Showing posts with label us. Show all posts
Showing posts with label us. Show all posts

M-Net's Big Brother ALL STARS: Images from day 14 (Sunday August 1, 2010)

It’s day 14 on M-Net’s Big Brother All Stars --- and Hannington and Sammi are shocked when they are evicted into the brand new BIG BROTHER BARN where their tasks will also see them caretaking chickens and cows! In an action packed show that also saw Ghanaian singing sensations Ruff & Smooth head onto the Big Brother stage, Big Brother revealed an exciting new twist to the popular reality series. Evicted housemates will now enter the Barn and at the end of 9 weeks, audiences will pick which housemates get a chance to return to the main Big Brother All Stars house to compete for the USD 200 000!Stay tuned to M-Net’s BIG BROTHER ALL STARS with 24/7 coverage on DStv channel 198 plus daily edited shows on M-Net and AfricaMagic. For more information on the series, log on to www.mnetafrica.com/bigbrother. Pictured here: Uti

RAIS KIKWETE KUFUNGUA MKUTANO WA 49 WA UMOJA WA MASHAURIANO YA KISHERIA ASIA NA AFRIKA!!

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Oliver Mhaiki (kushoto)akitangaza kwa waandishi wa habari juu ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano wa 49 wa mwaka wa Umoja wa Mashauriano ya Kisheria baina ya Nchi za Asia na Afrika(AALCO) unatarajiwa kuanza tarehe 5.08.2010 hadi 8.08.2010 mjini Dar es salaam. kulia ni Mkurugenzi wa Katiba na Haki za Binadamu kutoka Ofisi ya Mwanasheria mkuu wa Serikali Mathew Mwaimu. Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO -Dar es salaam.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya M. Kikwete anatarajiwa kufungua mkutano wa 49 wa mwaka wa Umoja wa Mashauriano ya Kisheria baina ya nchi za Asia na Afrika (AALCO) unaotarajiwa kufanyika katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 5-8 Agosti mwaka huu (2010).

Hii ni mara ya pili kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huu. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1986 wakati mkutano kama huu ulipofanyika mjini Arusha.

Mkutano huu unatarajiwa kuhudhuriwa na wajumbe wapatao 200 kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo Mawaziri wa Sheria, Wanasheria Wakuu na viongozi mbalimbali waandamizi wa sekta ya sheria kutoka nchi wananchama wa AALCO na mashirika mengine ya kimataifa.

Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria na Sekretariati ya AALCO iliyopo New Delhi, India ipo katika maandalizi ya mwisho ya mkutano huu.

Katika mkutano huu, wajumbe watapokea na kujadili taarifa mbalimbali za utendaji kazi wa Umoja huu na zile zinazogusa sheria za kimataifa. Aidha, wajumbe watajadili masuala mtambuka kama mapambano dhidi ya rushwa, mabadiliko ya tabia nchi, hifadhi ya mali asili na tamaduni.

Pamoja na mambo mengine, mkutano huu utajadili changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia kwa lengo la kupata suluhu na kuzishauri Nchi Wananchama namna bora ya kupambana nazo.
AALCO, ambayo awali ilifahamika kama Kamati ya Mashauriano ya Kisheria ya Asia (ALCC), ilianzishwa mwezi Novemba 1956 baada ya Mkutano wa Bandung (Bandung Conference) wa mwaka 1955. Nchi saba waanzilishi ni Burma (sasa Myanmar), Ceylon (sasa Sri Lanka), India, Indonesia, Iraq, Japan, Misri na Syria ambazo wakati huo zilijulikana kama Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu (United Arab Republic).

Baadaye wigo ulipanuliwa na kujumuisha nchi za Afrika. Mnamo mwezi Aprili, 1958 jina la Kamati hiyo lilibadilishwa na kuwa Kamati ya Mashauriano ya Kisheria baina ya nchi za Asia na Afrika (Asian-African Legal Consultative Committee).

Mkutano wa 40 wa Kamati ya Mashauriano ya Kisheria ya Asia na Afrika uliofanyika New Delhi, India mwaka 2001 uliridhia mabadiliko ya jina na kuwa Umoja wa Mashauriano ya Kisheria baina ya Nchi za Asia na Afrika (Asian–African Legal Consultative Organisation - AALCO).

Kwa sasa AALCO ina nchi wanachama 47. Nchi hizo ni Misri, Bahrain, Bangladesh, Brunei, Botswana, Cameroon, Cyprus, Korea Kaskazini na Gambia. Nchi nyingine ni Ghana, India, Indonesia, Iraq, Iran, Japan, Jordan, Kenya, Kuwait, Lebanon na Libya.

Wanachama wengine ni Malaysia, Mauritius, Mongolia, Myanmar, Nepal, Nigeria, Oman, Pakistan, China, Qatar, Korea Kusini, Saudi Arabia, Senegal, Sierra Leone, Singapore, Somalia, Afrika Kusini, Sri Lanka, Palestina, Sudan, Syria, Thailand, Uturuki, Uganda, Umoja wa Falme za Kiarabu, Yemen na Tanzania.

ALIYEKUWA MISS TANZANIA 2004,FARAJA KOTA AMPONGEZA MUMEWE

WABUNGE waliomaliza muda wao Mohamed Dewji kushoto na Mbunge mwezake Lazaro Nyalandu wakishangilia kwa pamoja baada kupata ushindi mkubwa katika majimbo yao, Mohamed Dewji aliibuka kwa asimilia 95 katika jimbo la Singinda Mjini huku Nyalandu akiibuka kwa asilimia 89 katika jimbo la Singida Kaskazini.

Faraja Kota katkati ambaye ni mke wa Razaro Nyalandu pamoja na mumewe kulia wakiwa katika picha ya pamoja Mohammed Dewji aliyekuwa Mbunge wa Singida Mjini wakifurahi ushindi walioupata katika majimbo katika kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi kwenye majimbo yao, Faraja Kota aliwahi kuwa Miss Tanzania mwaka 2004 hivi sasa ni mama wa watoto wawili.

MZEE MALECELA AKUBALI MATOKEO MTERA!!

Mzee Samwel Malecela.

HABARI TOKA JIMBO LA MTERA LINASEMA MGOMBEA LIVINGSTONE LUSINDE AMEMSHINDA MH. JOHN SAMWEL MALECELA KATIKA KURA ZA MAONI NA ANATEGEMEA KUWA NDIYE ATAYEPITISHWA KUGOMBEA UBUNGE KWA TIKETI YA CCM KWA JIMBO HILO, KWA MUJIBU WA MATOKEO YALIYOTANGAZWA SAA 4 LEO

(Habari hii ni kwa hisani ya www.issamichuzi.blog )

MUZASHA TOURS AND SAFARIS YADHAMINI MISS TANZANIA MWAKA MMOJA!!

Mkurugenzim wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga akizungumza mbele ya waandishi wa habari kwenye hoteli ya Holiday Inn jijini Dar es salaam leo wakati alipotangaza rasmi udhamini wa kampuni ya Muzasha Tours Safari katika Miss Tanzania mwaka huu,kutoka kushoto ni Benito Mandele Mwanasheria wa Muzasha, Benedict Mulokozi Mkurugenzi, Muzamil Katunzi Mkurugenzi Mkuu na Erasmus Kwayu Mkurugenzi Uendeshaji.
Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga akibadilishana hati za mkataba na Mkurugenzi mkuu wa Muzasha Tours Safaris, Muzamil Katunzi wanaoshuhudia tukio hilo ni Miss Tanzania anayemaliaza muda wake Miriam Gerald, Erasmus Kwayu na Benedict Mulokozi.

Dk. Asha-Rose Migiro Azindua Mradi wa Maktaba Mtandao LRCT

. Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dk. Asha-Rose Migiro akibofya Kompyuta kuashiria uzinduzi rasmi wa Mradi wa Maktaba Mtandao wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania (LRCT) uliofanyika jana jijini Dar es salaam.
(Picha zote na Ofisa Habari wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Munir Shemweta)
Akikabidhiwa zawadi na Mwenyekiti wa Tume Jaji Profesa Ibrahim Juma.

Akiwa na makamishna wa Tume kutoka kushoto Kamishna Manyesha, Onel Malisa, Mohamed Ismail, Jaji Profesa Juma Mwenyekiti wa Tume na Katibu Mtendaji wa Tume Japhet Sagasii.



ISAYA NA CAROLINE WAMEREMETA ZAIDI JIJINI DAR ES SALAAM!!

Bwana Isaya na mke wake Caroline wakitoka kanisani mara baada ya kufunga ndoa takatifu katika kanisa la KKKT Usharika wa Kijitonyama jumamosi iliyopita na kufuatiwa na sherehe kubwa iliyofanyika kwenye ukumbi wa SunSet ulioko Mbezi Makonde jijini Sar es salaam na kuhudhuria na ndugu , marafiki na jamaa zao. wadau wa FULLSHANGWE tunawatakia maisha malefu maharusi hawa na Mungu awabariki na kuwapa Afya, Mafanikio na Amani katika maisha yao mapya.
Hapa wakipozi kwa picha kwenye Hoteli ya Giraffe Ocean View iliyoko Mbezi Beach.

Dada wa Bwana Harusi anayeitwa Subi akiwamiminia maharusi Kinywaji cha Champaign mara baada ya kufungua rasmi katika sherehe hiyo.

Maharusi wakiwa wametulia na wapambe wao katika meza kuu wakati sherehe yao ilipokuwa ikiendelea.

Kocha wa Simba Patrick Phiri akiwasili kwenye uwanja wa Mwalimu J.K. Nyerere leo!!

Kocha Mkuu wa Timu ya Simba ya Dar es Salaam, Patrick Phiri (katikati) akiwasili kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo mchana kwa ajili ya kuinoa timu hiyo inayojiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu ujao, ambapo kocha huyo atakua na kazi ya ziada kukiandaa kikosi hicho kwa ajili ya mchezo na watani wao wa jadi Dar Young African katika mchezo wa Ngao ya Hisani (Jamii) unaotarajia kuchezwa kwenye Uwanja wa Taifa Agosti 14 mwaka huu. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Geofrey Kaburu. Picha kwa hisani ya