Baadhi ya wananchi wakiliangalia basi la abiria aina ya DCM lililoteketea kwa moto baada ya kuacha njia na kugonga nguzo za umeme zenye Transfoma na kusababisha mlipuko karibu na kituo cha daladala Banana- Ukonga .Ajali hiyo iliyotokea jana usiku haikuleta madhara kwa abiria waliokuwemo ndani ya basi hilo.
Mafundi umeme wa Shirika la Ugavi wa Umeme Nchini(Tanesco) wakiondoka eneo la tukio baada ya kuangalia uharibifu uliotokea.Eneo la Banana litaendelea kuwa gizani kwa kipindi kisichojulikana mpaka itakapofungwa transfoma nyingine kutokana na Transfoma iliyokuwa ikifanya kazi kuungua (Picha na Aron Msigwa -Maelezo)
0 comments:
Post a Comment