Rais Kikwete akagua Faru Serengeti!!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua moja wa faru weusi(black rhino) waliorejeshwa nchini kutokea Afrika ya Kusini hivi karibuni katika makazi yao ya muda huko mbuga ya Serengeti.Faru hao baadaye wataachiliwa na kuishi katika mazingira ya asili.Rais Kikwete aliwakagua faru hao wakati alipokuwa njiani akitokea mji wa Mugumu wilayani Serengeti ambapo alizindua mradi mkubwa wa maji na kuongea na wananchi .
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapongeza vijana wadogo wawili Brittany Scalciewicz(10) na kaka yake Joey Scalciewicz kutoka jimbo la California nchini Marekani ambao wako nchini Tanzania kwa utalii na walifanikiwa kupanda na kufika kilele cha mlima Kilimanjaro hivi karibuni.Vijana hao wadogo pamoja na wazazi wao wanaitembelea mbuga maarufu ya Serengeti ma walikutana na Rais Kikwete katika uwanja wa ndege wa Seronera,wilayani Serengeti wakati Rais Kikwete alipokwenda kuzindua mradi mkubwa wa maji katika mji wa Mugumu jana
(picha na Freddy Maro)


You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment