BANDA LA JWTZ LAVUTIA WANANCHI WENGI KATIKA VIWANJA VYA SABASABA!!

Hili ndilo banda la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambalo limekuwa kivutio kwa wananchi wengi wanaojitokeza kwenda kwenye maonyesho ya biashara ya kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Mw. Julius K. Nyerere barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam.
Katika banda hilo kuna mambo mbalimbali yanayoonyeshwa na wataalamu mbalimbali wa jeshi hilo zikiwemo lininga kwa ajili ya kuonyesha matukio mbalimbali na kuwapa wananchi maelezo juu ya kazi ya jeshi hilo na wajibu wao kwa watanzania kwa ujumla, lakini pia kuna daftari katika banda hilo ambalo wananchi wanatoa maoni yao mara baada ya kutembelea banda hilo hivyo wanachi msisite kupita hapo na kujionea shughuli mbalimbali za jeshi letu makini.
Meneja wa banda hilo Luteni Kanali Kapambala Mgawe akitoa maelezo kwa wakazi mbalimbali wanaotembelea banda hilo katika kitengo cha huduma ya afya ambayo inatolewa na jeshi hilo kulia ni Kapteni Boniphace Njau ambaye ni Daktari.
Hii ni luninga kubwa mabayo inaonyesha mikanda mbalimbali ya matukio ya ukombozi na mambo ya maafa yaliyowahi kufanywa na Jeshi la wananchi luninga hii imekuwa ikivutia watu wengi sana.
Huyu ni mmoja wa wanajeshi makini na mkakamavu wa jeshi hilo ambaye yupo katika monyesho hayo.

Hawa ni maafisa mbalimbali wa Jeshi la Wananchi waliopo katika banda la JWTZ kwenye viwanja vya maonyesho vya sabasaba kutoka kulia ni Meja Ally Gumbo, Meja Robert Mjange, Meja Romanus Msilu, na Meja Dornard Msengi

Koplo Ally Mkungu akitoa maelezo kwa wananchi katika kitengo cha habari kinachochapisha Jarida la (ULINZI)

Luteni Asteria Komba akitoa maelezo kwa wananchi katika kitengo cha habari pia.

Hii ni moja ya kauli mbiu ya jeshi hilo katika maonyesho hayo

kama unavyoona watu ni wen.gi wanaotembelea banda hilo

Kulia ni Meneja wa banda Luteni Kanali Kapambala Mgawe pamoja na Arthur Waden na Mustapha Mhina waliopo katika monyesho hayo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment