MISS TANZANIA WAFANYA HAFLA YA KUWATAMBULISHA MUZASHA TOURS AND SAFARIS KAMA WADHAMINI WAPYA!!

Mkurugenzi wa Muzasha Tours and Safaris Bw. Muzamil Issa Katunzi wa pili kutoka kushoto akiwa na marafiki zake katika hafla ya kutambulisha hiyo kama wadhamini wenza wa Vodacom Miss Tanzania ambayo imedhamini mashindano hayo kwa shilingi milioni 61.
Katika picha kutoka kulia ni Benedict Mulokozi Mkurugenzi, Bw. Charles Mtawali Mkurugenzi wa CM. CO. LTD na mwisho kushoto ni Kulwa Katuzi, Hafla hiyo inayoendelea sasa hivi inafanyika kwenye hoteli ya Regency Park Mikocheni jijini Dar es salaam, FULLSHANGWE tunawapongeza Muzasha kwa kudhamini Vodacom Miss Tanzania kwani kwa nafasi hii mtaweza kusaidia katika kukuza utalii wa ndani jambo ambalo limekuwa likipigiwa mbiu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Bodi ya ke ya Utalii TTB.
Wadau mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo na kuburudika vya kutosha.
Mama Elsi Mgimba katikati akiwa na marafiki zake Miss Domestic Tourism Sia Ndeskoi kulia na Amanda Chale wakiwa katika hafla hiyo.

Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga kulia akifurahia jambo na maafisa wa kamati hiyo katika hafla ya kuwatambulisha wadhamini wapya wa Vodacom Miss Tanzania Kampuni ya Muzasha Tours and Safaris ya jijini kwenye hoteli ya Regency Park jijini Dar es salaam inayoendelea usiku huu, wanaofuatia katika picha ni Mkuu wa Itifaki Albert Makoye, Afisa Uhusiano Hidan Ricco na Miss Domestic Tourism Sia Ndaskoi.

Mdau Cesilia kutoka Radio Uhuru akichati na wadau mbalimbali katika hafla hiyo kulia ni Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment