Hili ndilo pozi la Starah Thomas mbele ya Camera ya FULLSHANGWE.
Starah Thomas akizungumza na FULLSHANGWE nyumbani kwake leo kulia ni mtoto wake wa kwanza Nicole na kushoto ni mtoto wake wa pili Jazz wakiwa na mama yao.
Mwanamuziki wa siku nyingi mwanamaa Starah Thomas yuko mbioni kutoa Single yake ya kwanza katika mwaka huu wa 2009 itakayokwenda kwa jina la (Nini Sina)baada ya kuwa kimya kwa kipindi kirefu akijipanga namna ya kutoka katika mwaka huu ambao ndiyo kwana tumeuanza.
Amesema nyimbo hii inaelezea mapenzi ya kweli katika ndoa ambapo mume na mke wanaelezana jinsi wanavyopendana kila mmoja kwa wakati wake, japokuwa mwanamke anakuwa na wasiwasi kwamba mbona sifa zimekuwa nyingi juu yake hivyo anaona labda anadanganywa.
Akiipasha zaidi FULLSHANGWE nyumbani kwake Stara amesema kwa kiasi kikubwa single hiyo imekamilika na itaanza kurushwa hivi karibuni katika vituo mbalimbali vya Radio, ameongeza kuwa nyimbo hiyo ambayo amemshirikisha mwanamuziki Chid Benz ameirekodi kwenye Studio ya 41 Records na producer ni Lamar.
Stara ameongeza kwamba sambamba na hilo pia sasa hivi anaendelea na programu ya kurekodi Video ya wimbo huo ambapo amesema nayo haitachukua muda mrefu itakuwa tayari kwa kusambazwa kwenye vituo vya Televisheni
Stara Thomas hakuishia hapo ameendelea kusema kuwa nanatarajia kukamilisha Albam yake itakayokuwa na nyimbo sita mwezi wa nne mwakahuu ili baada ya hapoazindue kuingiza sokoni anamalizia kwqamba katika Albam hiyo anataka mashairi ya nyimbo zake yaandikwe na wanamuziki kama Ngear, Q. Chilla na Ally Kiba.
1 comments:
stara nakuomba sana uwafundishe wasichana maarufu hapo bongo wapunguze mapepe wakuige wewe,,maana umefahamika more than 10 years past lakini hatujawahi kusikia mambo ya hovyo kwa upande wako... Ni jukum lako da stara maana ni wadogo zako na wote nyie ni watu maarufu,,do this if u have time
Post a Comment