RWANDA KUPATA WAWAKILI WA MISS EAST AFRICA 2009 JUMAMOSI!!



Hawa ni baadhi ya warembo wa Rwanda watakaowania kushiriki Miss East Africa 2009.

Warembo watakaoiwakilisha Nchi ya Rwanda katika mashindano ya kimataifa ya MISS EAST AFRICA 2009 watapatikana wiki hii katika mashindano yanayosubiliwa kwa hamu kubwa Nchini humo.
Mashindano hayo ya Rwanda yanaayoandaliwa na kampuni ya Rwanda Events Limited ya Nchini humo yatafanyika siku ya Jumamosi wiki hii jijini Kigali.
Washindi wawili wa mashindano hayo wataiwakilisha Nchi ya Rwanda katika fainali za mashindano ya MISS EAST AFRICA 2009 yatakayofanyika tarehe 18 Desemba, 2009 jijini Dar es salaam, Tanzania.
Wawakilishi wa Rwanda katika mashindano ya Miss East Africa mwaka jana yaliyofanyika Bujumbura, Burundi walikuwa ni Kaneza Brigitte na Idmulisa Dominique from RWANDA
Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu yanatarajiwa kushirikisha warembo 28 kutoka Nchi 14 ambazo ni pamoja na wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, na Burundi. Zingine ni Ethiopia, Eritrea, Djibouti, Somalia, Madagascar, Seychelles, Mauritius, Comoros, na Re union,
Mashindano ya Kimataifa ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Limited ya jijini Dar es salaam.
Wakati huohuo droo ya kila mwezi ya bahati nasibu ya Miss East Africa imefanyika jana na washindi kutangazwa. Washindi hao wa droo ndogondogo za kila mwezi wamejishindia zawadi mbalimbali zenye thamani ya shillingi million mbili ikiwa ni pamoja na pesa taslimu, simu za mkononi, ticketi za VIP za kuangalia fainali ya mashindano ya Miss East Africa, n.k.
Zawadi kubwa katika bahati nasibu hiyo inayoendelea Nchi nzima ni Gari aina ya Range Rover Sport, kutoka CMC Automobile Ltd. Ili kushiriki bahati nasibu hiyo unatakiwa kununua ticketi kutoka kwa wauzaji wa Magazeti Nchini, au kutuma SMS ya neno “SHINDA” kwenda namba 15567 kwa kutumia simu ya mkononi.

Tamasha la fiesta Tanga funika bovu!!

Wasanii kutoka kundi la Familia Chid Benz na Chiku wakilishambulia jukwaa la fiesta one love katika uwanja wa mkwakwani jijini Tanga usiku wa kuamkia leo
Prof Jay akiwapagawisha mashabiki wake vilivyo ndani ya uwanja wa mkwakwani katika tamasha la fiesta one love

SIMBA YAIBANJUA AZAM FC KWEUPEE HAPO SHAMBA LA BIBI!!

Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa pambano lao lililofanyika kwenye uwanja kwa Uhuru na Simba kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Azam Fc, kwa ushindi huo Simba inaendelea kuongoza ligi Hiyo ikiwa na pointi 27 na ikiwa imeshinda michezo yote 9 iliyocheza toka ilipoanza michuano ya ligi kuu ya Vodacom mwezi wa Agosti mwaka huu, na inatarajiwa kushuka dimbani tena kukutana na watani wao wa jadi timu ya Yanga ya jijini mchezo ambao unatarajiwa kupigwa oktoba 31 kwenye uwanja mkuu wa Taifa.
Kikosi Cha timu ya Azam Fc katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa pambano hilo.

Mwamuzi wa mchezo kati ya Simba Sports Club na Azam Fc akiwaeelekeza wachezaji wa simba kurudi katikati tayari kwa kuanza mpira wakati wachezaji hao walipokuwa wakishangilia goli lao lililofungwa na mchezaji wa Azam baada ya kubabatizwa na mpira wa kona uliopigwa na Mussa Hassan Mgosi.

Kocha wa Timu ya Simba Patrick Phiri akiongea na waandishi wa habari kuelezea mpambano kati ya timu yake na Azam Fc ambao umemalizika hivi punde na Simba kibuka na ushindi wa goli moja kwa bila.


Kocha wa Timu ya Azam Fc Itamor akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja ewa Uhuru mara baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya timu ya yake na Simba Sports Club.

MBUNIFU WA MAVAZI FATMA AMOUR AFANYA MAMBO MAKUBWA NCHINI MAREKANI!!

Fatma Amour amefanya mambo makubwa huko Marekani katika maonyeho ya mavazi yanayoendana na mafunzo ambapo Wanawake watanzania 13 wako nchini humo kwa mafunzo mbalimbali ya kazi za sanaa kwa mwezi mmoja, hili ni kundi la tatu kwenda nchini Marekani kwa mafunzo hayo makundi mengine mawili yameshakwenda na kupata mafunzo na wamerejea nchini.
Wanawake wasanii hao wanatoka mikoa ya Tanga, Zanzibar, Dar es salaam Arusha na Dodoma na Wilaya ya Bagamoyo wameendelea kushiriki katika maonyesha ya sanaa za aina mbalimbali yanayoandaliwa na vikundi vya sanaa vya Jimbo la Ohio nchini humo.
mafunzo yalianza tarehe 6 oktoba na yatamalizika tarehe 3 Novemba ambapo mpango huu wa mafunzo unadhaminiwa na serikali ya Marekani, wasanii hawa pia watatembelea jumuiya mbalimbali katika majimbo ya Michigan na Ohio,
Katika safari hiyo Mwanamitindo mbunifu wa Tanzania Fatma Amour Hamad wa Famour Designs amefanya mambo makubwa katika maonyesho na amezindua mitindo yake katika hafla ya uchangiaji wa sanaa yenye jina "Magic Of Tanzania" uzinduzi umefanyika jimbo la Ohio oktoba 12, katika uzinduzi huo pia pia ametambulisha na ataendelea kutambulisha mitindo na kazi zake nyingine za sanaa katika maonyesho mengine yanayoendelea sambamba na mafunzo yao nchini humo.

Fatmar Amour katikati akiwa na wanawake wenzie na wadau mbalimbali wa sanaa nchini humo.

Big Brother Revolution: Images from Day 46 - THURSDAY OCTOBER 22!!

It’s carnival time! Day 46 of M-Net’s BIG BROTHER REVOLUTION was packed with glitzy glamour, fast-paced dance and colorful celebration as carnival fever swept the house!
Thursday is Task Presentation day on BIG BROTHER REVOLUTION and this week, the housemates have been hard at work polishing their dance moves and costumes ahead of the big day. Having given their all and practiced late into the night, the housemates stood around quietly after their presentation as Big Brother delivered the verdict. Having scored 40 out of 60 points, in categories like liveliness, flair, team work and performance, the housemates lost only their second task – a big blow, considering they had wagered 100% of their Sha-Sha’s on the outcome. Kristal and Emma’s mutual animosity grew as she complained to Quinn that Emma wouldn’t let her use her extra pair of sneakers, after Kristal’s were confiscated for having visible branding on them. Itai was questioned about why he does not mention his girlfriend as much as he talks about a particular ex-girlfriend. He told the housemates that he is secure in his relationship and doesn’t feel the need to talk about his girlfriend all the time. Kristal remarked that it’s odd that everyone knows his ex-girlfriend’s name, but not his girlfriend’s, because he talks about his ex- more. Nkenna cornered Leonel to talk strategy beyond Sunday’s looming eviction, telling him that Kevin and Geraldine are the only people she trusts in the house. His response was: "If you want, you can count on me”, telling her that he doesn’t support people he doesn’t like. She asked him if he liked Kevin and Geraldine, which he said he does. Nkenna then proposed that Leonel, Elizabeth, Kevin, Geraldine and Nkenna be the last five housemates standing – the dawn of a new alliance?

Ferguson: It's a massive fixture!!

Sir Alex Ferguson has insisted form will play no part in what he deems Manchester United's biggest fixture: a meeting with Liverpool on Sunday. The Red Devils are in much the better shape as they prepare to face their great rivals at Anfield.
Ferguson's men are top of the Premier League and well on course for a place in the knockout stages of the UEFA Champions League. In contrast, Liverpool are lurching towards a crisis after a run of four successive defeats, which has left them struggling to maintain interest in both competitions.
Yet the United manager has faced Liverpool enough times during his long tenure at Old Trafford to know to expect the unexpected. "Manchester United and Liverpool games, as I have said many times, are without question massive games. That will never change," said Ferguson.
"It is the kind of game when I came to the club 23 years ago, I thought 'yeah'. In my first derby game with them I got a complete sense of the history of both teams and it hasn't changed. It is still a massive game.
Manchester United and Liverpool games are without question massive games. It is the game as far as I am concerned.
Sir Alex Ferguson
"It is the game as far as I am concerned, that won't change. We are going in in decent form, there is good confidence in our play, but it is a derby game and anything can happen in derby games. Going to Anfield at any time is a hard game."
Victory for United would add considerably to the growing pressure on Liverpool manager Rafa Benitez. Yet Ferguson, subject of a remarkable attack from the Spaniard last season, is quick to point out that is no concern of his.
"I'm not interested in Liverpool," the 67-year-old said. "I'm only concerned about what we do on Sunday."
United comfortably held off Liverpool to take the title last season, even though they lost twice at the hands of the Reds. The second of those occasions was a 4-1 humbling at Old Trafford but, having had the last laugh by equalling Liverpool's record of 18 league wins, Ferguson does not feel there are scores to settle.
"I don't see that we have a point to prove. Different games are shaped by circumstances of games," he said. "You can't look at last season as a barometer of our form or Liverpool's form. Derby games are derby games and anyone can win it. Strange things can happen. It has happened so many times."
Selection issuesWayne Rooney remains doubtful for United as he continues to struggle with a calf injury. The forward will be assessed tomorrow - his 24th birthday - before a decision is taken on whether to include him in the squad.
"He is always desperate to play," Ferguson explained. "That is the nature of the boy, you won't stop that. It is important how he does in training tomorrow. If he does train tomorrow we will have a better idea."
Ryan Giggs and Patrice Evra are both poised to return after suffering knocks against Bolton Wanderers last week, but Darren Fletcher is also doubtful and Park Ji-Sung is definitely out.
United's own performances have been questioned at times this season, most recently after an unconvincing 2-2 draw with Sunderland earlier this month. But Ferguson feels his side are now stronger for the recent return of veteran goalkeeper Edwin van der Sar.
Ruud Gullit said he was the best in the world and got no argument from the rest of the panel. He really is a fantastic goalkeeper.
Sir Alex Ferguson on Edwin van der Sar
The start of the 38-year-old Dutchman's season was ruined by a hand injury but he came back against Bolton and also featured in the midweek win at CSKA Moscow. Ferguson recently heard his number one described as the game's best goalkeeper on a TV programme and is in full agreement.
"Ruud Gullit said he was the best in the world and got no argument from the rest of the panel," Ferguson said. "His argument was quite right - look at his record over the years."His experience, his composure, his organisational ability - he really is a fantastic goalkeeper Story by www.fifa.com

TENGA AWAFAGILIA WACHEZAJI WA KULIPWA SIMBA, ASEMA WANASTAHILI KUITWA WACHEZAJI WA KULIPWA!!

Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Reodger Chila Tenge.

Rais wa Shirikisho la soka nchini TFF Bw. Reodiger Tenga amewasifu wachezaji wa kulipwa wa simba kutokana na uwezo mkubwa na nidhamu ambayo wachezaji hao wamekuwa wakionyesha mara kwa mara katika michezo mbalimbali ya ligi kuu ya Vodacom ambayo wamekwa wakishiriki na Timu yao.
Tenga ameyasema hayo leo mbele ya waandishi wa habari wakati wa mdahalo uliokuwa umeitishwa kati ya Rais huyo na chama cha waandishi wa habari za michezo TASWA katika makao makuu ya shirikisho hilo pale Karume ili kujadili mambo kadhaa juu ya mstakabali wa soka letu
Mdahalo huo ulikuwa ni wa kujadili hatua mbalimbali ambazo shirikisho la soka TFF limechukua dhidi ya waamuzi wanaovurunda katika uchezeshaji wao na kupelekea baadhi ya waamuzi kufungiwa maisha na kutojishirikisha na shughuli zozote za mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini, kuna waamuzi kadhaa wamefungiwa na shirikisho hilo wakiongozwa na bosi wao mwamuzi wa kati Othman Kazi
Rais huyo wa TFF aliwaelezea wachezaji Hirary Echesa, Emmanul Okwi na Joseph Owino wote wa Simba kuwa ni wachezaji mahiri na wanaostahili kuitwa wachezaji wa kulipwa kutokana na uwezo ambao wameonyesha katika michezo mbalimbali waliyocheza na kuonyesha kiwango cha hali ya juu kinidhamu, hivyo akasema wachezaji hao wanastahili kupongezwa kwa wanachokifanya na kwamba ni wachezaji wenye kuleta changamoto kubwa kwa wachezaji wetu wa ndani lakini pia kwa wachezaji wengine wa kulipwa wanaochezea timu za hapa nyumbani.

FREDRICK SUMAYE kuwa mgeni rasmi tamasha la kuchangia taassisi ya Saratani ya Ocean Road!!

Noel Tenga mkurugenzi wa Christian Directory and Consultancy (T) akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi zake zilizopo magomeni kulia ni mwimbaji Upendo Kilahiro.
Upendo Kilahiro akiimba katika moja ya maonyesho yake.

Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Fredriki Sumaye, anatarajiwa kuongoza maelfu ya watu katika tamasha kubwa la kuchangia taasisi ya Saratani ya Ocean Road litakalofanyika Mkoani Arusha hivi karibuni.
Tamasha hilo ambalo linatarajiwa kuwa la aina yake kuwahi kufanyika katika Mkoa huo wa Arusha, litafanyika Jumapili ya tarehe 8 Novemba 2009, katika Uwanja wa Karume.
Tamasha hilo la kihistoria linakwenda sanjari na kutambulishwa rasmi kwa albamu ya muziki wa Injili inayoitwa ‘Asante Yesu’ ya mwimbaji Upendo na Amon Kilahiro.
Uzinduzi wa albamu hii ya ‘Asante Yesu’ ya Upendo Kilahiro umekuja mara baada ya kupita kipindi cha takribani miaka mitatu tangu afanye tamasha kama hilo katika Mkoa huo wa Arusha wenye sifa ya kuwa na watalii wengi.
Baada ya kuwa katika safari za Injili katika nchi nyingi kama vile Afrika Kusini, Canada na Marekani sasa mwimbaji huyo amerudi nyumbani kuja kumtukuza Mungu.
Tamasha hili la kusifu na kuabudu pamoja na uzinduzi wa ‘Asante Yesu linasimamiwa na kuandaliwa na taasisi ya Christian Directory and Consultancy (T) kwa kushirikiana na Upendo na Amon Kilahiro.
Akizungumza na waandishi wa habari, msemaji wa taasisi ya Christian Directory and Consultancy(T), Bwana Noel Tenga alisema kuwa lengo kubwa la tamasha hilo ni kukusanya fedha za kufanya kampeni ya kusidia watu wenye uhitaji. Kampeni ambayo itakuwa ni ya kudumu na kwa sasa wamelenga kusaidia watua wagonjwa wa Saratani.
“Katika tamasha letu hili tuna lengo la kukusanya fedha ambazo sehemu kubwa itakwenda kusaidia wagonjwa wa Saratani katika taasisi ya Ocean Road.
“Tutazindua rasmi kampeni ya kusaidia watu wenye uhitaji, kwa safari hii tumekusudia kwenda kutoa msaada katika taasisi ya Ocean Road, hasa katika eneo la kununua mashine ya kuchujia maji na kukarabati sehemu ya majengo ya wodi ya wagonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi,” alisema Noel Tenga.
Aidha msemaji huyo alisema, tamasha hilo pia linatarajiwa kudhuriwa na watu mbalimbali wa kada tofauti tofauti, na kwamba mgeni rasmi wa tamasha hilo atakuwa Mh. Fredriki Sumaye, ambaye atasindikizwa na wageni wengine waalikwa ambao ni wabunge na wafanyabiashara mbalimbali kutoka katika Mkoa huo wa Arusha
Katika tamasha hilo mwimbaji Upendo na Amon Kilahiro wanatarajiwa kuimba nyimbo zote katika albamu hiyo ya Asante Yesu ‘live’ na si kama ilivyozoeleka katika matamasha mengine.
Tamasha hili litapambwa na waimbaji wengine wa nyimbo za injili hapa nchini ambao ni Christina Shusho, Jenifer Mgendi, Victor Aaron, JoJo Jose na mke wake Matlida Mlay na waimbaji wengine wengi.

MAMA SALMA KIKWETE AWATAKA WANAWAKE NCHINI KUCHAGUA VIONGOZI WANAOFAA!!

Mke wa Rais mama Salma Kikwete.

Na Anna Nkinda - Maelezo, Kilombero
23/10/2009 Wanawake nchini wametakiwa kushirikiana kwa pamoja ili waweze kuwachagua viongozi mahiri ambao atawaletea maendeleo katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji unaotarajia kufanyika mapema jumapili hii.
Wito huo umetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea kwa nyakati tofauti na wanachama wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) katika wilaya za Mvomero, Ulanga, Kilombero na Kilosa.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kuwa kila mtu anahaki ya kumchagua kiongozi anayemtaka hivyo basi kujitokeza kwa wingi kwa wanawake kupiga kura ndiko kutakakosaidia kumchagua kiongozi ambaye ataleta maendeleo na si kiongozi jina.
"Ninyi kama wanawake mnatakiwa kuangalia ni kiongozi wa Chama gani anayeweza kuitunza amani iliyopo hapa nchini kwani kuna baadhi ya watu wanapita na kuwadanganya kuwa njooni huku ni kuzuri ila mkumbuke kwamba amani ikipotea katika familia na katika nchi mtu wa kwanza kuathirika ni mwanamke", alisema.
Kwa upande wa kuongeza idadi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mwenyekiti huyo wa WAMA aliwataka wanawake hao kuhakikisha kuwa idadi ya wanachama inaongezeka kwa wanawaleta wanawake wenzao ambao si wanachama wa UWT katika umoja huo.
Mama Kikwete alisema, "Kuanzia sasa rafiki wa mwanamke awe ni mwanamke mwenzake, mkumbushane katika kulipia kadi za uwanachama kwani kuna baadhi yenu ambao ni wazito katika ulipaji wa ada pia msisahau kuwaunga mkono wanawake wenzenu kutoka CCM ambao wanagombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi huu" .
Akiwa wilayani Kilombero aliwapokea na kuwakabidhi kadi mpya za CCM wanachama wawili ambao ni Zainab Henji na Sakina Stambuli kwa niaba ya wenzao 22 waliohama kutoka chama cha CUF.
Taasisi ya WAMA iliwachangia wanawake hao mchango wa Tshs. 500,000 kwa kila wilaya na Tshs. 200,000 kwa wanawake wa tarafa ya Malinyi fedha ambazo watazitumia katika shughuli za maendeleo .

MAPOKEZI YA VODACOM MISS TANZANIA MIRIAM GERALD YAFANA JIJINI MWANZA LEO!!

Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald,akiwapungia mkono wananchi wa jiji la Mwanza walipompokea leo jijini humo, aliyesimama kushoto ni mmoja wa waandaji wa Vodacom Miss Mwanza Anita Zimbire. Miriam anatarajiwa kufanyiwa sherehe kubwa kesho jioni jijini Mwanza katika kumkaribisha rasmi ambapo mgeni wa heshima atakuwa mkuu wa Mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro.
Jinsi maandamano ya mapokezi ya Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald yalivyofana jiji Mwanza

Mzee Yahaya Msabaha (81)(kushoto)akisalimiana na Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald (kulia)kwenye ofisi za Vodacom jijini Mwanza alipoenda kupatiwa huduma za M Pesa, mara baada ya mrembo huyo kuwasili kutoka Dares Salaam (katikati)Mkurugenzi Mkuu wa masoko wa kanda ya ziwa wa Vodacom Tanzania Steven Kingu.

Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald,akimkabidhi mafuta ya kula mmoja wa watoto waishio katika mazingira magumu Laurance Malimi(kushoto) katika maeneo ya Bwiru jijini Mwanza mara baada ya kuwasili rasmi katika jijini humo akitokea Dares Salaam.

Afisa habari wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu(kushoto)akimpatia maelekezo Meneja wa Simba Telecom Bw.Rajendra(kulia) aliyekuwa mwajiri wa Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald, namna atavyompatia maua aliyeandaa kwa ajili ya mrembo huyo.

Tanzania Tourist Board says no to the opening of Kenyan entry Point (SAND RIVER / BOLOGONJA BORDER CROSSING POINT IS CLOSED)

Tanzania Tourist Board (TTB) would like to inform all Diplomatic Missions, within and overseas, Tourist Representatives, Tour Operators, Travel Agents, operators of tourist accommodation establishments, transporters, tourists and the general public that, the Sand River/Bologonja Border crossing point connecting Maasai Mara Game Reserve in Kenya and Serengeti National Park in Tanzania IS NOT OPEN.
TTB has seen the need to clarify the distorted information in order to avoid confusing and inconveniencing tourists intending to visit Serengeti National Park and Maasai Mara Game Reserve or vice versa, as per attached circular e-mail issued by Kenya Association of Tour Operators (KATO) on 18th September 2009. The circular e-mail reads as follows, quote:
“Dear Member,
SAND RIVER BORDER CROSSING
Arising from talks held between the E.A. member states, we are pleased to confirm that in a move that will dramatically reduce the travel time between Mara and Serengeti, an agreement has been reached to open up Sand River Gate in the Maasai Mara. This will now take effect as a new official border crossing between Kenya and Tanzania.
The development was announced by the Minister for Tourism, Hon. Najib Balala, after he obtained confirmation about the opening from both Immigration Chiefs.
Our initial enquires to confirm the actual situation on the ground reveals that there is full deployment of Immigration staff on the Kenyan side at Sand River, whereas they are yet to be deployed on the Tanzanian side. This unfortunately means that travellers cannot be cleared from Kenya into Tanzania (or vice versa) as there is lack of immigration personnel on one side of the Border.
This has been brought to the attention of the relevant authorities and we will continue to follow up closely until the situation is rectified.
Kind regards,
Fred Kaigua
CHIEF EXECUTIVE” – end of quote.
The e-mail circular is misleading as there is no agreement of any kind reached to open the Sand River/Bologonja border point. The agreed designated border point being used to cross by road from Maasai Mara to Serengeti is Isebania/Sirari, now being commonly used by all Tour Operators from Tanzania/Kenya.
We would like our esteemed clients to note that, Tanzania has no intention to re-open the Sand River/Bologonja Border point. The entry point will remain closed for environmental reasons. The fragile ecosystem of the area which is a World Heritage Site cannot be sacrificed for the purpose of shortening the route between Maasai Mara and Serengeti.
TTB wishes to inform all Tourist Agents and the general public that, according to the Tourism Co-operation Agreement between the United Republic of Tanzania and the Republic of Kenya following the Arusha Summit Communique of November 16th, 1983, Article X(b), tourists shall be transported in and out of each Country through designated border posts or regional towns.
The designated border points between Kenya and Tanzania are:-
Tanzania Kenya
Namanga Namanga
Sirari Isebania
Holili Taveta
Horohoro Lungalunga
For more information, contact:
The Managing Director
Tanzania Tourist Board
P.O. Box 2485
Dar es Salaam
Tel: +255 22 2111244/5
Fax: +255 22 2116420
Email:
safari@ud.co.tz / ttb@ud.co.tz
Website:
http://www.tanzaniatouristboard.com/

Simba wataka timu ya Yanga isitafute anayewaroga!!

Msemaji wa Klabu ya Simba Cliford Ndimbo.

Klabu ya Simba ya Jijini Dar es Salaam imewataka wapinzani wao wa jadi Yanga kutowatupia lawama pale wanapopata tatizo na waangalie vizuri walipojikwaa na si walipoangukia.Hayo yamesemwa na Msemaji wa Simba Cliford Ndimbo baada ya kupata taarifa kutoka Yanga kuhusu kufungiwa kwa mchezaji Moses Odhiambo na Amiri Maftah kumesababishwa na Simba.
Ndimbo amesema Ligi Kuu ya Mwaka huu imeendeshwa vizuri na makosa ambayo yanafanyika katika michezo mbali mbali inafanyiwa kazi na kutolewa maamuzi, hivyo amepongeza Shirikisho la kandanda Tanzania kwa kazi nzuri waliyoifanya katika Ligi inayoendelea.Simba hadi sasa imejikusanyia jumla ya pointi 24 katika msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara
(habari kwa hisani ya http://www.viwanjani.blogspot.com/.)

RUTI ZATAJWA KWA WAKIMBIA BAISKEL MWANZA!!

Meneja Matukio na Promosheni wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa(kushoto)akifafanua jambo wakati wakitangaza njia (route)zitakazotumika katika mashindano ya mbio za baiskeli ,wa pili kutoka kushoto Mwenyekiti wa kamati ya ufundi CHABATA Godfrey Jax, Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania kanda ya ziwa Benedict Emmanuel, Meneja Masoko wa Vinywaji vya baridi vya Pepsi Vis Rao Mwanza.Mashindano haya yatakafanyika tarehe 23 na 24 yameandaliwa na Vodacom Tanzania wakishirikiana na CHABATA.

Mwanza, 22. 10. 2009. Kampuni ya simu za mkoni ya Vodacom Tanzania imetangaza njia zitakazotumiaka kwa mashindano yam bio za baiskel jijini Mwanza mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kesho kutwa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Mwanza, wakati wa mkutano mahususi wa kutaja njia za mbio hizo (route), Meneja Matukio na Promosheni wa Vodacom Tanzania, Rukia Mtingwa, alisema mashindano hayo yamepangwa kufanyika tarehe 23 na 24 mwezi huu.
Alisema Vodacom Tanzania imeandaa mashindano hayo yatakayofanyika jijini Mwanza kwa lengo la kuendeleza mchezo huo.
Mbio hizi zimegawanyika katika sehemu kuu tatu,mbio za kilimeta 10 za walemavu,kilometa 80 kwa wanawake na kiliometa 196 kwa washindani wanaume,Mbio za kilometa 10 zitakazofanyika ijumaa tarehe 23,octoba2009,zitaanzia kiwanda cha vinywaji cha Pepsi na kumalizikia hapo.
Mshindi wa siku hiyo atatangazwa siku ya jumamosi tarehe 24,octoba 2009,kwa upande wa mbio za wanawake ambazo ni KL 80,zitaanzia Natta Hotel na kuelekea njia ya Musoma hadi Lugeye,hapo watageuza na kurudi hadi Natta Hotel,Mbio za Kilometa 196,zitaanzia pale Natta Hotel,na kupita Nyerere Road,watakwenda hadi Nyashimo ambapo watageuka na kurudi ambapo zitamalizikia Bugando kwenye njia panda ya kuelekea Bugarika.
Baada ya hapo utoaji wa zawadi kwa washindi utafuatia ambapo mshindi wa kwanza kwa kilometa 196 atapata kitita cha Shilingi Milioni moja na laki mbili(1,200000)wakati mshindi wa pili atazawadiwa Sh.Laki tisa(900,000)Mshindi wa tatu atapokea Sh.laki sita(600,000)katika kundi hili mshindi wan ne hadi wa kumi atazawadiwa Sh.laki nne na nusu(450,000)mshindi wa kumi na moja hadi 20 atapokea Sh.laki mbili(200,000)kila mmoja na wakati mshindi wa 21 hadi 30 ataondoka na kitita cha sh.laki mojamoja(100,000)Kwa upande wa Kilometa 80,Mshindi wa kwanza atazawadiwa Sh.1000,000,mshindi wa pili atapewa sh.750,000,mshindi wa tatu atazawadiwa sh.500,000,mshindi wan ne hadi wa kumi atapewa sh.320,000,mshindi wa kumi na moja hadi wa 20 atazawadiwa sh.120,000 wakati mshindi wa 21 hadi wa 30 atapewa sh.60,000.Kwa upande wa mbio za walemavu,Mshindi wa kwanza wa kiume na wakike atapokea sh.300,000,washindi wa pili watazawadiwa sh.200,000,na washindi wa tatu kila mmoja atapokea sh.100,000,na kuanzia mshindi wan ne hadi wa kumi atapokea sh.50,000.Vodacom Tanzania itatoa zawadi kwa washindi wote yenye jumla y a thamani ya sh.Milioni kumi na sita na laki tano na arobaini(16,540,000) ,zoezi ambalo litafanyika uwanja wa CCM Kirumba ambapo pamoja na mambo mengine,kutakuwa na burudani mbalimbali kundi la wasanii la TMK Wanaume Family,Tiptop Connections wakisindikizwa na Berry Black.
Naye Mratibu wa mashindano hayo Godfrey Jax, alisema mashindano ya mwaka huu ni ya ubora zaidi kupita ya miaka ya nyumba na yatakuwa na ulinzi mkali na haya yote ni kutaka kuyafanya mashindano haya kuwa na kiwango cha hali ya juu ya kimataifa.

Zaidi ya shilingi milioni mia moja kumi na mbili zimetolewa na mashirika kujenga kituo cha afya Mtimbira!!

Waziri wa Afdya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa.

Na Anna Nkinda - Maelezo, Ulanga
22/10/2009 Zaidi ya shilingi milioni mia moja kumi na mbili zimetolewa na mashirika yasiyo ya kiserikali ya Empower na World Lung Foundation kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Theatre, wodi ya wazazi na maabara ili kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto katika kituo cha afya Mtimbira kilichopo wilayani Ulanga katika mkoa wa Morogoro.
Hayo yamesema jana na Mkuu wa kituo hicho Dk. Eliazari Kweka wakati akisoma taarifa ya kituo kwa mke wa Rais Mama Salma Kikwete alitembelea zahanati hiyo na kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vya afya.
Dk. Kweka alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa wodi ya wazazi ambayo ujenzi wake umegharimu Tshs. 45,000,000/= kutawawezesha kina mama wajawazito 16 kupata huduma ya uzazi kwa wakati mmoja.
Alizitaja changamoto zinazokikabili kituo hicho kuwa ni upungufu wa watumishi pamoja na vifaa mbalimbali vya kutolea huduma ya mama na mtoto.
Kituo hicho kinatoa huduma kwa wagonjwa wa ndani na wa nje, huduma za wajawazito na watoto, huduma za kujifungua, uzazi wa mpango, huduma za maabara,ushauri nasaha na upimaji wa Virusi vya Ukimwi (VVU) , upatikanaji wa dawa za kupunguza makali ya VVU, huduma za dharula za magonjwa ya kinywa na huduma ya kifua kikuu na ukoma.
Naye Mama Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) aliwataka wanawake wajawazito kuhudhuria kliniki na Hospitali mapema ili waweze kupata huduma na matibabu jambo mbalo litawasaidia kujifungua salama mtoto mwenye afya njema.

WAFANYA BIASHARA KUTOKA UJERUMANI WAJIONEA FURSA ZA UWEKEZAJI NCHINI!!

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Wafanyabiashara na wawekezaji toka Ujerumani waliokuja kujionea fursa za uwekezaji na biashara nchini, wafanyabiashara hao walimtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam Oktoba 20, 2009.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

UCHAGUZI wa Viongozi TASABA India Bangalore!!

Ndugu WATANZANIA India-Bangalore Tunaelekea kwenye Uchaguzi wa TASABA,umefika wakati wa kupata Rais Bora na Viongozi Wenzake na Mpenda Haki,Mleta Maendeleo na si Fisadi,Mwenye ushirikiano kwa kila Mtanzania .Tafadhali tunaomba Umpigie Kura Ndugu yetu FIDELIS MSOMEKELA katika nafasi ya Urais TASABA na ANGEL TUNGARAZA kuwa makamu wa Rais hapa Bangalore India bila Kusahau William G Mziray kuwa Muweka hadhina wa TASABA.Kwa uongozi Huu TASABA itapata mafanikio na tutaweza kushiriki katika uchaguzi ujao bila shaka tukiwa Bangalore.
Wako katika Kujenga ushirikiano kwa watanzania.

Life's challenges are not supposed to paralyze you, they're supposed to help you discover who you are.Mkole Shadrack Kamenya,
Narayana Hrudyalaya Institute Of Medical Scince,Narayana hrudayalaya Hospitals,Department Of Perfussion,2nd Floor,Operation Theatre 06.
No. 258/A, Bommasandra Industrial Area,Anekal Taluk, Bangalore 560 099,India.Mobile:+919686805401