MCHEZA filamu wakike maarufu nchini Irene Uwoya, amesema kwasasa inabidi wasanii wachanga wajitokeze kurithi mikoba yao wao ambao kwasasa ni maarufu Afrika nzima.
Akizungumzia hili Irene alisema, kutokana na wao kutingwa na majukumu inabidi wasanii wachanga wajitokeze waweze kurithi mikoba yao kwani kwasasa wanashindwa kujikita moja kwa moja katika fani ili kuweza huku wakihudumia familia zao.
Alisema ukiangalia wacheza filamu wengi kwasasa wanamajukumu ikiwa wengine wameolewa na wengine kuwa na watoto pamoja na kuwaza maisha zaidi kuliko umaarufu."Iwapo watajitokeza wachanga ni lazima watajikita zaidi katika fani kwani ukiwa ndio unaibukia unakuta unatamani umaarufu jambo ambalo utajikuta wanafanya kazi kwa kujituma zaidi tofauti na sisi," alisema Irene.
Alisema kwasasa wao wamekuwa wakisubiri kushirikishwa zaidi badala ya kutunga kama awali livyokuwa wakati wanautafuta umaarufu, pia hata katika hafla mbalimbali wanashindwa kuhudhuria kutokana na majukumu yao ya kila siku.
Irene alisema yeye yupo tayari kuwapa mbinu zote za kucheza filamu pamoja na kuutafuta umaarufu kwa mtu ambaye atataka kufanya hivyo, ikiwa ni njia mojawapo ya kuinua vipaji vya wasanii wa watanzania.
Irene ambaye kwasasa ni mke wa ndoa wa mcheza soka kutoka nchini Kongo Ndikumana, bado anaendelea kucheza filamu pamoja na kushirikishwa katika filamu mbalimbali za wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini huku akihudumia familia yake ambapo mpaka sasa ameshacheza filamu nyingi pamoja na video ya muziki wa Tax bubu wa msanii Matonya.
Habari kwa hisani ya www.burudan.blog
0 comments:
Post a Comment