Rais wa zamani wa Uganda Godfrey Lukongwa Binaisa amefariki dunia.
Kwa mujibu wa binti yake Nakalema, Binaisa aliyekuwa na umri wa miaka 90 amefariki usiku wa kuamkia leo akiwa nyumbani kwake mjini Kampala.
Mzee Binaisa alikuwa Rais baada ya utawala wa Idi Amin kuondolewa mwaka 1979.
Aliteuliwa Juni 1979 na baraza tawala la wakati huo la National Consultative Council- NCC kuchukua hatamu baada ya kuondolewa kwa hayati Prof Yusuf Kironde Lule aliyetawala kwa siku 68 tu.
Binaisa naye aliondolewa madarakani mwezi Mei mwaka 1980 na tume ya kijeshi ambayo ilikuwa inaongozwa na hayati Paul Muwanga akiwa na Rais wa sasa wa Uganda Yoweri Museveni kama naibu wa Muwanga.
Amewaacha watoto wanne. Mazishi bado hayajajulikana.
Kwa habari zaidi tembelea
0 comments:
Post a Comment