Meneja Matukio na Promosheni wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa(kushoto)akifafanua jambo wakati wakitangaza njia (route)zitakazotumika katika mashindano ya mbio za baiskeli ,wa pili kutoka kushoto Mwenyekiti wa kamati ya ufundi CHABATA Godfrey Jax, Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania kanda ya ziwa Benedict Emmanuel, Meneja Masoko wa Vinywaji vya baridi vya Pepsi Vis Rao Mwanza.Mashindano haya yatakafanyika tarehe 23 na 24 yameandaliwa na Vodacom Tanzania wakishirikiana na CHABATA.
Mwanza, 22. 10. 2009. Kampuni ya simu za mkoni ya Vodacom Tanzania imetangaza njia zitakazotumiaka kwa mashindano yam bio za baiskel jijini Mwanza mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kesho kutwa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Mwanza, wakati wa mkutano mahususi wa kutaja njia za mbio hizo (route), Meneja Matukio na Promosheni wa Vodacom Tanzania, Rukia Mtingwa, alisema mashindano hayo yamepangwa kufanyika tarehe 23 na 24 mwezi huu.
Alisema Vodacom Tanzania imeandaa mashindano hayo yatakayofanyika jijini Mwanza kwa lengo la kuendeleza mchezo huo.
Mbio hizi zimegawanyika katika sehemu kuu tatu,mbio za kilimeta 10 za walemavu,kilometa 80 kwa wanawake na kiliometa 196 kwa washindani wanaume,Mbio za kilometa 10 zitakazofanyika ijumaa tarehe 23,octoba2009,zitaanzia kiwanda cha vinywaji cha Pepsi na kumalizikia hapo.

Mshindi wa siku hiyo atatangazwa siku ya jumamosi tarehe 24,octoba 2009,kwa upande wa mbio za wanawake ambazo ni KL 80,zitaanzia Natta Hotel na kuelekea njia ya Musoma hadi Lugeye,hapo watageuza na kurudi hadi Natta Hotel,Mbio za Kilometa 196,zitaanzia pale Natta Hotel,na kupita Nyerere Road,watakwenda hadi Nyashimo ambapo watageuka na kurudi ambapo zitamalizikia Bugando kwenye njia panda ya kuelekea Bugarika.
Baada ya hapo utoaji wa zawadi kwa washindi utafuatia ambapo mshindi wa kwanza kwa kilometa 196 atapata kitita cha Shilingi Milioni moja na laki mbili(1,200000)wakati mshindi wa pili atazawadiwa Sh.Laki tisa(900,000)Mshindi wa tatu atapokea Sh.laki sita(600,000)katika kundi hili mshindi wan ne hadi wa kumi atazawadiwa Sh.laki nne na nusu(450,000)mshindi wa kumi na moja hadi 20 atapokea Sh.laki mbili(200,000)kila mmoja na wakati mshindi wa 21 hadi 30 ataondoka na kitita cha sh.laki mojamoja(100,000)Kwa upande wa Kilometa 80,Mshindi wa kwanza atazawadiwa Sh.1000,000,mshindi wa pili atapewa sh.750,000,mshindi wa tatu atazawadiwa sh.500,000,mshindi wan ne hadi wa kumi atapewa sh.320,000,mshindi wa kumi na moja hadi wa 20 atazawadiwa sh.120,000 wakati mshindi wa 21 hadi wa 30 atapewa sh.60,000.Kwa upande wa mbio za walemavu,Mshindi wa kwanza wa kiume na wakike atapokea sh.300,000,washindi wa pili watazawadiwa sh.200,000,na washindi wa tatu kila mmoja atapokea sh.100,000,na kuanzia mshindi wan ne hadi wa kumi atapokea sh.50,000.Vodacom Tanzania itatoa zawadi kwa washindi wote yenye jumla y a thamani ya sh.Milioni kumi na sita na laki tano na arobaini(16,540,000) ,zoezi ambalo litafanyika uwanja wa CCM Kirumba ambapo pamoja na mambo mengine,kutakuwa na burudani mbalimbali kundi la wasanii la TMK Wanaume Family,Tiptop Connections wakisindikizwa na Berry Black.
Naye Mratibu wa mashindano hayo Godfrey Jax, alisema mashindano ya mwaka huu ni ya ubora zaidi kupita ya miaka ya nyumba na yatakuwa na ulinzi mkali na haya yote ni kutaka kuyafanya mashindano haya kuwa na kiwango cha hali ya juu ya kimataifa.

0 comments:
Post a Comment