RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA MASHUJAA!!

Rais Jakaya Kikwete pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Davis Mwamunyange na viongozi wengine wa jeshi wakitoa heshima zao leo wakati wa maadhimisho ya siku ya kuwakumbuka mashujaa waliopigana vita kuu ya Dunia 1939-1943.maadhimisho hayo yamefanyika leo asubuhi katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo Mabalozi, Mawaziri, Viongozi wa vyama vya siasa, Marais na Mawaziri wakuu wastaafu . viongozi pamoja na wananchi.
(Picha zote ni za Aron Msigwa na Mwanakombo Jumaa) - MAELEZO.

Safu ya viongozi wakuu serikali Mabalozi tasisisi na chama.

Wakazi wa jiji la Dar es salaam wakiangalia matukio mbalimbali wakati wa maadhimisho ya siku ya mashujaa.

Mzee Ali Hassani Mwinyi Rais Mstaafu (kushoto) akisalimiana na kanalli mstaafu JWTZ mzee Shadrack Malinzi.

Kiongozi wa mabalozi nchini Balozi Juma Khalfan Mpango akiweka shada la maua jeo jijini mkatka maadhimisho ya mashujaa.

Kanali mstaafu wa JWTZ mzee Shadrack Malinzi (87) akiongea na waandishi wa habari baada ya maadhimisho katika viwanja vya mnazi.

Baadhi ya askari wakiwa kaatika viwanja vya Mnazimmoja leo

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment