MSONDO WAWASAKA FM ACADEMIA KWA UDI NA UVUMBA!!

Hapa Roman Mg'ande akajitosa kuongeza burudani kwa mashabiki yaani ikawa ni kushangweka tu, wakati huohuo kundi hili kupitia kwa wanamuziki wake wakongwe Said Mabera na Roman Mg'ande wametamba kuwa wako tayari hata saa nane za usiku kupambanishwa na kundi la Fm Academia (watoto wa mujini) wameongeza kuwa wale ni watoto wadogo tu hawawezi moto wao kwani staili ya bendi yao ni tofauti kabisa na bendi hiyo inayopiga muziki wa asili ya kongo lakini kwa lugha ya kiswahili Mabera amesema wao wanapiga muziki wenye asili ya ngoma za wenyeji wa pwani ambao ni maarufu sana hapa nchini, kama kuna mtu anaweza kutukutanisha na ana hela hata saa sita za jua kali au usiku mkubwa tukiamshwa usingizini tutawaonyesha kazi ya msondo tu, kuna habari kuwa Fm Academia hawataki kukutanishwa na Bendi ya Msondo hata kidogo ila sababu ya kukataa bado haijajulikana pata matukio zaidi katika picha chini.
Rapa wa bendi hiyo Roman Mg'ande akighani huku akishangaa mtetemesho wa mnenguaji wa bendi hiyo mamaa Nzawisa wakati alipokuwa akitetemesha jukwaa.

Wadau Phil Mmari kushoto na Kocha Julio Arberto Pereira (Jamhuri Kihwelo) kati hawakuikosa burudani hiyo.

Wana muziki wa kundi zima la Mondo Ngoma Music Band likipagawisha mashabiki katika viwanja vya Leaders mwishoni mwa wiki iliyopita katika Bonanza linalofanyika kila wiki katika viwaja hiyvo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment