MAPOKEZI YA VODACOM MISS TANZANIA MIRIAM GERALD YAFANA JIJINI MWANZA LEO!!

Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald,akiwapungia mkono wananchi wa jiji la Mwanza walipompokea leo jijini humo, aliyesimama kushoto ni mmoja wa waandaji wa Vodacom Miss Mwanza Anita Zimbire. Miriam anatarajiwa kufanyiwa sherehe kubwa kesho jioni jijini Mwanza katika kumkaribisha rasmi ambapo mgeni wa heshima atakuwa mkuu wa Mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro.
Jinsi maandamano ya mapokezi ya Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald yalivyofana jiji Mwanza

Mzee Yahaya Msabaha (81)(kushoto)akisalimiana na Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald (kulia)kwenye ofisi za Vodacom jijini Mwanza alipoenda kupatiwa huduma za M Pesa, mara baada ya mrembo huyo kuwasili kutoka Dares Salaam (katikati)Mkurugenzi Mkuu wa masoko wa kanda ya ziwa wa Vodacom Tanzania Steven Kingu.

Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald,akimkabidhi mafuta ya kula mmoja wa watoto waishio katika mazingira magumu Laurance Malimi(kushoto) katika maeneo ya Bwiru jijini Mwanza mara baada ya kuwasili rasmi katika jijini humo akitokea Dares Salaam.

Afisa habari wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu(kushoto)akimpatia maelekezo Meneja wa Simba Telecom Bw.Rajendra(kulia) aliyekuwa mwajiri wa Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald, namna atavyompatia maua aliyeandaa kwa ajili ya mrembo huyo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment