PATA MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA YALIYOJIRI LEO!!

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Capt. John Chiligati akiongea na waandishi wa habari leo kuhusu mafanikio ya wizara yake katika kipindi cha miaka mitatu ya utawala wa serikali ya awamu ya nne katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo jijini Dar es salaam ,Kushoto ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi wa wizara hiyo Bw Gerald Mango.

Mwenyekiti wa umoja wa Vijana CCM mkoa wa Arusha Bw. James Millya akiongea na wanahabari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo kuomba vyombo vya sheria vimchukulie hatua Mbunge wa Simanjiro Mh. Ole Sendeka kutokana na kitendo cha kumpiga kofi anachodaiwa kufanya mbuge huyo katika moja ya vikao vilivyofanyika mkoani humo hivi karibuni hata hivyo naye Mh. Ole Sendeka alifanya mkutano na wanahabari katika ukumbi huohuo akidai kushambuliwa na Bw. Millya, lakini habari zaidi zinapasha kuwa waheshimiwa hao ni ndugu yaani mtu na mjomba wake.
Wanyama wamesaidia kwa kiasi kikubwa kutatua tatizo la usafiri vijijini kama mdau Anna Nkinda katika picha hii iliyopigwa huko Pemba ikionyesha Watoto pamoja na mizigo yao wakiwa wamepanda mkokoteni unaokokotwa na ng’ombe majira ya jioni wakitokea Gombani kwenda Macho manne mjini Pemba. Wananchi wengi wa Pemba wamekuwa wakitumia usafiri wa ng’ombe kusafirisha mizigo yao.

Mvuvi ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akiwa anavua samaki kwa kutumia vifaa hafifu katikati ya bahari ya Hindi jambo ambalo linaweza kusababisha kuzolewa na mawimbi makubwa ya maji na kuhatarisha maisha wake.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment