Hannover palikuwa hapatoshi! Ras makunja Na kikosi chake cha kutuliza ghasia Ngoma Africa band a.k.a FFU a.k.a wazee wa kukaanga mbuyu! siku ya jumapili 14-06-2009 jioni mzimu wa muziki wao wa dansi la bongo, ulifanikiwa kuziteka nyoyo za mashabiki katika maonyesho makubwa ya muziki ya kimataifa Masala World Beat Festival,mjini Hannover,Ujerumani.
Majira ya saa 12 jioni Ras Makunja a.k.a "Bw.Kichwa Ngumu" alikiongoza jukwaani Kikosi cha The Ngoma Africa band, kilichokuwa kimesheheni wanamziki washambuliaji akiwamo yule mchawi wa solo Christian Bakotessa a.k.a Chris-B, Pia kulikuwa na mwanamziki mgeni mwalikwa Mr.Buti Jiwe ambaye alikuwa (Guest Artist),wengine alikuwapo yule mwadada anayekwenda sambamba na wanamuziki wa kiume katika kushambulia jukwaa Dada Severn Onkomo aka Sevasha.
Kiongozi wa bendi hiyo Ebrahim Makunja a.k.a ras makunja alikiamrisha kikosi chake nacho bila kurembaremba kilijibu mashambulizi kwa kuporomosha muziki mkali ambao midundo yao ya bongo dansi aliwazidi nguvu mashabiki na dakika chache wakaanza kudatishwa kama si kudata ! na kujikuta wapo katika Kindumbwe Ndumbwe cha Kuitikia kwa sauti kila walipoamrishwa na Ras Makunja!
Wataalamu wa mziki na maporomota walikuwa roho juu kila mmoja akiwa anataka kufanya kazi na bendi hiyo ambayo imetajwa kuwa ni moja ya bendi za Africa Mahiri sana kwa sasa katika nchi za Ulaya, watayarishaji wa onyesho hilo wamesema haijawihi kutokea katika historia ya maonyesho hayo kwa "Mziki wa dansi wa kiafrika" kuwadatisha mashabiki kwa kiwango kubwa kiasi kile! wamesema muziki wa The Ngoma Africa Band una nguvu isiyo ya kawaida! labda kutokana na midundo yake na jinsi wanamuziki wanavyojua kushambulia jukwaa kupanga vyema sauti, vyombo na jinsi wanavyocheza na kuwafanya mashabiki wasiweze kulala!
Bendi hiyo maarufu kwa tabia za kuwatia kiwewe washabiki wake huko ulaya kwa kutumia muziki wa dansi wa Tanzania,
Bendi hiyo imejikuta ina nafasi ya pekee katika ushindani wa muziki wa kimataifa.
Kwa sasa The Ngoma Africa inachukuliwa kama Klabu inayowaunganisha maelfu ya mashabiki kimataifa, kiongozi wa bendi hiyo Ras Makunja alikaliliwa akisema kuwa misheni na mtazamo wa Ngoma Africa band,kwa sasa si kuutangaza muziki wa dansi wa bongo tu,bali pia kuhakikisha wanamuziki wa bongo dansi wanapata nafasi ya kimataifa kwa kupitia bendi ya The Ngoma Africa,kamanda huyo wa The Ngoma Africa band.
Bendi hiyo ipo katika medani ya dansi kwa muda wa miaka 16, na imefanikiwa kulitangaza dansi la bongo na kujinyakulia nafasi ya pekee kimataifa.
wasikilize hapa www.myspace.com/thengomaafrica pia ukiwataka wasiliana nao kwa: http://de.mc588.mail.yahoo.com/mc/compose?to=ngoma4u@ngomaafrica

1 comments:
ngoma africa utafikili hawana hakili nzuri
Post a Comment