Showing posts with label POLITICS. Show all posts
Showing posts with label POLITICS. Show all posts

WAZIRI WA KAZI PROF.KAPUYA AZINDUA MWAKA WA VIJANA!!

Mgeni Rasmi Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Prof. Athman Jma Kapuya akiongea na vijana wakati wa kongamano la vijana lililoandaliwa na Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa YUNA na kufanyika ukumbi wa APEADU kwenye ofisi za Umoja huo mtaa wa Mafinga Kinondoni Jijini Dar es salaam katika kuadhimisha siku ya vijana Duniani.
Katika kongamano hilo vijana wamejadili mambo mbalimbali yanayowahusu kama vile Elimu, Afya, Ajira, Michezo, Haki zao na mambo mengine mengi wanayokumbana nayo katika maisha ya kawaida kama vijana huku wakiazimia kuomba Serikali iwaruhusu kuunda Baraza la Vijana la Taifa litakalosimamia mambo yao yote ili kuwatetea na kuwasimamia katika mipango mbalimbali ya Kisera inayowahusu vijana.
Katika Hotuba yake Waziri Kapuya amewaasa vijana kuunda Baraza litakalokuwa ni la kitaifa zaidi kuliko kuwa Baraza la kiubabaishaji linaloweza kuleta athari kubwa kwa taifa Waziri pia alizindua mwaka wa Vijana unaoanza leo tarehe 12 Agosti 2010 mpaka Agosti 11 , 2011 na utakuwa ukiadhimisha kila mwaka Duniani kote.
Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Prof. Athman Juma Kapuya akiingia kwenye ukumbi wa mkutano wa kati wa kongamano la vijana lilioandaliwa na Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa YUNA na kufanyika ukumbi wa APEADU kwenye ofisi za umoja huo Mtaa wa Mafinga Kinondoni jijini Dar es salaam nyuma ya Waziri ni Mwakilishi wa UNIDO Nchini Emmanuel Kalenzi.
Vijana kutoka shule na Asasi mbalimbali za vijana waliohudhurika katika kongamano la vijana lililofanyika leo kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha siku ya vijana Duniani.

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii yakabidhi vifaa Tiba Dodoma!!

Katibu Mkuu wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii bi. Blandina nyoni amekabidhi vifaa mbalimbali vya tiba katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, makabidhiano hayo yamefanyika juzi mkoani humo na hii ni moja ya mashine ya usingizi iliyokabidhiwa kwa hospitali hiyo
Katibu mkuu Bi Blandina Nyoni akikabidhi moja ya vifaa tiba vinavyotumika kwa ajili ya operesheni ya akina mama wajawazito kwa katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma bi. Madenge

Moja ya kitanda kinachotumika kulazia mgonjwa anayehitaji uangalizi wa hali ya juu katika chumba cha watu mahututi(ICU)

MWENYEKITI WA (YUNA) HAPA NCHINI AWAPA CHANGAMOTO VIJANA!!

Mwenyekiti wa Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa hapa (YUNA) chini Benny Kikove akizungumza na wajumbe waliohudhurika kwenye kongamano la vijana linaloendelea kwenye ofisi za UN katika ukumbi wa APEADU Mtaa wa Mafinga Kinondoni jijini Dar es salaam, kongamano hilo linajadili mambo mbalimbali yanayowahusu vijana pamoja na changamoto wanazokumbana nazo katika ujana wao katikamkuadhimisha siku ya vijana duniani.
Wanafunzi wa shule mbalimbali wakiwa katika kongamano hilo wamesema wana matarajio mengi mara baada ya kongamano hilo kwani litawafanya kupeana uzoefu mbalimbali katika kukabili chanagamoto wanazokutana nazo katika maisha ya sasa.

Mmoja wa Wajumbe wa mkutano huo na Afisa wa UN hapa nchini Bi Hoyce Temu kushoto akiandika mambo mbalimbali yanaojadiliwa na vijana katika kongamano hilo.


Wajumbe mbalimbali wakimsikiliza mwenyekiti wa Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa hapa nchini YUNA Bw. Benny Kikove wakati alipokuwa akiongea na wajumbe wa konamano hilo asubuhi hii.

WAGOMBEA UBUNGE WA CUF (W) ILALA WAJITAMBULISHA!!

Mgombea Ubunge kupitia Chama Cha Wannanchi CUF Hussein Siyoverwa akizungumza mbele ya wanahabari leo kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo wakati wagombvea hao kutoka Majimbo ya Ilala, Segerea na Ukonga walipojitambulisha mbele ya wanahabari, wanaofuatia katika picha ni Kimangala Ayubu Mussa na Gulam Nasoro Mkurugenzi wa Uenezi, Mahusiano ya Umma CUF Wilaya ya Ilala.
Wagombea wa ubunge katika majimbo ya Ilala, Segerea na Ukonga kupitia Chama Cha Wananchi CUF wakionyesha fomu zao mbele ya waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo mara baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi wa Wialaya ya Ilala leo, kutoka kulia ni Heko Pori Ukonga,Husein Siyoverwa Ilala na Kimangala Ayubu Musa Segerea.

Rais Kikwete azindua Ujenzi wa Miundombinu ya Mfumo wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete ,Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia John Mc Intyre(watatu kulia),Waziri wa Miundombinu Dr.Shukuru Kawambwa(kushoto) na Waziri wa TAMISEMI Mhe.Selina Kombani(kulia) wakifunua kitambaa kuashiria kuzindua rasmi ujenzi wa Miundombinu ya mfumo wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za uzinduzi zilkizofanyika Ferry kivukoni jijini Dar es Salaam leo mchana.
(Picha na Freddy Maro)
Mtendaji Mkuu wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka jjijini Dar es Salaam(Dar Rapid Transit Agency ) Bwana Cosmas Takule akieleza jinsi mradi huo utakavyofanya kazi pindi utakapo kamilika hivi karibuni jijini Dar es Salaam huku Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaamm williuma Lukuvi wakisikiliza kwa makini.

Mtendaji Mkuu wa Mradi wa mabasi yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam Bwana Cosmas Takule akionyesha mchoro wa ramani ya utekelezaji wa mradi huo jiji Dar es salaam huku Rais Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri wa Miundombinu Dr.Shukuru Kawambwa, Waziri wa TAMISEMI Bi.Selina Kombani na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya dunia Bwana John Mc Intyre wakisikilza kwa makini wakati wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa miundombinu ya mradi huo zilizofanyika Ferry Kivukoni, jijini Dar es Salaam leo mchana.



SIKU NILIPOKUTANA NA MKURUGENZI WA MASHITAKA ELIEZER FELESH!!

Siku nilipokutana na Mkurugenzi wa Mashitaka wa Serikali nchini (DPP) Eliezer Felesh katika mkutano wa wanasheria wa Africa na Asia uliokuwa ukifanyika kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski hivi karibuni hapa nchini na kujadili mambo mbalimbali ya kisheria,tuliongea na kubadilishana mawazo mbalimbali na Mh Felesh na nilifurahi kukutana na mtu mkarimu kama huyu.
Mwandishi wa habari mwandamizi wa Mwananchi Mkinga Mkinga akizungumza na Mwanasheria mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema katika mkutano huo huku wanahabari wakiwaangalia na kusikiliza kwa makini.

RAIS KIKWETE ALIPOTEMBELEA NANENANE MKOANI DODOMA HIVI KARIBUNI!!

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao (KIUMO) Bwana Geoffrey Kirenga akimwelezea Rais Jakaya Kikwete namna ya utekelezaji wa Mpango wa Ruzuku ya Pembejeo za Kilimo kwa kutumia utaratibu wa vocha nchini wakati wa Maonyesho ya Nanenane Mkoani Dodoma hivi karibuni.
(Picha zote na Anna Itenda wa Maelezo)
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Bi Nyabaganga Taraba (kushoto) akimwelezea Rais Jakaya Mrisho Kikwete jinsi ya utaratibu wa kuendeleza miradi ya Umwagiliaji alipotembelea kwenye Maonyesho ya Nanenane Mkoani Dodoma .

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Bi Nyabaganga Taraba (kushoto) akimwelezea Rais Jakaya Mrisho Kikwete jinsi ya utaratibu wa kuendeleza miradi ya Umwagiliaji alipotembelea kwenye Maonyesho ya Nanenane Mkoani Dodoma .

Rais Jakaya Kikwete mpenzi wa watoto akiwa kwenye picha ya pamoja na mtoto Betha Chiwanga na mama yake Neema Chiwanga walipokutana na Rais njiani wakati wa maonyesho ya nanenane Mkoani Dodoma hivi karibuni.



Mkurugenzi Mkuu wa Jukwaa la Wakulima na Wafugaji (Farmers Centre Ltd )akimwonyesha madawa mbalimbali yanayotumika kwa ajili ya Wakulima na wafugaji kwenye maonyesho ya Nanenane yaliyofanyika Mkoani Dodoma hivi karibuni .

Msajili John Tendwa aliasa Baraza la Vyama vya Siasa!!


Benjamin Sawe Maelezo Dar es Salaam.



Msajili wa Vyama vya Siasa John Tendwa ameliasa Baraza la Vyama vya Siasa kuhakikisha uchaguzi wa mwaka huu unakuwa wa Kidemokrasia na wa amani.
Bwana Tendwa alisema hayo jana (leo) jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa kwanza wa Baraza la vyama vya siasa ambapo alilitaka Baraza lililoundwa kisheria kuishauri serikali na jamii hasa katika kipindi cha uchaguzi.




Aidha alisema Baraza hilo si la kujitolea bali limeundwa kwa mujibu wa sheria na linawajibika kwa serikali na ni mshairi mkuu wa serikali katika shughuli za kisiasa. Alisema ni wajibu kwa baraza hilo kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu na alilitaka baraza hilo kutoa tamko kulaani vitendo vinavyovunja amani na sheria ikiwa ni pamoja na kukemea vyama vya siasa vilivyoanza kampeni kabla ya tarehe ya kampeni.





Pia alivionya vyama vya siasa kuachana na siasa za kutumia lugha ya matusi wakati wa kampeni na ni wajibu wa Baraza hilo kutoa miongozo mbalimbali ambayo itafuatwa na vyama vya siasa.. Bwana Tendwa alilitaka Baraza hilo kuitisha mikutano ya mara kwa mara ambapo itatoa miongozo ambayo italiweka taifa katika mahala pazuri ili kufanikisha uchaguzi kwa amani na utulivu.





Alisema baadhi ya vyama vya siasa vimeanza kapeni kabla ya uchaguzi na vinajua kufanya hivyo ni kukiuka sheria za uchaguzi na moja ya athari za kuanza kampeni kabla ya uchaguzi ni kuwekeana pingamizi na kama likikubalika chama kitakuwa hakina mgombea hivyo amevitaka vyama kufuata taratibu na sheria za uchaguzi.





Akitoa shukrani kwa niaba ya Baraza hilo Mwenyekiti wa Baraza hilo Dr.Emanuel Makaidi amesema hawatamuogopa mwanasiasa au chama chochote cha siasa kitakachokiuka maadili kwani Baraza hilo limeundwa kwa mujibu wa kanuni na sheria. Dr. Makaidi alisema Baraza hilo litakuwa mshauri mzuri wa Serikali katika mambo ya kisiasa hasa katika kipindi cha uchaguzi.

Rais Kikwete aongoza Sherehe za Nanenane Dodoma!!

Katibu Mkuu wa wizara ya Afya Blandina Nyoni akipokea kombe la ushindi wa jumla(overall winner) kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete mara baada ya banda la Wizara ya Afya kuibuka mshindi kwa kutoa huduma Bora wakati wa maonyesho ya kilimo yaliyofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Mjini Dodoma leo.(Picha na Freddy Maro)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi walohudhuria kilele cha sherehe za Wakulima, nanenane mjini Dodoma leo mchana



Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi zawadi ya trekta Mkulima Martin Mlimila baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika safu ya wakulima bora wakati wa kilele cha sikukuu ta Wakulima Nanenane iliyofanyika katika viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia kiazi kikuu na mazao mengine yaliyolimwa kwa ubora kutoka banda la Iramba, Singida wakati alipopita kukagua mazao na bidhaa mbalimbali za kilimo katika viwanja vya Nzuguni,mjini Dodoma wakati wa kilele cha siku ya wakulima nchini.

MKUTANO WA KIMATAIFA WA SHERIA NCHI ZA AFRIKA NA ASIA WAMALIZIKA - DSM.

Waziri wa Sheria na Mwanasheria Mkuu wa Gambia Edward Anthony Gomez(kulia) akisisitiza jambo kwa Naibu mwanasheria mkuu wa Tanzania Bw. George Masaju leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa 49 wa Umoja wa Mashauriano ya sheria kwa nchi za Asia na Afrika(AALCO). Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

Viongozi wa mkutano wa 49 wa mkutano wa Umoja wa Mashauriano ya sheria kwa nchi za Asia na Afrika wakiongozwa na Rais wa mkutano huo Waziri wa Sheria na Katiba wa Tanzania Mathias Chikawe (wa pili kulia) kufuatilia Michango mbalimbali kutoka kwa wajumbe wa nchi wanachama wanaoshiriki mkutano huo (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam. Mkutano huo unaomalizika leo jijini Dar es salaam umehudhuriwa na nchi 30.
Mwanasheria mkuu wa nchi ya Brunei Darussalam Mrs. Hayati Salleh akimkabidhi zawadi Waziri wa Sheria na Katiba wa Tanzania Mathias Chikawe leo jijini Dar es salaam wakati wa kuhitimisha mkutano wa 49 wa Umoja wa Mashauriano ya sheria kwa nchi za Asia na Afrika(AALCO).

Wajumbe wa mkutano wa 49 wa Umoja wa Mashauriano ya sheria kwa nchi za Asia na Afrika (AALCO) kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika na Asia.
Wajumbe wa mkutano wa 49 wa Umoja wa Mashauriano ya sheria kwa nchi za Asia na Afrika (AALCO) kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika na Asia wakichangia masuala mbalimbali wakati wa mkutano huo unaomalizika leo jijini Dar es salaam.

Mpambe wa Mandela alipewa 'mawe ya Naomi'


Aliyekuwa mkuu wa mfuko wa kusaidia watoto wa Nelson Mandela, Jeremy Ratcliffe, alisema alipokea almasi ambazo hazikuchongwa kutoka kwa mwanamitindo Naomi Campbell.




Alitoa kauli hiyo baada ya Bi Campbell kutoa ushahidi wake kwenye kesi ya uhalifu wa kivita inayomkabili kiongozi wa zamani wa Liberia Charles Taylor.



Inadaiwa alipokea almasi hizo kutoka kwa Bw Taylor mwaka 1997, zinazoweza kumhusisha na 'almasi haramu zinazotumika kugharamia vita'
Bw Ratcliffe alisema yuko tayari kutoa ushahidi The Hague na kwa sasa amekabidhi mawe hayo kwa mamlaka husika.



Alisema katika taarifa iliyopelekwa BBC, " Nilipewa almasi tatu ndogo ambazo hazikukatwa na Naomi Campbell tarehe 26 Septemba, 1997."




Katika kesi hiyo, Bi Campbell alisema alipewa "mawe machafu" baada ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Nelson Mandela ambapo Bw Taylor naye alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa.




Alisema watu wawili ambao hawakuwafahamu walikwenda chumbani kwake na kumpa mawe hayo.
Aliiambia mahakama kuwa hakuwa na ushahidi wowote kuwa zilitoka kwa Bw Taylor na alimpa Bw Ratcliffe kwasababu alitaka mawe hayo yatolewe kwenye mashirika ya hisani.
Kwa habari zaidi nenda www.bbcswahili.com

PROF. IBRAHIM LIPUMBA ACHUKUA FOMU ZA KUGOMBEA URAIS LEO!!

Mgombea urais kupitia Chama Cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba kulia kwa pamoja na mgombea mwenza Duni Haji Duni wakinyanyua fomu zao juu kuonyesha kwa wanachama wao mara baada ya kuchukua katika ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Taifa jijini Dar es salaam leo kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama hicho na mgombea urais kwa upande wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.

Rais wa zamani wa Uganda afariki dunia

Rais wa zamani wa Uganda Godfrey Lukongwa Binaisa amefariki dunia.
Kwa mujibu wa binti yake Nakalema, Binaisa aliyekuwa na umri wa miaka 90 amefariki usiku wa kuamkia leo akiwa nyumbani kwake mjini Kampala.


Mzee Binaisa alikuwa Rais baada ya utawala wa Idi Amin kuondolewa mwaka 1979.

Aliteuliwa Juni 1979 na baraza tawala la wakati huo la National Consultative Council- NCC kuchukua hatamu baada ya kuondolewa kwa hayati Prof Yusuf Kironde Lule aliyetawala kwa siku 68 tu.

Binaisa naye aliondolewa madarakani mwezi Mei mwaka 1980 na tume ya kijeshi ambayo ilikuwa inaongozwa na hayati Paul Muwanga akiwa na Rais wa sasa wa Uganda Yoweri Museveni kama naibu wa Muwanga.
Amewaacha watoto wanne. Mazishi bado hayajajulikana.
Kwa habari zaidi tembelea

WILBROAD SLAA KATIKA ZOEZI LA KUTAFUTA WADHAMINI MKOANI MTWARA!!

Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Wilbroad Slaa akihutubia maelfu ya wakazi wa Mtwara katika harakati za kutafuta udhamini. Picha kwa hisani ya
(www.mjengwa.blog )

Sehemu ya umati mkubwa wa wakazi wa Mtwara waliohudhuria mkutano huo.


Mkutano wa wanasheria wa Africa na Asia (AALCO) wafunguliwa jijini Dar es salaam!!

Waziri wa Katiba na Sheria Mathias Chikawe(kushoto) na Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Philip Marmo (kulia) wakipata maelezo ya vitabu mbalimbali vya sheria kutoka kwa Bw. Omary Mwinyihery Afisa Masoko wa kampuni ya uchapishaji wa vitabu vya sheria (LawAfrica Publishing Ltd) leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa 49 wa Umoja wa Mashauriano ya sheria kwa nchi za Asia na Afrika.
(Picha na Aron Msigwa – MAELEZO).
Mkurugenzi wa Taasisi ya kupambana na Rushwa TAKUKURU Dk. Edward Hosea kushoto Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Friderick Werema kulia na Naibu Mwanasheria mkuu George Masaju pamoja na washiriki wengine wa mkutano huo wakifuatilia kwa makini wakati ulipokuwa ukiendelea leo mara baada ya kufunguliwa rasmi.
Mwanasheria mkuu wa Malaysia na Rais wa mkutano wa mwaka wa 48 wa Umoja wa Mashauriano ya sheria kwa nchi za Asia na Afrika(AALCO) Bw. Abdul Gani Patail akiongea na washiriki wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam.

Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Philip Marmo kushoto na viongozi wa Mkutano wa 49 wa Umoja wa Mashauriano ya sheria kwa nchi za Asia na Afrika wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam.

Washiriki wa mkutano wa 49 wa Umoja wa Mashauriano ya sheria kwa nchi za Asia na Afrika wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki kutoka mataifa ya Bara la Asia wakiwa katika mkutano huo.

SIJAKATA TAMAA KISIASA ASEMA SHAMSI VUAI NAHODHA!!


Na Juma Mohammed, Maelezo Zanzibar.
Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha amesema hajakata tama kisiasa kwani ikitokea fursa yengine yoyote ya kuwania Urais wa Zanzibar hatosita kugombea kwa kuwa anaamini anazo sifa zinazotakiwa na Chama cha Mapinduzi(CCM).




Nahodha ambaye ni Mwakilishi wa Jimbo la Mwanakwerekwe alisema jana katika upandishaji bendera Tawi la CCM Mwanakwerekwe Mjini Unguja, alisema akiwa kijana anaamini nanaweza kutimiza matakwa ya CCM na wananchi wote kwa ujumla. “Napenda kuwaeleza kuwa mimi sijakata taamaa, bado nina matumaini na ikiwa itatokea fursa hiyo nitagombea tena, lakini kwa sasa ninayo kazi moja tu nayo ni kukisaidia Chama changu mgombea wetu Dk. Shein ashinde katika Uchaguzi Mkuu” Alisema Nahodha.




Waziri Kiongozi alisema kuwa kama walivyo wazee vijana nao wana uwezo mkubwa katika nafazi za uongozi na wanaosema vingine wamefilisika kisiasa. “Hata wazee wasiokuwa makini wapo kama ilivyo kwa baadhi ya vijana, lakini si sahihi vijana wakanyimwa nafasi ya uongozi eti tu sababu ya ujana wao” Alisema Nahodha ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 48.



Nahodha alitumia fursa hiyo kuwataka radhi waliokereka katika Jimbo lake juu ya hatua ya kuwania tena Uwakilishi akisema alifanya hivyo kwa faida ya Chama na Serikali na kuahidi ataweka uzito mkubwa kiutendaji katika Jimbo iwapo atawaa tena nafasi hiyo.



Akizungumzia umuhimu wa ujenzi wa majengo bora ya matawi ya CCM, Nahodha ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu, alisema majengo ya Chama hicho lazima yaendane na hadhi ya CCM.



Hata hivyo, alionya kwamba uhai na uimara wa CCM hautokani na majengo mazuri pekee, bali namna wanachama wake watakavyokienzi ndani ya nyoyo zao na viongozi kuwajibika. Nahodha alichangia ujenzi wa jengo hilo shilingi milioni 2 taslimu na kuahidi kutoa shilingi milioni tatu kabla ya Uchaguzi Mkuu ili kutoa msukumo kwa Tawi hilo liweze kutumika mapema.

UN Secretary-General's statement on United Republic of Tanzania

United Nations Secretary-General Ban Ki Moon.
The Secretary-General congratulates the people of the United Republic of Tanzania, particularly of Zanzibar, for the peaceful holding of their recent referendum in Zanzibar. He also welcomes the inter-party agreement between the two main political parties, Chama Cha Mapinduzi and Civic United Front, that led to the referendum, aimed at paving the way for a long term reconciliation.
The Secretary-General is encouraged by the determination of the people of Zanzibar to build a peaceful and united future, and reiterates the readiness of the United Nations to assist them.

Matokeo ya kura za maoni kinondoni, kawe, ubungo na A-Taun leo

Jimbo la Kinondoni

Iddi Mohamed Azzan ameibuka kidedea baada ya kupata kura 6196, akifuatiwa na Mustafa Muro kura 3059 huku Shy-Rose Banji akipata kura 2830.

Wagombea wengine katika Jimbo hilo ni pamoja na;

Mpoki Mwambulukutu..... kura 985
Godwin Kabisa..... kura 443
Kakolwa Mbano..... kura 395
Nkuruma Munjori..... kura198
Mackdonald Lunyilija..... kura146
Issa Omari.....kura 111
Bakari Maige..... kura 98.

Jimbo la Kawe.


Katika jimbo hili Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya ya Kinondoni Angela Charles Kizigha ameshinda kwa kupata kura 3140 akifuatiwa na Kippy Warioba aliyepata kura 2752 wakati Zainuddin Adamjee amepata kura 2466.

Wengine katika jimbo hilo ni;

Aric Suma..... kura 1576
Jumaa Pijei..... kura 646
Mohamoud Madenge..... kura 588
Margaret Lema..... kura 443
Dr Malima Bundara..... kura 340
Faustin Kikova..... kura 240
Omary Wahure..... kura 214
Dr Petrnilla Ngiloi..... kura 191
Harold Maruma..... kura 172
Biton Mwenisongole..... kura 160
Elias Nawera..... kura 140
Japhet Robi..... kura 78
Nicodumus Chegula..... kura 68.

Jimbo la Ubungo

Hawa Mgonja Ng'umbi ndiye anayeng'ara katika matokeo ya uchaguzi wa kura za jimbo hilo ambapo amepata kura 7970, akifuatiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Shamsa Mwangunga aliyeambulia kura 6998 wakati Nape Nnauye akiondoka na kura 3734.

Matokeo ya wagombea wengine katika jimbo hilo;
Alfred Nchimbi..... kura 848
Michael Lupiana..... kura 516
Perpetua Haule..... kura 393
Dr Apollo Kissai..... kura 316
Peter Msuya..... kura 216
Assumpta Nalitoleta....192
Gaspar Hizza..... kura 181
Eliona Nkya..... kura 159
Slaus Mwisomba..... kura 158
Zangina Zangina..... kura 107.

ARUSHA

Naye Woinde Shizza wa Globu ya Jamii Arusha anaripoti kwamba matokeo ya kura za maoni kwa upande wa ubunge jimbo la arusha Dk. Batlida Burian amepatakura 9970 na aliyekuwa mbunge wa miaka 5 iliyopita Mh. Felix Mrema amepata kura 4347, Dk. Hamis Said Kibola amepata kura 834, Deogratias Mtuo amepata kura 268, Aloyce Peter Kilimbo amepata kura 116, Michael Sekajingo amepata kura 105. Hivyo mshindi ni Dk. Burian

Kwa uapnde wa ubunge jimbo la aAumeru Magharibi Bw. Goodluck Joseph ole Medeye ameibuka mashindi na kummwaga aliyekuwa mbunge wa miaka 5 E Mh. Elisa Mollel na wengineo walioshinda ni Jeremiah Sumari katika jimbo lake la Meru.
KWA HISANI YA http://www.michuzi.blog/

Matokeo zaidi kura za maoni za CCM leo



Matokeo toka jimbo la Tanga mjini Yanaonesha kwamba mbunge anayemaliza muda wake Mh. Harith Mwapachu, ameangushwa na mgombea Omari Nundu.

Mwapachu, ambaye amepata kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, ameangushwa na mpinzani wake kwa kuzidiwa kura 5293 huku Kassim Kisauji akipata kura 5087.

Katika Jimbo la Muheza, mbunge anayemaliza muda wake Herbet Mntangi ameshinda kwa kura 9,142, akifuatiwa na Julius Shemwaiko (6,595) na Jonathan Mhina (629).

Korogwe Mjini Yussufu Nasiri ameshinda kwa kura 2513, akifuatiwa na Joel Bendera (2258) na Mariam Nafutalkura (428).

Kwa matokeo zaidi yaliyopatikana leo

nenda libeneke la michuzi-matukio

RAIS KIKWETE KUFUNGUA MKUTANO WA 49 WA UMOJA WA MASHAURIANO YA KISHERIA ASIA NA AFRIKA!!

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Oliver Mhaiki (kushoto)akitangaza kwa waandishi wa habari juu ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano wa 49 wa mwaka wa Umoja wa Mashauriano ya Kisheria baina ya Nchi za Asia na Afrika(AALCO) unatarajiwa kuanza tarehe 5.08.2010 hadi 8.08.2010 mjini Dar es salaam. kulia ni Mkurugenzi wa Katiba na Haki za Binadamu kutoka Ofisi ya Mwanasheria mkuu wa Serikali Mathew Mwaimu. Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO -Dar es salaam.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya M. Kikwete anatarajiwa kufungua mkutano wa 49 wa mwaka wa Umoja wa Mashauriano ya Kisheria baina ya nchi za Asia na Afrika (AALCO) unaotarajiwa kufanyika katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 5-8 Agosti mwaka huu (2010).

Hii ni mara ya pili kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huu. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1986 wakati mkutano kama huu ulipofanyika mjini Arusha.

Mkutano huu unatarajiwa kuhudhuriwa na wajumbe wapatao 200 kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo Mawaziri wa Sheria, Wanasheria Wakuu na viongozi mbalimbali waandamizi wa sekta ya sheria kutoka nchi wananchama wa AALCO na mashirika mengine ya kimataifa.

Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria na Sekretariati ya AALCO iliyopo New Delhi, India ipo katika maandalizi ya mwisho ya mkutano huu.

Katika mkutano huu, wajumbe watapokea na kujadili taarifa mbalimbali za utendaji kazi wa Umoja huu na zile zinazogusa sheria za kimataifa. Aidha, wajumbe watajadili masuala mtambuka kama mapambano dhidi ya rushwa, mabadiliko ya tabia nchi, hifadhi ya mali asili na tamaduni.

Pamoja na mambo mengine, mkutano huu utajadili changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia kwa lengo la kupata suluhu na kuzishauri Nchi Wananchama namna bora ya kupambana nazo.
AALCO, ambayo awali ilifahamika kama Kamati ya Mashauriano ya Kisheria ya Asia (ALCC), ilianzishwa mwezi Novemba 1956 baada ya Mkutano wa Bandung (Bandung Conference) wa mwaka 1955. Nchi saba waanzilishi ni Burma (sasa Myanmar), Ceylon (sasa Sri Lanka), India, Indonesia, Iraq, Japan, Misri na Syria ambazo wakati huo zilijulikana kama Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu (United Arab Republic).

Baadaye wigo ulipanuliwa na kujumuisha nchi za Afrika. Mnamo mwezi Aprili, 1958 jina la Kamati hiyo lilibadilishwa na kuwa Kamati ya Mashauriano ya Kisheria baina ya nchi za Asia na Afrika (Asian-African Legal Consultative Committee).

Mkutano wa 40 wa Kamati ya Mashauriano ya Kisheria ya Asia na Afrika uliofanyika New Delhi, India mwaka 2001 uliridhia mabadiliko ya jina na kuwa Umoja wa Mashauriano ya Kisheria baina ya Nchi za Asia na Afrika (Asian–African Legal Consultative Organisation - AALCO).

Kwa sasa AALCO ina nchi wanachama 47. Nchi hizo ni Misri, Bahrain, Bangladesh, Brunei, Botswana, Cameroon, Cyprus, Korea Kaskazini na Gambia. Nchi nyingine ni Ghana, India, Indonesia, Iraq, Iran, Japan, Jordan, Kenya, Kuwait, Lebanon na Libya.

Wanachama wengine ni Malaysia, Mauritius, Mongolia, Myanmar, Nepal, Nigeria, Oman, Pakistan, China, Qatar, Korea Kusini, Saudi Arabia, Senegal, Sierra Leone, Singapore, Somalia, Afrika Kusini, Sri Lanka, Palestina, Sudan, Syria, Thailand, Uturuki, Uganda, Umoja wa Falme za Kiarabu, Yemen na Tanzania.