs to pick a side and take a gamble and Kaone is not on the side he has picked.

Mzee wa "aladji aladji" kuwasha moto Bilicanas Club leo.



Baada ya kuzikonga nyoyo za wapenzi wa lile songi lililobamba sana hapa bongo la Alaji Alaji,ndani ya tamasha la Fiesta Jipanguse 2010 ndani ya viwanja vya Lidaz Club,kutoka kwa mwanamuziki wa Ivory Coast Jeff Bogolabang, leo usiku atalitikisa tena goma la alaji alaji ndani ya Bilicanas Club (Much More) kwenye uzinduzi wa Clouds Tv kujumuisha vipindi na muziki kutoka kituo cha MTV BASE.


Katika uzinduzi huo utakaokuwa na msisimko mkubwa kwa wadau wa mambo ya muziki na burudani ,utapambwa na wasanii wengine wa hapa nyumbani na pia kutoka kwa wale watani zetu wa jadi kutakuwepo na wale wakali wa kusugua sugua sahani CODERED DJ'S,ambao pia walifamya makamuzi ya kiaina ndani ya tamasha la Fiesta Jipanguse.


Aidha katika taarifa iliyotolewa na Clouds TV/MTV BASE,imeeleza kuwa kuanzia agasti 10 2010,watazamaji wa Clouds TV watapata nafasi ya kuburudishwa kwa masaa mawili ya vipindi vya muziki na mitindo ya maisha kutoka katika kituo cha televisheni cha Kimataifa,kinachorusha matangazo yake Afrika pekee cha MTV BASE.Burudani hiyo itarushwa hewani jumatatu hadi jumapili kati ya saa 12 jioni na saa 1 usiku,na vile vile kukiwa na mwendelezo wa burudani kati ya saa 4 na saa 5 usiku kwa siku za wiki.

BANTU NITE!!! FACE CLUB READING.

A BRAND NEW SEDUCTIVE & AFRO NITE LIKE NEVA BEFORE
BANTU NITE !!!!
SAT 28Th AUGUST 2010 BANK HOLIDAY W,KEND
COME & BANJUKA WITH FINEST DEEJAYS ON THE MIX
BONGODEEJAYS(TANZANIA) in collabo with TAMUSANA DJS(KENYA)
PLUS GUEST DEEJAYS
PLAYING THE BEST IN BONGO FLAVA -GENGE - ZOUK,LINGALA,NAIJA,KWAITO,R n B - HIP HOP,DANCE HALL & MANY MORE
venue -FACE CLUB
time 10PM-6AM
NO WORK ON MONDAY,SO DONT LET YOUR CURIOSITY TROUBLE YOUCOME AND JOIN US PARTY HARD TILL DAWN
For more info visit www.bongodeejays.blogspot.com

HIVI NDIYO VIJIMAMBO VYA FIESTA JIPANGUSE 2010 RRRRRRAH!!

Mdau Philip Seyayi wa JWT akitoa pozi la kupongeza tamasha la Fiesta Jipanguse 2010 huku akiwa ameshikilia glasi ya kinywaji chake cha "Mfalme wa raha kamili" wakati alipokuwa akijipangusa na fiesta kwenye viwanja vya Leaders usiku wa kuamkia leo jijini Dar es salaam. ilikuwa ni bonge la Shangwe kwa mashabiki waliohudhuria katika onesho hilo.
Wasanii wawili wakali Fid Q kushoto na Jo Makini "Mwamba wa Kaskazini"wakipozi kwa picha ya pamoja, ukiangalia hii picha ni kama kila mtu anapiga picha yake kwani haionyeshi kama wanashoo love lakini huku ndiyo kujipangusa na Fiesta kwenyewe.
B 12 mtangazaji wa Clouds kipindi cha XXL naye akajipendekea kwa warembo kiaina hebu mcheki hapa ili mradi kujipangusa tu.
Mdau Kajala na Barbara Hassan wakapozi kwa picha na vivazi vyao vilivyowakaa sawasawa.
Hawa walikuwa wamebanwa vilivyo katika vyuma vya uzio uliowekwa kutenganisha jukwaa na mashabiki kutokana na wingi wa watu waliohudhuria kwenye onesho hilo kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni usiku wa kumakia leo lakini hawakusikia maumivu zaidi ya shangwe za Fiesta Jipanguse "Rrrrah".

LIL KIM NA JUMA NATURE WAFANYA KWELI FIESTA JIPANGUSE LEADERS!!

Mwanamuziki Lil Kim kutoka Marekani akifanya mambo makubwa jukwaani usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la Fiesta Jipanguse ambapo aliwastua mashabiki pale alipomuita Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Bongofleva kutoka Nyumbani na kuimba wimbo wa Mugambo akishirikiana na mwanamuziki huyo,


Wanamuziki hao wakiwa jukwaani wamefanya onesho la kukata na shoka huku wakionyesha ushirikiano mkubwa katika uchezaji kitu kilichopelekea mashabiki kuwashangilia kwa nguvu kana kwamba wanamuziki hao wamezoeana kwa muda mrefu.


Awali mwanamuziki Lil Kim alipokuwa mazoezini katika viwanja hivyo mishale ya saa kumi na mbili alisikika akiulizia mwanamuziki wa numbani ambaye anafanya vizuri kimuziki wakati akiongea na mtangazaji wa Radio Clouds anayeitwa Ruebeny, ili kujibu swali hilo mtangazaji huyo alimwambia kuna mwanamuziki anaitwa Juma Nature ana nyimbo nyingi nzuri lakini ana wimbo wake unaitwa Mugambo wimbo huu ni maarufu na unapendwa sana hapa nyumbani.


Kwa maelezo hayo Lil Kim alikubali kuimba nyimbo hiyo na mwanamuziki Juma Nature kitu ambacho kimethibitisha uwezo wa mwanamuziki Juma Nature katika muziki wa kizazi kipya Bongofleva, Hongera Juma Nature umewakilisha Vyema Tanzania.
Lil Kim katika staili ya kihindi.
Sasa akapanda wanadada Lil Kim kutoka Marekani hapa akiwa pamoja na wanenguaji wake wakifanya mambo makubwa jukwaani.

Wanamuziki kutoka Nigeria awakifanya vitu vyao jukwaani, walikonga mioyo ya mashabiki kwa kiwango fulani.

Mwanamuziki Hamis mwinjuma aka Mwana FA akiwa jukwaani akichana mistari katika tamasha la Fiesta Jipanguse.

Mh. Temba wa kundi la TMK Family akiwa jukwaani pamoja.

Mwanamuziki Dully Sykes pamoja na wanenguaji wake wakifanya vitu vyao katika jukwaa la Fiesta Jipanguse usiku wa kuamkia leo.

Mashabiki wakinyanyua mikono yao juu.

Mashabiki mbalimbali wamehudhuria katika tamasha la Fiesta Jipanguse lililofanyika usiku wa kumakia leo kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni.

MWANAMUZIKI LIL KIM ATEMBELEA LEADERS NA KUJIONEA JUKWAA KABLA YA KUKATA KIU YA WABONGO!!

Mwanamuziki Lil Kim kutoka Marekani ambaye amewasili leo akiwa katika viwanja vya Leaders Kinondoni kwa ajili ya kujaribu vyombo kabla hajapanda jukwaani hapo baadae hapa akijadiliana jambo na wanamuziki wake alioongozana nao Lil Kim huenda akafanya kitu na mwanamuziki Juma Nature jukwaani hapo leo manake kuna maelezo amepewa kuhuhusu m wimbo wa Mugambo wa mwanamuziki huyo kutoka Tanzania wakati alipokuwa akiulizia wimbo ambao ni wa kitamaduni na wa kiafrika.
Hapa Lil Kim akizungumza na Ruebeny mtangazaji wa Redio Clouds wakijadili mambo kadhaa kwa ajili ya tamasha hilo.

Mwanamuziki Lil Kim wa Marekani akiwasili kwenye viwanja vya Leaders kwa jili ya kuangalia mazingira na kujaribu vyombo kabla hajafanya mambo yake makubwa hapo baadae.
Tayari mashabiki wameshafurika kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni kwa ajili ya kushuhudia tamasha kubwa la muziki la Fiesta Jipanguse 2010 "Rrrrrrah " kama unavyoona umati huu ulikaa chini kwa hamu kubwa ukimwangalia mwanamuziki Lil Kim ambaye yuko hapa akijaribu vyombo kwa sasa.

MWANAMUZIKI LADY JAY DEE AFUNIKA MZALENDO PUB NA KUDHIHIRISHA UKOMANDOO WAKE KATIKA GEMU LA MUZIKI!!

Mwanamuziki Lady Jay Dee akiwalisha keki mashabiki wake wakati wa onesho lake la kutimiza miaka kumi katika gemu ya muziki kwa mafanikio makubwa, onesho limefanyika usiku wa kuamkia leo pale Mzalendo Pub na kukusanya mashabiki lukuki huku kukiwa na misururu mikubwa ya kununua tiketi, hata hivyo baadhi ya mashabiki walishindwa kuingia kutokana na uingi wa watu waliohudhuria onesho hilo.
Jay Dee alimshukuru Mungu, Wazazi wake Mumewe na Mashabiki wake ambao ndiyo hasa kwa kiasi kikubwa wamechangia yeye kufikia hapo alipofikia katika mafanikio yake kimuziki, katika onesho hilo aliwashirikisha wanamuziki Chegge wa TMK Family na TID wa Top Band ambao ameimba nao baadhi ya nyimbo zake alizozipiga katika onesho hilo, Hongera sana Lady Jay Dee umefunika ile mbaya.
Lady Jay Dee akipagawisha mashabiki wake kwenye onesho la kutimiza miaka kumi katika muziki onesho lililofurika mashabiki kama unavyoona mdau.
Top In Dar (TID) akifanya vitu vyake kwenye wimbo walioshirikiana na mwanamuziki Lady Jay Dee usiku wa kuamkia leo lilikuwa ni onesho la kufurahisha na lililofurika mashabiki kiasi kwamba hata wengine walishindwa kuingia kutokana na msongamano.
Mwanamuziki Chegge wa kundi la TMK Family kutoka Kimumeni Temeke akimpa shavu Lady Jay dee katika onyesho lake la kutimiza miaka kumia katika muziki usiku wa kuamkia leo kulia ni mwanamuziki Hessein Machozi.
Lady Jay Dee na kundi lake la Machozi Band wakifanya mambo makubwa jukwaani.
Mdau Jofrey Mwakibete wa Mo Blog mwenye fulana nyeusi naye akajichanganya pamoja na mashabiki katika kupata shangwe za mwanamuziki Jay Dee.
Melisa akipata hisia kali wakati mwanamuziki Lady Jay Dee alipokuwa akifanya mambo makubwa jukwaani usiku wa kuamkia leo kwenye onesho lake la kutimiza miaka kumi katika muziki lililofanyika kwenye ukumbi wa Mzalendo Pub jijini Dar es salaam nyuma ni lafiki yake Dark.
Kulia ni Eve Temu na Jaquiline Temu pamoja na marafiki zao walikuwepo Mzalendo Pub ili kushuhudia onesho kali na la kukata na shoka la Mwanadada Lady Jay Dee katika kutimiza miaka kumi kwenye fani ya muziki.
Mdau Jafari kushoto akishoo love na marafiki zake.
Watangazaji wa kipindi cha Powerbreakfasti kutoka redio Clouds Paul James mwenye kofia na Barbara Hassan wakiwa na marafiki zao kulia ni mdau Nick Magarinza aka "Nick Butt" nao walijimwaga mzalendo Pub usiku wa kuamkia leo.

Mdau Rangia kulia akiwa amepozi wakati onesho la Lady Jay Dee lililpokuwa likidendelea kwenye ukumbi wa Mzalendo Pub Jijini Dar usiku wa kuamkia leo, katikati ni Mama Hasheem Thabeet na kushoto ni mdau Dulla Makubelly wakifuatilia kwa karibu onesho hilo.

Mwigizaji wa Filamu Dr. Cheni na Maiwaifu wake Sabrina nao walimpiga tafu Lady Jay Dee usiku wa kuamkia leo.
Kutoka kushoto ni Gadiner G Habash, George Kavishe Meneja wa kinywaji cha Kilimanjaro Lager na maiwaifu wake.
Ankal wa Blogu ya Jamii na Shear Illusion wakipozi kwa picha.
Mashabiki wa Machozi Band wakijimwaga stejini.

MWANAMUZIKI JEFF DOGOLABANGO (ALANDJI) AONGOZA USAFI MWANANYAMALA HOSPITALI!!

Mwanamuziki kutoka Ivory Coast Jeff Dogolobango anayetamba na wimbo wake mpya wa (Alandji)kushoto pamoja na Meneja Mkuu Uhusiano na Mawasiliano wa Serengeti Breweriers Ltd Teddy Mapunda wakishiriki kwenye kampeni ya kufanya usafi katika Hospitali ya Mwananyamala na Kituo cha polisi cha Oysterbay leo ikiwa ni pamoja na kupiga vita ugonjwa wa Maralia kupitia kampeni ya Zinduka.
Kampeni hiyo imeshirikisha wasanii wanaoshiriki kwenye tamasha la Fiesta Jipanguse 2010 "Rrrrrah", wafanyakazi wa Serengeti Breweriers pamoja na wafanyakazi wa Clouds Fm, ambapo wote kwa pamoja, wasanii walioshiriki katika zoezi hilo wanatarajiwa kupanda katika jukwaa la Fiseta Kesho kwenye Viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es salaam
Pia wanashiriki wanamuziki wakubwa kama vile Lil Kim kutoka nchini Marekani na J. Martin kutoka Nigeria watakaowasili wakati wowote kuanzia sasa ili kuja kuwarusha mashabiki wa tamashi hilo hapo kesho.
Mkuu wa kituo cha polisi cha Oysterbay Kamanda G.C.Mapunda akipaka rangi katika kuta za jengo la kituo hicho wakati wa kampeni ya kufanya usafi kituoni hapo iliyofanywa na wasanii mablimbali wanaoshiriki katika tamasha la Fiesta Jipanguse 2010 linalotarajiwa kufanyika kesho kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es salaam.
Teddy Mapunda na Mwanamuziki Keisha wakifanya usafi kwa kupiga deki katika lango kuu la kuingilia kwenye kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar es salaam leo.
Mmoja wa wakurugenzi wa Redio Clouds Ruge Mutahaba akizungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Kamanda E.J. Kalinga kushoto wakati wasanii mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa Serengeti Breweriers na Clouds FM walipoenda kituoni hapo kufanya usafi ikiwa ni pamoja na kupaka rangi kwenye majengo ya kituo hicho, wa pili kutoka kulia ni Meneja Mkuu Uhusiano na Mawasiliano SBL Teddy Mapunda na katikati ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Oysterbay kamanda G.C.Mapunda.
Wafanyakazi wa Serengeti Breweriers wakifanya usafi katika wodi hospitalini hapo.
Meneja Mkuu wa Uhusiano na Mwasiliano SBL Teddy Mapunda akizungumza na wanahabari wakati wa kampeni ya kufanya usafi kwenye hospitali ya Mwananyamalea leo katikati ni Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dr. Zuhura Majapa na kushoto ni Ruge Muhataba wa Clouds Fm Redio.

Kweli sio kwamba unaweza kufanya kila kitu Mtangazaji wa Redio Clouds kipindi cha Powerbreakfast Gerald Hando kushoto alishindwa kuunganisha kofia aliyopewa kwa ajili ya kutumia kwa tahadhari wakati akifanya usafi katikati ni B 12 mtangazi Clouds na kuliani Jo Makini Mwamba wa Kaskazini.
Wanamuziki Keisha kushoto na Angel kulia wakipozi kwa picha na watoto katika hospitali ya Mwananyamala leo wakati wanamuziki hao waliposhiriki katika zoezi la kufana usafi hospitalini hapo.
Meneja Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano wa Serengeti Breweriers Ltd Teddy Mapunda akizungumza na wasanii mbalimbalii wakati wa kufanya usafi katika hospitali ya Mwananyamala leo kwa ajili ya kutekeleza kampeni ya usafi katika Manispaa hiyo.