Maadhimisho ya mapinduzi ya Zanzibar yafana!!


Rais wa Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume akikagua gwaride wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 45 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Sherehe hizo zimefanyika jana katika uwanja wa michezo wa Gombani uliopo mjini Chakechake Pemba.
Picha na Anna Nkinda - Maelezo


12/DEC/2008. WANANCHI wameaswa kutumia ipasavyo rasimali zilizopo katika maeneo yanayowazungika, ili ziweze kuwainua kiuchumi na hatimaye kuondokana na umaskini miongoni mwao. Hayo yamesemwa jana Kisiwani Pemba na Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Amani Abeid Karume wakati wa kilele cha maadhimisho ya sherehe za miaka 45 ya mapinduzi Zanzibar ya tarehe 12 Dec 1963 Amesema kuwa katika miaka ya hivi karibuni pato la wananchi wa visiwa vya umguja na pemba imeendelea kukua na kustawi kwa haraka kutokana na mikakati madhubuti iliyowekwa na Serikali yake ikiwemo ya uborehsaji wa sekta za maendeleo katika makazi ya jamii. “Wananchi wa Zanzibar wana kila sababu ya kujivunia sura mpya ya maendeleo iliyopo nchini, na kutokana ni juhudi na ushirikiano wa pamoja uliopo kati ya Serikali na wananchi, na zaidi hali hii inajidhihirisha katika nyanja za uchumi na ustawi wa jamii” Anaongeza kuwa katika kipindi cha mwaka 2007, uchumi wa Zanzibar kama ilivyo kawaida na miaka ya nyuma uliendeklea kukua katika kasi ya kulidhisha ya kiwango cha asilimia 6.5 kwa mwaka ikiwa ni chini ya matarajio yaliwekwa ya asilimia 6.8 kwa mwaka. Anaitaja sababu iliyosababisha kutofikiwa kwa matarajio hayo ni kuongezeka kwa pato la taifa kutoka Tshs 510.0 Bilioni mwaka 2006 hafdi kufikia Tshsd 588.4 Bilioni mwaka 2007, wastani ambao ni mkubwa katika vigezo vya umaskini vilivyowekwa na Benki ya Dunia. Kwa upande mwingine Raisi Karume amesema kuwa ongezeko hilo limesababisha kuongezeka kwa wastani wa pato la kila mwananchi kutoka Tshs 458,867 sawa na Dola 367 mwaka 2006 hadi Tshs 518,000 ikiwa ni sawa na Dola 415 mwaka 2007, na akaongeza kuwa kwa mazingira ya hapa kwetu kiwango cha pato hilo bado kidogo. “Ukuaji huu wa uchumi umechangiwa zaidi na ukuaji wa sekta mbalimbali za maendeleo katika nchi yetu leo hii, hivyo bado natoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji mali kwani Serikali ipo nyuma yenu katika kutoa misaada itayohitajika” Anazitaja sekta hizo na viwango vyake katika mabano ni sekta ya huduma (43.9%), sekta ya kilimo (27.3%), sekta ya viwanda (15.4%), na sekta nyingine kwa ujumla zilichangia (13.4%) ya ukuaji wa pato la taifa. Kuhusu sekta ya huduma, Raisi Karume alisema kuwa katika mwaka 2007, Serikali ya mapinduzi Zanzibar imeinisha jumla ya miradi mipya ya maendeleo 62 inayojumuisha hoteli, mikahawa, maduka, na nyumba za kukodisha, ambapo miradi 20 tayari imekwisha anza kazi yake katika mikoa yote ya unguja na pemba. Aidha aliongeza kuwa mradi huo uliogharimu Dola za kimarekani Milioni 717.00 unatarajia kutoa ajira kwa wananchi 65,000 wa visiwa vyote viwili vya Unguja na pemba. Akizungumzia hali ya mtikisiko wa kiuchumi unaoikabili ulimwengu kwa sasa, Raisi Karume alisema kuwa kupungua kwa nafaka katika soko la dunia, kupanda kwa kasi isiyo ya kawaida ya bei za mafuta katika soko la dunia, pamoja na kuvurugika kwa mfumo na masoko ya fedha ni baadhi ya matukio makubwa yaliyoathiri mwenendo wa uchumi wa dunia Ameongeza kuwa upandaji wa bei za mafuta ulisababisha kuongezeka kwa gharama za maisha hasa kwa watu wa kipato cha chini na kati, hatua ambayo ilichangia kuporoka kwa uchumi wa katika nchi tajiri na maskini duniani. Kutokana na hatua hiyo, Raisi Karume aliongeza kuwa mataifa hayo tayari yamefanya jitihada mbalimbali za kujenga imani kwa sekta za uwekezaji nchini mwao, zoezi litakalochukua muda kupata ufumbuzi wa haraka katika masoko ya fedha. Alifafanua kuwa marekebisho ya sekta hizo katika nchi hizo, hayana faida yoyote kwa nchi maskini na badala yake itaendelea kuleta usumbufu na shida kwa wananchi wengi wa nchi maskini.. katika kukabiliana na changamoto hiyo, Raisi Kareume amesema kuwa Serikali yake imejipanga kikamilifu kuzuia adha hiyo ili isiweze kuwafikia wananchi kwa kujiwekea mikakati mbalimbali ikiwemo ya kuondoa kodi za ushuru kwa baadhi ya bidhaa za chakula ukiwemo mchele. “Wakuu wa nchi tajiri duniani kila wakutanapo katika mikutano yao mikubwa moja ya ajenda kuu wanazozijadili ni mustakadhi wa hali ya kiuchumi katika siku zijazo, hivyo nasi katika kujipanga na hilo hatuna budi kuimarisha vyanzo vyetu vya uchumi zikiwemo benki zetu” Katika kuimarisha kuimarisha na kuboresha sekta za rasirimali watu Zanzibar, Raisi Karume amesema kuwa miradi ya miundombinu mbalimbali imeimarishwa ili iweze kutoa huduma bora na salama kwa ustawi wa jamii ya wananchi wa visiwa vya unguja na Pemba. “Tunatambua kuwa ili mwananchi aweze kupiga hatua za kimaendeleo ni vyema awe na nyenzo imara zitazomwezeka kunufaikia na rasirimali zilizopo ni kama ardhi, maji na fedha ni vyema kwa Serikali ijiimarishe katika uboreshaji wa miundombinu” Raisi Karume anasema kuwa katika kipindi cha mwaka 2008, Serikali ya mapinduzi imeendelea kusimamia na kutekeleza malengo ya sekta mbalimbali zilizoathimiwa hapo awali ili kuboresha hali za wananchi vya Zanzibar. Katika kuimarisha sekta ya Afya, Raisi Karume alisema kuwa Serikali tayari imekwisha mashine mpya ya kisasa ya X-Ray yenye uwezo wa kubaini maradhi yaliyomo katika sehemu ya kichwa, kifua na tumbo, hivyo kuwapunguzia wananchi adha ya kupata athari zinazoweza kutibika kwa urahisi. “Mashine hiyo inatarajiwa kuanza kazi mwezi april mwaka huu, itafungwa katika hospitali ya Mnazi mmoja unguja, hivyo kupunguza shida na gharama za usafirishaji wa wagonjwa nje ya Zanzibar” Katika kuimarisha sekta ya Elimu Zanzibar, Raisi Karume alisema kuwa katika kuteleleza Sera ya Elimu ya Zanzibar serikali yake imeadhimia kufungua jumla ya shule za sekondari 21 katika kila Wilaya za mikoa ya pemba na unguja, ili kutoa fursa kwa vijana wengi waweze kuipata elimu hiyo bila ya usumbufu. “Wahisani wametusaidia katika nyanja ya elimu, kwa mfano Benki ya Kiarabu kwa maendeleo ya Afrika wametoa jumla ya Dola za kimarekani milioni 6 kwa ajili ya kujenga shule mbili huko kibuteni Unguja na mkanyageni pemba, hivyo ni jukumu lenu wazazi kuwapeleka watoto wenu mashuleni” Aidha aliongeza kuwa Serikali yake ina akiba ya vitabu vya sekondari 1,088,000 vilivyochapishwa, na vina uwezo wa kuhudumia wanafunzi wote wa Sekondari Zanzibar. Katika kuboresha sekta ya elimu ili iweze kwenda na wakati, Raisi Karume amesema kuwa Teknolojia ya habari na mawasiliano itasisitizwa kutolewa kwa wanafunzi na walimu wa Shule za Zanzibar ili wasiachwe nyuma na mabadiliko yanayotokea ulimwenguni kwa sasa. Katika sekta ya nishati, Raisi Karume alisema kuwa Serikali yake imedhamiria kuondoa tatizo la umeme kwa wananchi wa pemba, kwa kufufua mradi wa megawati 20 unaotegemewa kuanza kazi mwezi Desemba mwaka huu. Mradi huu wa umeme toka Tanga uliogharimu jumla ya Dola za kimarekani milioni 60, wenzetu wa serikali ya Norway wamejitolea kutupatia Dola milioni 37, huku sisi Serikali ya mapinduzi Zanzibar ikitoa Dola Milioni 7.5, unataraji unakuwa ni wenye manufaa katika kuboresha maisha na shughuli za maendeleo ya wananchi wa Zanzibar Mwisho kabisa Raisi Karume aliwaomba wananchi kuthamini jitihada na harakati za kimaendeleo zinazofanywa na Serikali katika kuboresha hali za maisha ya wananchi katika maeneo ya visiwa vyote viwili vya unguja na pemba. Sherehe hizo kwa mara yam kwanza katika kipindi cha miaka kumi iliyopita zimefanyika kisiwani pemba na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa akiwemo Raisi wa awamu ya pili, Alhaji Ally Hassani Mwinyi, Raisi wa Awamu ya tatu Raisi Benjamin William Mkapa, Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda, Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha, Naibu Waziri Kiongozi wa Serikali ya mapinduzi Zanzibar Ali Juma Shamuhuna, pamoja na mabalozi wanaowakilisha nchi zao kisiwani Zanzibar.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment