Maadhimisho ya mapinduzi ya Zanzibar yafana!!


Rais wa Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume akikagua gwaride wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 45 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Sherehe hizo zimefanyika jana katika uwanja wa michezo wa Gombani uliopo mjini Chakechake Pemba.
Picha na Anna Nkinda - Maelezo


12/DEC/2008. WANANCHI wameaswa kutumia ipasavyo rasimali zilizopo katika maeneo yanayowazungika, ili ziweze kuwainua kiuchumi na hatimaye kuondokana na umaskini miongoni mwao. Hayo yamesemwa jana Kisiwani Pemba na Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Amani Abeid Karume wakati wa kilele cha maadhimisho ya sherehe za miaka 45 ya mapinduzi Zanzibar ya tarehe 12 Dec 1963 Amesema kuwa katika miaka ya hivi karibuni pato la wananchi wa visiwa vya umguja na pemba imeendelea kukua na kustawi kwa haraka kutokana na mikakati madhubuti iliyowekwa na Serikali yake ikiwemo ya uborehsaji wa sekta za maendeleo katika makazi ya jamii. “Wananchi wa Zanzibar wana kila sababu ya kujivunia sura mpya ya maendeleo iliyopo nchini, na kutokana ni juhudi na ushirikiano wa pamoja uliopo kati ya Serikali na wananchi, na zaidi hali hii inajidhihirisha katika nyanja za uchumi na ustawi wa jamii” Anaongeza kuwa katika kipindi cha mwaka 2007, uchumi wa Zanzibar kama ilivyo kawaida na miaka ya nyuma uliendeklea kukua katika kasi ya kulidhisha ya kiwango cha asilimia 6.5 kwa mwaka ikiwa ni chini ya matarajio yaliwekwa ya asilimia 6.8 kwa mwaka. Anaitaja sababu iliyosababisha kutofikiwa kwa matarajio hayo ni kuongezeka kwa pato la taifa kutoka Tshs 510.0 Bilioni mwaka 2006 hafdi kufikia Tshsd 588.4 Bilioni mwaka 2007, wastani ambao ni mkubwa katika vigezo vya umaskini vilivyowekwa na Benki ya Dunia. Kwa upande mwingine Raisi Karume amesema kuwa ongezeko hilo limesababisha kuongezeka kwa wastani wa pato la kila mwananchi kutoka Tshs 458,867 sawa na Dola 367 mwaka 2006 hadi Tshs 518,000 ikiwa ni sawa na Dola 415 mwaka 2007, na akaongeza kuwa kwa mazingira ya hapa kwetu kiwango cha pato hilo bado kidogo. “Ukuaji huu wa uchumi umechangiwa zaidi na ukuaji wa sekta mbalimbali za maendeleo katika nchi yetu leo hii, hivyo bado natoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji mali kwani Serikali ipo nyuma yenu katika kutoa misaada itayohitajika” Anazitaja sekta hizo na viwango vyake katika mabano ni sekta ya huduma (43.9%), sekta ya kilimo (27.3%), sekta ya viwanda (15.4%), na sekta nyingine kwa ujumla zilichangia (13.4%) ya ukuaji wa pato la taifa. Kuhusu sekta ya huduma, Raisi Karume alisema kuwa katika mwaka 2007, Serikali ya mapinduzi Zanzibar imeinisha jumla ya miradi mipya ya maendeleo 62 inayojumuisha hoteli, mikahawa, maduka, na nyumba za kukodisha, ambapo miradi 20 tayari imekwisha anza kazi yake katika mikoa yote ya unguja na pemba. Aidha aliongeza kuwa mradi huo uliogharimu Dola za kimarekani Milioni 717.00 unatarajia kutoa ajira kwa wananchi 65,000 wa visiwa vyote viwili vya Unguja na pemba. Akizungumzia hali ya mtikisiko wa kiuchumi unaoikabili ulimwengu kwa sasa, Raisi Karume alisema kuwa kupungua kwa nafaka katika soko la dunia, kupanda kwa kasi isiyo ya kawaida ya bei za mafuta katika soko la dunia, pamoja na kuvurugika kwa mfumo na masoko ya fedha ni baadhi ya matukio makubwa yaliyoathiri mwenendo wa uchumi wa dunia Ameongeza kuwa upandaji wa bei za mafuta ulisababisha kuongezeka kwa gharama za maisha hasa kwa watu wa kipato cha chini na kati, hatua ambayo ilichangia kuporoka kwa uchumi wa katika nchi tajiri na maskini duniani. Kutokana na hatua hiyo, Raisi Karume aliongeza kuwa mataifa hayo tayari yamefanya jitihada mbalimbali za kujenga imani kwa sekta za uwekezaji nchini mwao, zoezi litakalochukua muda kupata ufumbuzi wa haraka katika masoko ya fedha. Alifafanua kuwa marekebisho ya sekta hizo katika nchi hizo, hayana faida yoyote kwa nchi maskini na badala yake itaendelea kuleta usumbufu na shida kwa wananchi wengi wa nchi maskini.. katika kukabiliana na changamoto hiyo, Raisi Kareume amesema kuwa Serikali yake imejipanga kikamilifu kuzuia adha hiyo ili isiweze kuwafikia wananchi kwa kujiwekea mikakati mbalimbali ikiwemo ya kuondoa kodi za ushuru kwa baadhi ya bidhaa za chakula ukiwemo mchele. “Wakuu wa nchi tajiri duniani kila wakutanapo katika mikutano yao mikubwa moja ya ajenda kuu wanazozijadili ni mustakadhi wa hali ya kiuchumi katika siku zijazo, hivyo nasi katika kujipanga na hilo hatuna budi kuimarisha vyanzo vyetu vya uchumi zikiwemo benki zetu” Katika kuimarisha kuimarisha na kuboresha sekta za rasirimali watu Zanzibar, Raisi Karume amesema kuwa miradi ya miundombinu mbalimbali imeimarishwa ili iweze kutoa huduma bora na salama kwa ustawi wa jamii ya wananchi wa visiwa vya unguja na Pemba. “Tunatambua kuwa ili mwananchi aweze kupiga hatua za kimaendeleo ni vyema awe na nyenzo imara zitazomwezeka kunufaikia na rasirimali zilizopo ni kama ardhi, maji na fedha ni vyema kwa Serikali ijiimarishe katika uboreshaji wa miundombinu” Raisi Karume anasema kuwa katika kipindi cha mwaka 2008, Serikali ya mapinduzi imeendelea kusimamia na kutekeleza malengo ya sekta mbalimbali zilizoathimiwa hapo awali ili kuboresha hali za wananchi vya Zanzibar. Katika kuimarisha sekta ya Afya, Raisi Karume alisema kuwa Serikali tayari imekwisha mashine mpya ya kisasa ya X-Ray yenye uwezo wa kubaini maradhi yaliyomo katika sehemu ya kichwa, kifua na tumbo, hivyo kuwapunguzia wananchi adha ya kupata athari zinazoweza kutibika kwa urahisi. “Mashine hiyo inatarajiwa kuanza kazi mwezi april mwaka huu, itafungwa katika hospitali ya Mnazi mmoja unguja, hivyo kupunguza shida na gharama za usafirishaji wa wagonjwa nje ya Zanzibar” Katika kuimarisha sekta ya Elimu Zanzibar, Raisi Karume alisema kuwa katika kuteleleza Sera ya Elimu ya Zanzibar serikali yake imeadhimia kufungua jumla ya shule za sekondari 21 katika kila Wilaya za mikoa ya pemba na unguja, ili kutoa fursa kwa vijana wengi waweze kuipata elimu hiyo bila ya usumbufu. “Wahisani wametusaidia katika nyanja ya elimu, kwa mfano Benki ya Kiarabu kwa maendeleo ya Afrika wametoa jumla ya Dola za kimarekani milioni 6 kwa ajili ya kujenga shule mbili huko kibuteni Unguja na mkanyageni pemba, hivyo ni jukumu lenu wazazi kuwapeleka watoto wenu mashuleni” Aidha aliongeza kuwa Serikali yake ina akiba ya vitabu vya sekondari 1,088,000 vilivyochapishwa, na vina uwezo wa kuhudumia wanafunzi wote wa Sekondari Zanzibar. Katika kuboresha sekta ya elimu ili iweze kwenda na wakati, Raisi Karume amesema kuwa Teknolojia ya habari na mawasiliano itasisitizwa kutolewa kwa wanafunzi na walimu wa Shule za Zanzibar ili wasiachwe nyuma na mabadiliko yanayotokea ulimwenguni kwa sasa. Katika sekta ya nishati, Raisi Karume alisema kuwa Serikali yake imedhamiria kuondoa tatizo la umeme kwa wananchi wa pemba, kwa kufufua mradi wa megawati 20 unaotegemewa kuanza kazi mwezi Desemba mwaka huu. Mradi huu wa umeme toka Tanga uliogharimu jumla ya Dola za kimarekani milioni 60, wenzetu wa serikali ya Norway wamejitolea kutupatia Dola milioni 37, huku sisi Serikali ya mapinduzi Zanzibar ikitoa Dola Milioni 7.5, unataraji unakuwa ni wenye manufaa katika kuboresha maisha na shughuli za maendeleo ya wananchi wa Zanzibar Mwisho kabisa Raisi Karume aliwaomba wananchi kuthamini jitihada na harakati za kimaendeleo zinazofanywa na Serikali katika kuboresha hali za maisha ya wananchi katika maeneo ya visiwa vyote viwili vya unguja na pemba. Sherehe hizo kwa mara yam kwanza katika kipindi cha miaka kumi iliyopita zimefanyika kisiwani pemba na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa akiwemo Raisi wa awamu ya pili, Alhaji Ally Hassani Mwinyi, Raisi wa Awamu ya tatu Raisi Benjamin William Mkapa, Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda, Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha, Naibu Waziri Kiongozi wa Serikali ya mapinduzi Zanzibar Ali Juma Shamuhuna, pamoja na mabalozi wanaowakilisha nchi zao kisiwani Zanzibar.

Basi la abiria kuteketea kwa moto Banana Ukonga!!

Baadhi ya wananchi wakiliangalia basi la abiria aina ya DCM lililoteketea kwa moto baada ya kuacha njia na kugonga nguzo za umeme zenye Transfoma na kusababisha mlipuko karibu na kituo cha daladala Banana- Ukonga .Ajali hiyo iliyotokea jana usiku haikuleta madhara kwa abiria waliokuwemo ndani ya basi hilo.

Mafundi umeme wa Shirika la Ugavi wa Umeme Nchini(Tanesco) wakiondoka eneo la tukio baada ya kuangalia uharibifu uliotokea.Eneo la Banana litaendelea kuwa gizani kwa kipindi kisichojulikana mpaka itakapofungwa transfoma nyingine kutokana na Transfoma iliyokuwa ikifanya kazi kuungua (Picha na Aron Msigwa -Maelezo)


STARAH THOMAS KUTOKA NA "NINI SINA"!!

Hili ndilo pozi la Starah Thomas mbele ya Camera ya FULLSHANGWE.
Starah Thomas akizungumza na FULLSHANGWE nyumbani kwake leo kulia ni mtoto wake wa kwanza Nicole na kushoto ni mtoto wake wa pili Jazz wakiwa na mama yao.

Mwanamuziki wa siku nyingi mwanamaa Starah Thomas yuko mbioni kutoa Single yake ya kwanza katika mwaka huu wa 2009 itakayokwenda kwa jina la (Nini Sina)baada ya kuwa kimya kwa kipindi kirefu akijipanga namna ya kutoka katika mwaka huu ambao ndiyo kwana tumeuanza.
Amesema nyimbo hii inaelezea mapenzi ya kweli katika ndoa ambapo mume na mke wanaelezana jinsi wanavyopendana kila mmoja kwa wakati wake, japokuwa mwanamke anakuwa na wasiwasi kwamba mbona sifa zimekuwa nyingi juu yake hivyo anaona labda anadanganywa.
Akiipasha zaidi FULLSHANGWE nyumbani kwake Stara amesema kwa kiasi kikubwa single hiyo imekamilika na itaanza kurushwa hivi karibuni katika vituo mbalimbali vya Radio, ameongeza kuwa nyimbo hiyo ambayo amemshirikisha mwanamuziki Chid Benz ameirekodi kwenye Studio ya 41 Records na producer ni Lamar.
Stara ameongeza kwamba sambamba na hilo pia sasa hivi anaendelea na programu ya kurekodi Video ya wimbo huo ambapo amesema nayo haitachukua muda mrefu itakuwa tayari kwa kusambazwa kwenye vituo vya Televisheni
Stara Thomas hakuishia hapo ameendelea kusema kuwa nanatarajia kukamilisha Albam yake itakayokuwa na nyimbo sita mwezi wa nne mwakahuu ili baada ya hapoazindue kuingiza sokoni anamalizia kwqamba katika Albam hiyo anataka mashairi ya nyimbo zake yaandikwe na wanamuziki kama Ngear, Q. Chilla na Ally Kiba.

MAISHA NI MAZURI LAKINI MAGUMU!!

Kutokana na ugumu wa maisha wanawake wengi jijini wamejitokeza katika kufanya biashara ndogondogo ili angalau kupata fedha kidogo za kujikimu kimaisha kama mwanamke huyu ambaye jina lake halikupatikana mara moja aliponaswa na Camera ya FULLSHANGWE akiuza maji ya chupa maeneo ya Kamata jana jijini huku jua likimpiga vyakutosha.

NAIBU WAZIRI WA MIUNDOMBINU ATEMBELEA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TCAA!!

Mkuu wa kitengo cha kuongoza ndege cha Mamlaka ya Usafiri wa anga Tanzania (TCAA) Bw Solomon Mwang’onda akitoa maelezo jinsi kitengo hicho kinavyofanya kazi kwa naibu waziri wa miundombinu Hezekiah Chibulunje jana wakati wa ziara yake jijini Dar es salaam.


Mkurugenzi wa masuala ya ufundi na Huduma wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania Bw. Suleman Said akitoa ufafanuzi kwa Naibu waziri wa Miundombinu Hezekiah Chibulunje kuhusu upanuzi wa uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Mwl. Julius Nyerere wakati wa ziara yake uwanjani hapo jana jijini Dar es salaam.
picha na Aron Msigwa wa MAELEZO


Sauti za Busara Festival Artists 2009

Iddi Achien'g
Kenya
Born in Nairobi, Iddi Achien’g was introduced to music by her mother who sang around her as she went about her daily chores. Growing up in a musical family, with a brother who played guitar and piano and sisters who sang in the church choir, she was exposed to music both in church and at home. It wasn’t long before she too joined the youth choir.
After school, while pursuing music and drama professionally, she met one of Kenya’s best renowned music producers and arrangers, Tabu Osusa. Impressed by her vocal prowess and stage command, he signed her onto the Nairobi City Ensemble as the lead and only female vocalist. Under his tutelage, she further sharpened her musical intellect.
She kicked off her solo career by recording and releasing her debut album, Thim Lich, earning a nomination at the Kisima awards in the afro-fusion category. Iddi has toured and performed at festivals and shows worldwide. In October of 2007 she was in Oslo, Norway, for the World Music Festival, and the Bergen International Festival. Iddi has performed in Djibouti, Sweden, Ethiopia, Tanzania and Uganda.
Iddi sings in Luo, her mother tongue as well as other languages including Kiswahili, Luganda, Dinka, Arabic and English. She sites her musical influences as Angelique Kidjo, Dobet Gnahore, Haddy Njie, Ogoya Nengo and Baaba Maal, among others. A socially conscious artiste, through her music Iddi addresses social issues with emphasis on co- existence, love, peace, freedom, development of African women and a deeper understanding and appreciation of her culture.
Currently in the process of recording her fifth album, Iddi Achien’g says her music style is termed as “afro-fusion contemporary benga” growing in popularity around the country and abroad. It is a fusion of traditional music interspersed with modern beats, styles and arrangements. The traditional instruments orutu, djembe, nyatiti always feature in her songs as heard on Thim Lich (the forest is an unpredictable place) It can be described as ‘A Truly Kenyan Sound’. Globalization is not all about economic standardisation. We should all make a pro active contribution to our diversity with an objective of appreciating the very best of one another’s culture.”

Mashindano ya Golf yafanyika Lugalo!!

Mchezaji gofu, Dennis Timoyebwa kipiga mpira Dar es Salaam
jana (Alhamisi Januari 8, 2009) wakati wa mashindano ya gofu ya Zain/Lugalo Fiddle
yanayorindima kila Alhamisi katika viwanja vya TPDF Lugalo, Dar es Salaam.

Mchezaji gofu, Raphael Letara (kulia) akikabidhiwa zawadi ya
mwavuli wa Zain na nahodha wa timu ya gofu ya Jeshi la Wananchi Tanzania
(JWTZ) ya Lugalo, Meja Samuel Hagu baada ya kuibuka mmoja wa washindi wa
mashindano ya gofu ya Zain/Lugalo Fiddle yanayorindima kila Alhamisi katika
viwanja vya TPDF Lugalo, Dar es Salaam jana.


SASA CLUB BILLICANAS NI SHANGWE TU!!

Waalikwa mbalimbali wakishangweka wakati wa Uzinduzi rasmi wa klabu ya Billicanas uliofanyika usiku wa kuamkia leo jijini klabu hiyo ilikuwa katika ukarabati mkubwa kwa muda mrefu picha kwa hisani ya IssaMichuzi.blogspot.com

ZAIN REWARDS PROGRAM YAZINDULIWA!!

Mkurugenzi Mtendaji wa Zain Tanzania, Khaled Muhtadi akionyesha katalogi yenye orodha ya zawadi za mabilioni ya fedha ambazo wateja wa Zain watapokea kwa kushiriki katika programu mpya ya Uaminifu, ‘Zain Rewardz Program’ iliyozinduliwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana (Januari 7, 2008). Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Zain Tanzania, Irene Mlola.


Mkurugenzi Mtendaji wa Zain Tanzania, Khaled Muhtadi (wa pili kulia) akionyesha katalogi yenye orodha ya zawadi anuwai za mabilioni ya fedha ambazo wateja wa Zain watapokea kwa kushiriki katika programu mpya ya Uaminifu, ‘Zain Rewardz Program’ iliyozinduliwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana (Januari 7, 2008). Kushoto ni Meneja Masoko wa Zain Tanzania, Costantine Magavilla, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Zain Tanzania, Irene Mlola na Tammy Whyman kutoka Kampuni ya Delta Partners.


BUSHOKE ADONDOSHA (DUNIA NJIA)!!

Albamu ya Dunia Njia ya mwanamuziki Bushoke iko tayari na itaanza kuuzwa rasmi madukani Jan 10, 2009. Itakuwa katika mfumo wa Tapes na CD. Kwa maulizo ya kibiashara, tafadhali piga simu na:+255 774 770077

Msanii Rutta Maxmilian Bushoke a.k.a Bushoke tayari amedondosha albamu yake yenye jina la Dunia Njia ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa burudani Bongo.Akipiga stori na ShowBiz, msanii huyo ambaye ni memba wa kundi la ‘Makole Hexagon’ alisema kwamba, albamu hiyo ambayo ilikuwa inafanyiwa kazi nchini China itadondoka kitaani Januari 10, mwaka huu ikiwa na ngoma zaidi ya 10, ‘Dunia Njia’ ikiwa ndiyo imebeba jina la santuri hiyo.“Ndani ya albamu hiyo kuna nyimbo kibao kali kama Chupa ya Coca, Nimeshafika ambao nimemshirikisha Ramso, Angel ft Mr. Blue, Nimekuchagua Wewe, Mapenzi Yaongee, Rain On Me niliowashirikisha Beron na Vampos, Dodoma, Hala, Wanashindwa Lala, na ‘Usiende mbali’ ambao ni wa Juliana wa Uganda,” alisema Bushoke.Aidha, mchizi amewataka mashabiki wake waisikilize albamu hiyo ili wapate kuona tofauti aliyoifanya kunako kazi zake za sasa badala ya yeye mwenyewe kujifagilia kwani moto mkali, habari kwa hisani ya http://www.abdallamrisho.blogspot.com/

WAZIRI NGELLEJA AZUNGUMZIA MAFANIKIO YA WIZARA YAKE KATIKA UTAWALA WA AWAMU YA NNE!!

Waziri wa Nishati na Madini William Ngelleja akiongea na waandishi wa habari leo (hawapo pichani) kuhusu mafanikio ya wizara hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu cha utawala wa awamu ya nne katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo. Kulia ni Naibu Waziri wa wizara hiyo Adam Malima akimsikiliza kwa makini, pata matukio zaidi katika picha chini.


Waziri wa Nishati na Madini William Ngelleja akiongea na waandishi wa habari leo (hawapo pichani) kuhusu mafanikio ya wizara hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu cha utawala wa awamu ya nne katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo. Huku Naibu (kulia) Adam Malima na Katibu Mkuu wa wizara hiyo (kushoto) Athur Mwakapugi wakimsikiliza kwa makini.

Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini pamoja na waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa wizara hiyo William Ngelleja (hayupo pichani) wakati akiongea na waandishi wa habari leo kuhusu mafanikio ya wizara yake kwa kipindi cha miaka mitatu cha utawala wa awamu ya nne katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.

MISS EAST AFRICA WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO!!

Mkurugenzi wa Lena Event na mwandaaji wa Miss East Afrca Bw. Lena Calist akizungumza na wanahabari kwenye hoteli ya Movenpick leo jijini wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano hilo lililofanyika nchini Burundi hivi karibuni ambapo mshindi wa kwanza amekabidhiwa gari aina ya Toyota Lexus. mshindi wa pili dola 5.000 na mshindi wa tatu dola 3.00 wanaofuatia kushoto katika picha ni Miss East Africa Claudia Noyimana, Balozi wa Burundi nchini Mh. Leandre Bagegwanubusa na mshindi wa tatu Rahwa Ghebrehuwet wa Eritrea kwa matukio zaidi katika picha shuka chini uweze kupata uhondo.
Balozi wa Burundi nchini Mh. Leandre Bagegwanubusa akizungumza mbele yawanahabari wakati alipokabidhi zawadi za washindi wa shindano la Miss East Africa lililofanyika jijini Bujumbura Burundi, katikati ni Miss East Africa Claudia Noyimana na mwisho ni mwandaaji wa shindano hilo Lena Calist.

Miss East Africa Claudia Noyimana akizungumza mbele ya waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Movenpick wakati wa kukabidhiwa zawadi yake ya gari mara baada ya kushinda taji hilo hivi karibuni nchini Burundi kulia ni mwandaaji na Mkurugenzi wa Lena Event Bw. Lena Calist.

Hapa Miss East Africa Claudia Noyimana akikabidhiwa Funguo za Gari lake aina ya Toyota Lexus linaloonekana nyuma yao na Balozi wa Burubdi nchini Mh. Leandre Bagegwanubusa kwenye Hoteli ya Movenpick leo katikati anayeangalia tukio hilo ni mwaadaaji na mkurugenzi wa kampuni ya Lena Event Bw. Lena Calist na maofisa mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo.

Miss East Africa Claudia Noyimana wa nne kutoka kulia akiwa pamoja na Balozi wa Burundi nchini Mh.Leandre Bagegwanubusa aliyeko mwisho kulia pamoja na mke wake na kushoto ni mwandaaji wa mashindano hayo Lena Calist pamoja na mshindi wa pili Annet John na mshindi wa tatu Rahwa Ghebrehuwet mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao kwenye Hoteli ya Movenpick jijini leo.

Baadhi ya maofisa wa kamati ya mashindano hayo yaliyofanyika nchini Burundi kutoka kulia ni John wa Valey Spring, Evans Bukuku wa Event lites,John Tall, Harrisday Mallango wa Eventlites na Bahati Singh.



Miss East Africa Claudia Noyimana wa Burundi katikati akiwa na mshindi wa pili Annet John kutokaTanzania kushoto na mshindi wa tatu Rahwa Ghebrehuwet wa Eritrea wakipozi mble ya Camera ya FULLSHANGWE katika viunga vya Hoteli ya Movenpick mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao.

NEW ZANZIBAR MOLDEN TAARAB YAENDELEA KUMWAGA RAHA JIJINI!!

Mwimbaji Mwamvita Shaibu wa New Zanzibar Molden Taarab akiongoza wenzake katika kuimba kwenye onyesho lililofanyika ijumaa mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa Equator Grill Mtoni kwa Azizi Ally.

Kundi la muziki wa Taarab la New Zanzibar Molden Taarab limeendelea kuwapa shangwe mashabiki wake katika kumbi mbalimbali za burudani ambapo katika muendelezo wa burudani hizo Camera ya Bwana FULLSHANGWE ijumaa hii iliwanasa katika ukumbi wa Equator Grill Mtoni kwa Azizi Ally jijini wakiwapagawisha mashabiki kama wanavyoonekana katika picha kutoka kulia ni waimabji Mwamvita Shaibu, Mwnamkuu Zayumba, Zena Mhamed na Zubeda Mlamali wakifanya vitu vyao

Chokoraa aanza 2009 kwa kumwaga damu!!


* Achanika kidevu, ang'oka meno mawili ukumbini

RAPAna mwimbaji nguli wa bendi ya muziki wa dansi ya African Stars 'Twanga
Pepeta International', Khalid Chuma 'Chokoraa', ameanza mwaka mpya wa 2009
vibaya, kwa kumwaga damu ukumbini.

Chokoraa alimwaga damu juzi usiku wakati Twanga Pepeta ilipokuwa ikitumbuiza
katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya 2009 kwenye ukumbi wa Triple A jijini
Arusha. Twanga ilitua Arusha baada ya mkesha wa mwaka mpya kupagawisha
mashabiki kwenye hoteli ya Safari Park jijini Nairobi, Kenya.

Akizungumza Dar es Salaam jana baada ya kurejea kutoka Arusha, Chokoraa
alisema aliumia vibaya na kupasuka chini ya kidevu, akang'oka meno mawili na pia
kupata maumivu sehemu za kifua baada ya kuteleza na kuanguka vibaya.

"Mwaka 2009 nimeuanza vibaya kwa kumwaga damu, Januari mosi majira ya saa 6
na ushei usiku kwenye shoo ya kufungua mwaka Arusha, katika mishemishe za
kupagawisha mashabiki nilikuwa nacheza shoo bize, nikatelekeza, nikafikia kifua na
kidevu, nikachanika na meno mawili kungo'oka," alisema Chokoraa.

Twanga Pepeta inayodhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania,
imerejea nchini jana (Ijumaa) na leo inatarajia kuwachengua mashabiki kwa staili zake
mpya za 'Sugua Kisigino' ya Saulo John 'Ferguson', 'Nimeokota Kidude' ya
Chokoraa na Weka Selo, Kitumbua mbona wauza usiku, Obama, Wizi Mtupu na
Mambo Maregea za Msafiri Said 'Diouf'.

Chokoraa alisema Twanga Pepeta itaangusha moja moja kwa kuporomosha nyimbo
mpya zinazotarajiwa kuwemo kwenye albamu ya 10 ya bendi hiyo itakayozinduliwa
mwaka huu ikiwa ni pamoja na Sumu ya Mapenzi ambao ni utunzi wake, Shida
Darasa na Mtoto wa Mjini (Charles Gabriel 'Chaz Baba') na Nazi Haivunji Jiwe
(Thabit Abdul).

WARATIBU MISS EAST AFRICA KUKUTANA NA WANAHABARI JUMAPILI!!

Rais Nkurunziza akiwa na washindi wa Miss East Africa 2008 ikulu Bujumbura muda mfupi baada ya kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu mashindano ya Miss Africa mwaka huu yaliyofanyika Bujumbura kwa mafanikio makubwa. kulia kwa Rais ni muandaaji wa mashindano hayo Mr.Rena Callist, na kushoto mkwa Rais ni Miss East Africa 2008 Claudia Niyonzima. wengine kutoka kushoto ni Serge Nkurunziza, mratibu wa Rena Events Limited Nchini Burundi, Mshindi wa Pili Anneth John wa Tanzania, na Rahwa Ghebrehiwet wa Eritrea.kushoto kwa Miss East Africa ni baadhi ya wanakamati wa mashindano hayo waandaaji watakutana na waandishi wa habari siku ya jumapili mahali pa mkutano na wakati watatoa taarifa zaidi

Zain Sarakasi Mama Afrika yasogezwa mbele!!

Wasanii wanaounda kundi la sarakasi la Zain Sarakasi Mama Afrika, wakionyesha umahiri wao wakati wa moja ya maonyesho yao Dar es Salaam juzi. Shoo hiyo ya sarakasi ya Zain iliyozinduliwa nchini Novemba 26, 2008, itaendelea kurindima hadi Januari 18, mwaka huu Dar es Salaam.