Rais Kikwete ziarani Mugumu Serengeti!

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Huduma ya maji kwa Jamii Mhandisi Frida Rweyemamu(watatu kushoto) akitoa maelezo ya mradi wa maji wakati Rais Jakaya kikwete(katikati) alipokagua bwawa kubwa la maji katika mji wa Mugumu wilayani Serengeti jana.Kushoto ni Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya.Rais Kikwete ameshauri mradi wa ufugaji samaki na uvuvi ufanyike katika bwawa hilo.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi wa mji wa Mugumu waliojitokea kumlaki wakati wa ufunguzi wa mradi wa maji mji wa Mugumu wilaya ya Serengeti jana.

Rais Jakaya Kikwete,waziri wa Maji profesa Mark Mwandosya na Mbunge wa Serengeti Dr.Wanyancha wakijadiliana jambo wakati wa ufunguzi wa mradi wa maji katika Mji wa Mugumu,wilayani Serengeti jana(picha na Freddy Maro)

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment