YANGA YAIPA KICHAPO MTIBWA SUGAR MAGOLI 2-1

Kocha Papic wa timu Yanga.

Klabu ya yanga ikiwa inaendelea na mechi za kirafiki kwa ajili ya kujiweka safi na ligi kuu Tanzania bara imeendelea kushusha kipigo kwa timu pinzani ambapo kwa mara nyingine imeifunga timu ya Mtibwa Sukari magoli mawili kwa moja katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.


Lakini mchezo huo uliingia dosari baada ya mwamuzi wa mchezo huo kumtoa nje kocha wa yanga Kostadic Papic kwa kosa la kumlalamikia mshika kibendera namba moja ambaye kila wakati alikuwa anakataa mipira iliyokuwa inarushwa na mchezaji mkongwe Fredy Mbuna jambo lilomfanya kocha Papic kuja juu na kumlalamikia mshika kibendera huyo. habari wa hisani ya www.janejohn5,blog

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment