CAMERA YA FULLSHANGWE INAKULETEA MATUKIO YA ONYESHO LA MAVAZI LA "LADY IN RED" KATIKA PICHA!!

Hapa ni kama anasema Du Mwanamke huyu ana mabo makubwa!!
Mama Asia Idarous akiwa na Mumewe mara baada ya maonyesho ya mavazi kumalizika jana kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski, maonyesho hayo yalishirikisha wabunifu wengi wa mavazi wakiwemo Asia mwenyewe Mustafa Hassanali, Ally Remtulla Zamda George, Farha Disgner Khadija Mwanamboka na wabunifu wengine wengi chipukizi burudani ilikuwa ni kikundi cha ngoma za asili Simba Thietre bendi ya B. Band, onyesho hilo lilidaminiwa na makampuni kadha kama vile kampuni ya Bia TBL kupitia kinywaji cha Redds kampuni ya vipodozi na nywele Darling, kampuni ya simu za mkononi Zantel, New Habari Cooparation, NICE magazine, Televisheni ya Chanel Ten na mengine kwa, matukio zaidi ya picha shuka chini upate uhondo mdau.
Miss Universe Miriam Odemba na zawadi yake ya maua akiyokabidhiwa jana baada ya maonyesho hayo pale Kilimanjaro Kempiski Hotel kulia ni Mercy Garabawa.
Simba Thietre kwa kupuliza filimbi kutumia pua ndiyo wenyewe ukiwahitaji waone pale Numba ya Sanaa.

Miss Universe Miriam Odemba naye alionyesha cheche zake katikakuonyesha mavazi.



Mbunifu Khadija Mwanamboka katikati na mashati aliyobuni.
Mbunifu Zamda George katikati na Mavazi aliyobuni.
Mbunifu Ally Remtulla na mavazi aliyobuni.



Mambo ni jukwaani sasa.

Kulia ni Matukio chuma aliwahi kuwa Mr. University Mbunifu wa mavazi Khadija Mwanamboka kati na Fidelin

Hapa ni kama anasema mh jamani Jarida la Nice zuri!!

Kutoka kushoto na Albert Makoye wa kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga wa kamati ya Miss Tanzania na My wife wake na Richard mshindi wa Big Brother II na my waife wake wakiwa ametulia kimya kabala ya onyesho kuanza.

Mwitikio wa watu katika fani ya maonyesho ya mavazi nchini unazidi kushika kasi kama unavyoona wapenzi na washabiki wa mitindo ya mavazi nchini wanaongezeka kila kukicha katika maonyesho hii ni dalili njema kwa fani nzima ya mambo yanayohusiana na mavazi


Mamaa Fidelin Iranga kati na washkaji zake.

Wabunifu wa mavazi Farha na Ally Remtulla katika pozi la shangwe unawaonaje mdau? kazi kwako.


Mh haya sasa hapa Camera ya FULLSHANGWE iliwafuma dada Fina na kaka Mwinyi wa jarida Jipya kabisa la NICE amabalo sasa hivi toleo lake la kwanza tayari liko mtaani.
Hata kupozi kwenye Camera pia kunahitaji ubunifu na mitindo kama unavyowaona wakongwe hawa Asia Idarous na Mustafa Hassanali katika fani ya ubunifu wa Mavazi

Hili ndilo Vazi la khanga alilokuwa amejipigilia mbunifu wa mavazi Farha hebu mcheki madau!
Hapa Bazo akifanya mahojiano na msanii Joan huku Mwanamitindo maarufu nchini Fidelin Iranga akisubiri muda wake ufike apate kumwaga sera zake kuhusiana na mambo ya mitindo.

Crew ya Televisheni ya TBC ilifanya mabo makubwa kama unavyoona vijana wake Heri Kissoky aliyesimama na Camera Adrian aliyechuchumaa chini na Camera huku mtangazaji Bazo Komu akifanya mahojiano na Yvonne aliyewahi kuwa Miss Ubungo hapa ni kama anamuuliza "umenunua wapi hiki kiatu chako"?.

Naye John wa Valley Spring na kushoto na dugu zake hawakutaka kupitwa na mambo ya Lady in Red.
Mamaa Asia Idarous kulia akitoa maelekezo kwa Mc wa onyesho hilo Salma Msangi wa Chanel Ten huku mbunifu Ally Remtullah akiwaangalia.
Kutoka kushoto ni Sara wa http://www.angaliabongo.blogspot.com/ mbunifu Fatama Amour mbunifu Mustafa Hassanali na Asma makau nao hawakusita kuja kuona mambo makubwa ya Lady in Red pale Kilimanjaro Kempiski Hotel.

Banana Zorro na Siz Azizi wanamuziki wa B. Band walikuwepo kwenye onyesho hilo tayari kwa kufanya vitu vyao.
Wadau kutoka kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga kati na my wife wake na kushoto ni Albert Makoye mkuu wa Itifaki.
Wadau wa mitindo kutoka kushoto George Kavishe wa Meneja wa Redds Bosco Majaliwa katibu mkuu kamati ya Miss Tanzania Richard mshindi wa Big BrotherII na mdau mwingine kutoka Miss Kinondoni

RIPOTI JUU YA UANDISHI WA HABARI ZA VIJIJNI, UMASIKINI, SAYANSI NA UTAFITI YAZINDULIWA!!

Mkurugenzi wa kituo maalum cha utafiti wa vyombo vya habari Bw. Ayubu Ryoba akizungumza mbele ya wanahabari wakati wa uzinduzi wa Ripoti tatu tofauti zinazoonyesha jinsi ya kuandika habari za umasikini , habari za Vijijini na Habari za Sayansi na Utafiti kwenye kukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo nanayefuatia ni mgeni rasmi katika uzinduzi huo na mwenyekiti wa kituo maalum cha machapisho ya utafiti wa vyombo vya habari Prof. Juan Mwaikusa na mwisho ni katibu mtendaji wa baraza la habari Bw. Kajubi Mukajanga

Mgeni rasmi Prof. Juan Mwaikusa mwenyekiti wa kituo maalum cha machapisho ya utafiti vyombo vya habari akionyesha moja vitabu alivyovizindua jinsi ya kuandika habari za Umasikini, habari za vijijini na habari za Sayansi na Utafiti katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo kushoto kwake ni Kajubi Mukajanga katibu mtendaji Baraza la habari na kulia ni Ayubu Ryoba Mkurugenzi wa kituo maalum cha utafiti wa vyombo vya habari na mwisho ni John Mirenyi meneja uchapishaji na na utafiti baraza la habari.




Hivi ndivyo vitabu Vitatu maalum vyenye ripoti ya utafiti jinsi ya kuandika habari za Umasikini , Habari za Vijijini na Habari za Sayansi na utafiti vilivyoandaliwa kwa pamoja na Kituo cha utafiti wa vyombo vya habari na Baraza la habari ripoti hizo zimezinduliwa leo kwenye ukumbi wa Idara ya habari maelezo.

STARNDARD CHARTERED BANK YAZIDI KUMWAGA UDHAMINI RT!!

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Starndard Chartered Jeremy Awori Kushoto akikabidhi bendera ya Taifa kwa wanariadha Andrea Silvin Chulo na Aisha Rajab Mathia wakati wanariadha hao walipokabidhiwa tiketi za ndege za kwenda Hong Kong na kurudi nchini Andrew na Aisha wanakwenda Hong Kong kushiriki mbio za Hong Kong Greatest Race on Earth 2009 ambapo watakimbia mbio za Starndard Chartered Hong Kong Marathon zitakazofanyika Febuari 8 jumapili, wa pili kutoka kushoto ni katibu mkuu wa Chama cha Riadha nchini RT Bw. Suleman Nyambui, wanariadha hao wanakwenda kwenye mashindano hayo kwa udhamini wa Benki hiyo.
Wanariadha wawili Aisha Rajab Mathia kushoto na Andrea Silvin Chulo wakiwa wamejifunika Bendera ya Taifa mara baada ya kuongea na wanahabari katika makao makuu ya Benki ya Starndard Chartered kuhusu kushiriki kwao katika mbio za Hong Kong Greatest Race on Earth 2009 Benki hiyo pia imedhamini mbio hizo ambapo wanariadha hao watashiriki mbio za Starndard Chartered Hong Kong Marathon zitakazofanyika Jumapili Februari 8

MKUBWA FELLA AJA NA DAWA YA 2009, YAANZA KUPIGWA REDIONI!!

Mkubwa Fella akiwakilisha

Kundi la muziki wa kizazi kipya la TMK WANAUME FAMILY hatimaye limemtoa Meneja wao anayejulikan kwa jina la Mkubwa Fella, Meneja huyo ameamua kutoka na Albam yake inayokwenda kwa jina la (2009) Fella ameamua kusema kutokana na yanayoongelewa juu yake mara wasanii wakundi hilo wanapoamua kujitenga kwani wamekuwa wakiongea mambo mengi ya kumshutumu pasipokukumbuka au kuongelea hata zuri moja ambalo kiongozi wao huyo amewafanyia.
Mkubwa Fella anasema mimi nimewafanyia mengi hawa watoto wanaoondoka kundini na kunishutumu lakini hata hivyo nimeona kuwa hawa wasanii hawatanikumbuka kwa lolote hivyo nikaona nitoe nyimbo yangu ambayo itaifanya jamii inikumbuke daima kutokana na nyimbo hiyo ambayo nimezungumza mengi na natumaini mashabiki wa muziki wa bongofleva watanisikia.


Fella amesema nyimbo hiyo imerekodiwa na mtayarishaji maarufu hapa nchini ambaye ni Henrco wa Soundcrafters Record kule (Kiumeni) yaani Temeke, anasema katika nyimbo hiyo amemshirikisha msanii wa siku nyingi kutoka kundi la Big Dog Pose (BDP)Drez Chief ambaye anamuelezea kuwa amekamua vilivyo katika nyimbo hiyo.
Anaongeza kuwa nyimbo hiyo tayari imeshasambazwa katika vituo vyote vya Redio hapa nchini na baadhi ya vituo vilitarajiwa kuanza kuirusha hewani leo hivyo mashabiki wa muziki huu wakae mkao wa kuusikiliza ujumbe wangu kwao na hao watoto wanaosema eti mimi nimewanyonya sana.
Amemaliza kuwa Video ya nyimbo hiyo nayo iko tayari na imetengenezwa na Isangi Production hivyo katika muda mfupi ujao nayo itaanza kusambazwa katika vituo Vya Televisheni tayari kwa kuicheza, FULLSHANGWE tunakukaribisha kwenye gemu mkubwa Fella kama ilivyozoeleka kukuita hivyo ila Gemu ni tafu inabidi kukomaa kwelikweli.

Kundi la TMK WANAUME FAMILY lilimeguka mwaka jana na kuzaa kundi linaloitwa TMK WANAUME HALISI linaoongozwa na Mkali Juma Nature na hatimaye mwaka huu tena wasanii watatu Jebi, Y. Dash, na Y.P wamejitoa na kutangaza kuunda kundi lao linaloitwa TMK UNITY hata hivyo TMK WANAUME FAMILY liliobakia na vichwa vitatu Mh. Temba, KR Mulla na Chege linaonekana bado liko imarapengine ni kutokana na wasanii waliobaki kuonekana wenye uwezo mkubwa katika kundi hilo ukiacha Msanii Juma Nature ambaye ameonyesha bado ana uwezo binafsi kama yeye na si kama kundi la TMK WANAUME HALISI.

MWANASARAKASI YOGAYOGA ATAMBA NCHINI UJERUMANI!!

Msanii wa Kitanzania Michael Elias (Yogayoga) kulia anayefanya kazi zake nchini Ujerumani akiongea na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa WMCA wakati alipokuwa kakielezea mafanikio yake kisanii nchini humo na mipango yake hapa nyumbani kushoto ni Ally Kyelula (Dj Ally Coco), Yogayoga amesema anatarajia kujenga kituo cha utamaduni hapa nyumbani katika mkoa wa Dodoma katika kukuza zaidi kiwango cha sanaa ya kitanzania ili tupate wasanii zaidi wa kimataifa kutoka hapa nyumbani kama alivyo yeye hivi sasa,

Yogayoga alizaliwa mwaka 1978 Wilayani Mpanda katika mkoa wa Rukwa na alianza shule ya msingi mkoani humo mwaka 1987 na baadae mwaka 1989 alihamia mkoani Dodoma ambapo alisoma shule ya msingi ya Majengo na kumalizia elimu ya msingi shuleni hapo baadae alijiunga na shule ya Sekondari Mazengo alisoma hapo kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha tatu, lakini alishindwa kuendelea na masomo na kujiunga na vikundi vya mchezo wa Sarakasi, aliendlea na michezo hiyo na kufanya kazi na wasanii tofauti kama vile Saida Karoli na Wanne Star ilipofika mwaka 2007 aliondoka kwenda nchini Ujerumani kwa ajili ya maonyesho ya Sarakasi na kujiendeleza zaidi kimasomo ambapo kwa sasa ameungana na wasanii mbalimbali wa nchi za kiafrika na wamekuwa wakifanya maonyesho katika nchi tofauti za Ulaya na Marekani huku akiendelea na masomo ya kutengeneza vipindi na uongoza ji wa Filamu FULLSHANGWE inampa Bravo Yogayoga kwa juhudi zake hizo na inamtakia mafanikio mema kwa picha zaidi shuka chini mdau.
Hii ni Staili ya kupiga simu huku ukiwa umekaa kwa pozi kama hili.

Hapa msanii Michael Elias Yogayoga alisema anatoa staili hiyo ya sarakasi kama salamu kwetu wana habari wote.

NORA AMWAGA CHOZI MBELE YA WANA HABARI!!

Hapa anaonekana akiendelea kujifuta machozi kwa uchungu hata hivyo FULLSHANGWE inatoa ushauri wa bure kwa dada Nora kuwa hizi ndiyo Gharama za Umaarufu mtu ukiwa maarufu utatupiwa kila jambo hata neno kidogo litakuwa kubwa hivyo mtu maarufu unahitajika kuwa Jasiri, Mvumilivu mwenye hekima na upeo wa kupambanua mambo unayokumbana nayo kabla ya kukata tamaa na hasira na kupelekea kufanya maamuzi ambayo yanaweza kukugharimu zaidi katika maisha yako ya Umaarufu wako hivyo dada Nora sisi tunakupenda na tunakutakia kila mafanikio katika Shughuli zako za uigizaji, wadau hii imetokea katika mkutano wa waandishi wa Habari na Kampuni ya BEKNET iloyokuwa ikizungumzia uzinduzi wa Filamu yake inayoitwa Upande wa pili wa ndoa Isiyo na uaminifu utakaofanyikaCentury Cinemax Hall 1 chuo kikuu cha Dar-as alaam Ijumaa wiki hii ambapo kiingilio kitakuwa shilingi 5000 tu wote mnakaribishwa, kwa habari zaidi na picha shuka chini mdau.
Hali bado iliendelea kuwa ngumu kwa Nora kama unavyomuona katika picha hii akijifuta machozi huku wasanii wenzie wakiwa wametulia tuuli kulia ni Mzee Chilo na kushoto ni Elizabeth Chijumba.

Kama unavyomuona Mzee Chilo akijaribu kumtuliza Nora lakini hata hivyo alishindwa kuzuia machungu yake na kuendelea kulia kitu kilichopelekea kipindi Cha maswali kukoma na kuanza kipindi kingine cha kutoa Maoni ambapo waandishi kadhaa walitoa maoni yao kwa wasanii hao

Alijibu kwa kifupi kuwa hajui! wakati akiendelea kujibu alishindwa kuendelea na kuanza kububujikwa na machozi na kusema nashindwa hata kuongea lakini hata hivyo alionekana bado ana hamu ya kulijibu vizuri swali hilo japokuwa mmoja wa waigizaji wa kundi hilo Ahmed Olotu Mzee Chilo alimshauri atulie na kuachana na swali hilo.
Hali ilianza kubadilika hapa wakati mmoja wa waandishi wa habari alipomuuliza Nora kutokana na habari za kashfa ambazo zimekuwa zikimtuhumu muigizaji huyo juu ya mapenzi na wanaume tofauti kama unavyomuona Nora akisikiliza kwa makini swali hilo.
Alikuwa akisikiliza kwa makini maelezo ya mkurugezi wa BEKNET wakati akiongea juu ya uzinduzi wa filamu yao ambayo Nora ni mmoja wa waigizaji walioigiza katika filamu hiyo.
Hapa Muigizaji Nora alikuwa ni mwenye furaha kabisa kabla mkutano na waandishi wa habari haujaanza na hata ulipoanza.

BEKNET KUZINDUA FILAMU YA UPANDE WA PILI WA NDOA!!


Mkurugenzi wa BEKNET Bariki Keenja akizungumza na waandishi wa habari leo juu ya uzinduzi wa Filamu ya Upande wa pili wa Ndoa isiyo na Uaminifu unaotarajiwa kufanyika tarehe 6 FebruaryCentury Cinemax Hall 1 Chuo kikuu cha Dar- es alaam ambapo kiingilio kitakuwa shilingi 5.000 kwa kila mtu, katikati ni Gerrad Simbila muongozaji wa filamu hiyo na kushoto ni mmoja wa waigizaji Elia David Sinior

MABONDIA WA TANZANIA KUPANDA ULINGONI JIJINI NAIROBI FEB.7!!

Kiongozi wa msafara wa mabondia wa Tanzania wanaokwenda Nairobi Kenya kwa mapambano kadhaa ya ngumi Bw Ally Bakari akielezea maandalizi na safari yao kwa ujumla na matumaini yake kwa mabondia Omary Ramadhani, Venance Mponji, na Rashid Ally mabondia hao wamealikwa na Kenya Professional Boxing Comission.
Mabondia Omary Ramadhani kutoka kulia, Venance Mponji na mwisho Rashid Ally wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa msafara Bw. Ally Bakary (Champion) katikati wakati walipokutana na wanahabari Idara ya habari maelezo mabondia hao wanatarajiwa kuondoka kesho kwenda kenya kwa mapambano yasiyo ya ubingwa ambapo Omary Ramadhani atapambana na Morris Chule wa kenya pambano la Round 8, Venance Mponji atapambana na Samuel Kamau Round 8 na Rashid Ally atapambana na Nzan Round 6 mapambano hayo yote yatafanyika jijini Nairobi jumamosi 7 February


ZOMBE NA WENZAKE MAHAKAMANI TENA LEO!!

Mmoja wa watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya wafanya biashara watatu kutoka mkoani morogoro Bw. Abdallah Zombe kushoto akiwa katika mahakama kuu leo kabla ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa kulia ni askari magereza akiimarisha ulinzi mahakamani hapo, Zombe alitarajiwa kuanza kuwasilisha ushahidi wake leo.

THT YATOA ELIMU YA UKIMWI MASHULENI!!

Wasanii wa kikundi cha Tanzania House of Talent (THT) wakionyesha sanaa ya maigizo ya jinsi ya kupambana na maambukizi dhidi ya maradhi ya UKIMWI katika hafla iliyodhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania na kufanyika Shule ya Sekondari Jangwani, Dar es Salaam wikiendi.

ONYESHO LA MAVAZI LA MALKIA 2009 KUFANYIKA TAR.7 FEBRUARY!!

Mustafa Hasanali akisisitiza jambo wakati akiongea na wanahabari Idara ya Habari Maelezo leo juu ya onyesho la Malkia litakalofanyika tarehe 7 February Little Theatre Club jijini kulia kwake ni meneja uhusiano wa serengeti Breweries Teddy Mapunda.
Mbunifu wa mavazi Mustafa hasanali akiongea na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa idara ya habari maelezo juu ya onyesha la Malkia linalotarajiwa kufanyika tarehe 7 February Little Theatre Club jijini kulia ni meneja uhusiano wa kampuni ya bia Serengeti Teddy Mapunda na kushoto ni meneja uhusiano wa kampuni ya simu Zain Beatrice Singano wa mwisho kulia ni Bahati Singh kutoka motomedia.

Mustafa Hassanali akipozi katika picha na wadau wake wakubwa katika onyesho lake hilo la Malkia kulia ni Teddy Mapunda Meneja uhusiano wa kampuni ya bia ya Serengeti ambao wamedamini onyesho hilo kupitia bia ya Stella Artois na kushoto ni Beatrice Singano Meneja uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya Zain ambao pia ni wadhamini wa onyesho hilo.

ONYESHO LA MALKIA
Kwa walio wengi siku ya muhimu sana katika maisha ni siku ya ndoa au siku ya Harusi, ni siku inayokutanisha nyoyo mbili tofauti za watu wawili tofauti kwa pamoja na familia zao kwa sababu ya kusherehekea na kula mapochopocho ambayo roho inapenda baada ya miezi isiyopungua sita ya maandalizi mazito ili kuhitimisha harusi rasmi.
Harusi siyo harusi bila mavazi ya aina yake hivyo Mustafa hasanali mbunifu maarufu wa mavazi hapa nchini atafanya onyesho la mavazi ya harusi tarehe 7/2/2009 pale little Theatre Club karibu na ST. Peter Oysterbay, mustafa ni ameshabuni mavazi tofauti ya harusi mbalimbali na hivi sasa anakuja na kitu cha kipekee kwa Bi. harusi mtarajiwa ili kumuandaa kuhitimisha siku hii ya muhimu kabisa.
Pamoja na misukosuko ya kibiashara duniani maisha lazima yasonge mbele na hasa katika dunia yetu maridhawa ambapo ili mteja aweze kupata kitu kizuri zaidi lazima agharimie hivyo Zain, Stella Artois na MOTOMEDIA watafanikisha onyesho la Malikia kwa udhamini wao mzuri kwetu waandaaji wa onyesho la Malkia.
Iwe ni Ktchen Party Send Off au harusi yenyewe bila shaka mwanamke wa kisasa atapatachaguo la mavazi ya harusiya kipekee kutoka hapahap nyumbani kwa kuwa hakuna kisichowezekana - pamoja tunaweza

WAFUGAJI WA KIMASAI WALALAMIKIA KUNYANYASWA NA H. WILAYA YA KIROMBELO!!

Bw. Manget Motio mmoja wa wafugaji waliofika jijini kutoka kijiji cha Mabwegere na kuongea na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa Idara ya habari maelezo akielezea kile wafugaji hao walichodai kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kirombelo imekamata mifugo yao na kuwahamisha kwa nguvu katika vijiji vyao hivyo kupelekea adha kubwa kwa familia zao lakini pia hawana pa kwenda kwani wao wamezaliwa katika maeneo na vijiji hivyo Wilaya ya Kirombelo.

Mama Ester Ngongodi ambaye ni mfugaji kutoka kijiji cha Godes Wilayani Kirombelo akiongea na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa idara ya habari maelezo leo kuelezea unyanyasaji wanaofanyiwa na Halmashauri ya wiliya hiyo ambapo inadaiwa watendaji wa wilaya wamekamata mifugo yao na kuwalazimisha kuhamia katika wilaya zingine kwa nguvu na kupigwa faini ya mifugo ya kwa kulipia kati ya Sh 30.000 na 45.000 kwa ng'ombe mmoja

TID AFANYA KWELI NA KUPAGAWISHA SWEATY EASY!!

TID ameonyesha uwezo na kipaji kwani kwa mara ya kwanza kundi lake la Top Band likiongozwa na yeye mwenyewe limefanya onyesho kabambe katika hoteli ya Sweaty Easy iliyoko Oysterbay jijini TID alionyesha kuwa amekomaa kwani alifanikiwa kuteka nyoyo za mashabiki vilivyo ambapo onyesho hilo lilihudhuriwa na Mastaa kibao wakiwemo Lady Jay Dee, Dully Sykes, mtangazaji wa Luninga ya East Africa Tv Maimartha wa Jesse mwigizaji Steve Nyerere mwanamuziki wa Akudo Impact Chritian Bella mtangazaji Gadner G habasha wa Clouds na wengine wengi na walionyesha kufurahia onyesho hilo TID ana albam tatu Sauti ya Dhahabu , Burudani na Nyota yako na hivi sasa anakuja na Albam ya nne inayokwenda kwa jina la Prison Voice
TID kushoto na Kuche wakikamua jukwaani ilikuwa si mchezo wadau kweli Top Band imerudi ili kuwapa washabiki shangwe.
Kundi la Top Band likifanya vitui vyao katika hoteli ya Sweaty Easy iliyoko Ostybay jijini TID bendi yake walifanya mambo makubwa mwishoni mwa wiki iliyopita kuanzaia kushoto ni Kuche, Kidawa na Ommy


Mbunifu wa mavazi Farha anayetunia nembo ya FNAAZ DISGNER akiwa katika pozi na Steve Nyerere hii ilikuwa katika onyesho la TID na Bendi yake inayojulikana kwa jina la Top Band
Muigizaji Steve Nyerere wa pili kutoka kulia akiwa pamoja na Maimartha Jesse mwenye kofia na Matukio Chuma kushoto kwa Steve Nyerere ni Zawadi.

MASHINDANO YA MISS EAST AFRIKA 2009 YAZINDULIWA BUJUMBURA!!

Muandaaji wa Miss East Afrika kulia na Bw. Lena Calist na na Miss East Afrika wakiwa Mjini Bujumbura hivi karibuni
MISS EAST AFRICA 2009
02/02/2009

* MASHINDANO YA MISS EAST AFRICA 2009 YAMEZINDULIWA RASMI JANA TAREHE 31/01/2009 JIJINI BUJUMBURA NA KUHUDHULIWA NA WATU MBALIMBALI MASHUHURI AKIWEMO RAIS MSTAAFU WA NCHI HIYO NDUGU PIERRE BUYOYA.

* AKITANGAZA RASMI TAREHE YA KUFANYIKA KWA MASHINDANO HAYO, MKURUGENZI WA RENA EVENTS LIMITED YA JIJINI DAR ES SALAAM AMBAO NDIO WAANDAAJI WA MASHINDANO HAYO, NDUGU RENA CALLIST, ALISEMA KWAMBA FAINALI ZA MASHINDANO YA MISS EAST AFRICA MWAKA HUU ZITAFANYIKA SIKU YA IJUMAA TAREHE 07/08/2009 JIJINI BUJUMBURA BURUNDI KUANZIA SAA 1:35 USIKU KWA SAA ZA BURUNDI (SAWA NA SAA 2:35 USIKU KWA SAA ZA TANZANIA.)

* HII ITAKUWA NI MARA YA PILI MFURULIZO KWA MASHINDANO HAYO KUFANYIKA NCHINI BURUNDI KUFUATIA MASHINDANO HAYO KUFANYIKA NCHINI HUMO MWISHONI MWA MWAKA JANA KWA MAFANIKIO MAKUBWA.

* MASHINDANO HAYO YANAFANYIKA TENA NCHINI HUMO KUFUATIA
OMBI LA RAIS WA BURUNDI NDUGU PIERRE NKURUNZIZA ALIYEMUOMBA MKURUGENZI WA RENA EVENTS NDUGU RENA CALLIST AKITAKA MASHINDANO HAYO YAFANYIKE TENA NCHINI BURUNDI BAADA YA KURIDHISHWA NA KIWANGO CHA HALI YA JUU CHA MASHINDANO YALIYOFANYIKA MWAKA JANA NCHINI HUMO AMBAPO YALIWEZA KUITANGAZA SANA NCHI YA BURUNDI HUSUSAN KATIKA NYANJA ZA KITAMADUNI NA KI UTALII.

* KATIKA MASHINDANO YA MWAKA JANA MREMBO CLAUDIA NIYONZIMA WA BURUNDI ALIIBUKA MSHINDI WA MASHINDANO HAYO NA KUJINYAKULIA GARI LA KISASA AINA YA LEXUS RX 300 LENYE THAMANI YA TSHS MILLIONI 35. MASHINDANO HAYO YALITIZAMWA “LIVE”NA WATU WANAOKADIRIWA KUFIKIA MILLIONO 200 DUNIANI KOTE KUPITIA NJIA YA INTERNET NA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISION AMBAPO YALIWEZA KUONYESHA SURA MPYA YA BURUNDI YENYE MATUMAINI MAKUBWA YA MAENDELEO YA KIUCHUMI BAADA YA KUMALIZIKA KWA VITA VILIVYODUMU KWA MUDA MREFU NCHINI HUMO.

* KATIKA UZINDUZI HUO RAIS PIERRE NKURUNZIZA ALISEMA
SERIKALI YAKE ITAMSAIDIA MREMBO CLAUDIA NIYONZIMA KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE KATIKA JAMII HASWA KATIKA KUSAIDIA WATOTO YATIMA; KATIKA HOTUBA YAKE ILIYOSOMWA KWA NIABA YAKE NA WAZIRI WA MASUALA YA AFRIKA MASHARIKI, MHESHIMIWA HAFSA MOSI,RAIS PIERRE NKURUNZIZA PIA ALIZIOMBA SERIKALI ZA NCHI WASHIRIKI KUMSAIDIA MREMBO HUYO KWA KUWA YEYE SASA NI BALOZI WA UTAMADUNI NA AMANI WA AFRIKA MASHARIKI. RAIS PIERRE NKURUNZIZA PIA ALISEMA KATIKA HOTUBA YAKE KWAMBA SERIKALI YAKE IWASAIDIA IPASAVYO WAANDAAJI WA MASHINDANO HAYO ILI KUHAKIKISHA KWAMBA YANAFANIKIWA KWA KUWA WAANDAAJI HAO WAMEAMUA KUCHAGUA TENA NCHI YAKE KUWA MWENYEJI WA MASHINDANO YA MISS EAST AFRICA 2009 NA KWAMBA HIYO NI HESHIMA KUBWA KWA NCHI YA BURUNDI

* NAYE RAIS MSTAAFU WA BURUNDI NDUGU PIERRE BUYOYA ALIIPONGEZA KAMPUNI YA RENA EVENTS LIMITED KWA KUENDESHA MASHINDANO YA MWAKA JANA KWA MAFANIKIO MAKUBWA NA KUMSHUKURU NDUGU RENA CALLIST NA KAMPUNI YAKE KWA KUAMUA KUFANYA TENA MASHINDANO HAYO NCHINI BURUNDI

* MASHINDANO YA MISS EAST AFRIKA MWAKA HUU YATAZISHIRIKISHA NCHI 14 ZA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI AMBAZO NI TANZANIA, BURUNDI, RWANDA, KENYA NA UGANDA. ZINGINE NI DJIBOUTI, ERITREA, ETHIOPIA, SOMALIA, PAMOJA NA VISIWA VYA MAURITIUS, COMOROS, RE UNION, MADAGASCAR NA SEYCHELLES.

* MISS EAST AFRICA KWA SASA NDIO MASHINDANO MAKUBWA YA UREMBO KATIKA UKANDA HUU WA BARA LA AFRIKA NA MWAKA HUU YANATARAJIWA KUTIZAMWA NA MAMILIONI YA WATU WENGI ZAIDI DUNIANI KUPITIA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISION NA INTERNET AMBAPO PAMOJA NA MAMBO MENGINE, MASHINDANO HAYO YANAKUSUDIA KUTANGAZA UTAMADUNI WA WATU WA AFRIKA MASHARIKI PAMOJA NA KUONYESHAVITUO MBALIMBALI VYA UTALII VILIVYO KATIKA ENEO LA AFRIKA YA MASHARIKI.

* SHEREHE ZA UZINDUZI WA MISS EAST AFRICA 2009 ZILIFANA SANA KWA KUPAMBWA NA BURUDANI MBALIMBALI PAMOJA NA “FIREWORKS” ZA UMBARI WA KILOMETA TANO JUU ANGANI AMBAPO MBALI NA RAIS MSTAAFU NDUGU PIERRE BUYOYA PAMOJA NA WAZIRI WA MASUALA YA AFRIKA MASHARIKI, WENGINE WALIOHUDHURIA SHEREHE ZA UZINDUZI WA MISS EAST AFRICA 2009 NI PAMOJA NA MAWAZIRI MBALIMBALI WA SERIKALI YA BURUNDI, NA MABALOZI WA NCHI ZA NJE WALIOKO BURUNDI IKIWA NI PAMOJA NA BALOZI WA MAREKANI NCHINI HUMO NA WAGENI WENGINE WENGI MAARUFU.


BY: RENA CALLIST,
BUJUMBURA, BURUNDI TEL: +255 755 755 755

Washindi wa Zain Lugalo Golf wakabidhiwa zawadi!!


Mratibu wa mashindano ya gofu kwa niaba ya Zain
Tanzania, Femin Mabachi (kulia) akikabidhi zawadi ya begi lenye
vifurushi vya Zain kwa mshindi wa watoto wa mashindano ya gofu ya
Zain/Lugalo Fiddle, Victor Joseph katika viwanja vya TPDF Lugalo, Dar
es Salaam mwishoni mwa wiki.

TOVUTI MPYA YA MALIPO YAANZISHWA!!


Hatimaye ile siku yetu ya kuwapa watanzania kitu kipya imewajia.
Tarehe1 February 2009 Tunapatia Watanzania Kitu kipya yaani Hisapepe.com
Tunaomba upendo na ushirikiano wako kuibadili Tanzania.
Nimeambatanisha Blog Post, tutashukuru ukiutaarifu umma wa kitanzania juu ya Hisapepe.com wajioungezee kipato kwa staili ya kipekee
Tuna banners nyingi tu unaweza kuzipata hapa:
http://www.hisapepe.com/images/banners/promo/index.php
Na kwa utaratibu wetu wa kujipatia pesa kwa link ya mwaliko basi zangati hatua hizi
1. Ingia hisapepe.com
2. Nenda sehemu ya Lipwa Kualika Na kisha “Automatically” utapata ID (referral link) ama URL yako ambayo kwa hiyo mfumo wa Hisapepe utakutambua
3. Unapoweka banner au link katika blog yako basi weka ID/referral link hiyo ili wanaokuja Hisapepe.com wahesabike kama wako na utajipatia kama tulivyokwishaeleza katika ule waraka wa awalii.
4. Unaweza kubadili posts na banners upendavyo, hatuna tatizo, zingatia kuweka link yako badala ya kuweka tu Hisapepe.com
5. Kwa sasa tayari kuna Sign Up Bonus Watanzania 1000 wa kwanza watajipatia pesa pale tu wanapingia

Muda wote nipo kwa maswali na nitafurahi sana kujibu hata utakayoulizwa na wanachama wadau wako usipoteze muda wako wewe waelekeze tu
katika kituo chetu cha Huduma Kwa Mteja cha juu kwa juu http://www.hisapepe.com/pages/swahili/contact.php
Huna haja ya kusign up kupata huduma kwa mteja unafika tu na kuanza kupata maelekezo toka kwetu.
Hisapepe inapatikana kwa Kiswahili na kiingereza, bonyeza bendera kuchagua lugha.
Nipo Online leo na kesho nzima na kuendelea walau kuwekana sawa, usisite kutuuliza au hata kwa simu ukikwama 0715 733 833
Sintasita kusisitiza kuwa kazi yenu inahusika sana, blogs ama magazeti tando ndio yatabadili fikira za wengiKazi njema, Tuibadili TanzaniaStella Badi Sales Representative, Hisapepe Company Limited, P. O. Box 33996, info@hisapepe.com http://www.hisapepe.com/