Watu mbalimbali watembelea banda la bunge sabasaba!!

Afisa wa Bunge Ndg. Ismail Jimrodger ( Mwenye Suti) akitoa maelezo kuhusu Historia ya Maspika wa Bunge waliowahi kuongoza Bunge la Tanzania tangu Enzi za Ukoloni kama wanavyoonekana kwenye picha zilizo ukutani.
Umati wa wananchi waliofika kutembelea Banda la Bunge kwenye maonyesho ya Sabasaba wakiliangalia na kulishika vazi la Spika ( Joho la Spika) ili kujionea jinsi lilivyo: Joho la Spika limekuwa kivutio kikubwa sana katika Banda la Bunge.

Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta Bi. Lily Mraba akifafanua namna ya kuweza kupata sheria mbalimbali pamoja na Hansard kupitia mtandao wa Bunge ambao ni www.parliament.go.tz kwa baadhi ya wananchi waliofik katika banda la Bunge kwenye maonyesho ya Sabasaba. Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge


Katibu wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) Ndg. Mathew Kileo akiwaleleza wananchi waliofika katika Banda la Bunge kwenye Maonyesho ya Sabasaba namna Kamati za kudumu za Bunge zinavyofanya kazi Bungeni katika kutekeleza jukumu la Kuisimamia na Kuishauri Serikali.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment