Mwanamuziki mwalikwa Buti Jiwe alikuwapo jukwaani katika onyesho la masala Festival!!

Mr.Buti Jiwe mwenye kitambaa kichwani na Christian Bakotessa aka Chris-B.Mcharaza solo machachari.
Mr.Buti Jiwe aka Galinoma Jr,
Mwana Muziki wa Kizazi kipya cha mziki wa dansi,alikuwa msanii mwalikwa wa Ngoma Africa katika Onyesho la Masala Festival,kama unavyomuona jukwaani akienda sambamba na ndugu zake Ngoma Africa! Onyesho hilo lilifunikwa na mzuka wa muziki wa dansi wa Tanzania!
Bendi ya Ngoma Africa ilikuwa na lengo moja tu kuwadatisha washabiki wake! na kuhakikisha kuwa muziki wa bongo unachukua nafasi ya mwanzo bila ya kuwa na mpinzani katika anga za kimataifa.
Buti Jiwe anafanyia shughuli zake nchini Uholanzi anapatikana
butijiwe@yahoo.com

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment