PERUDA MWINUKA NA LAGHTNESS MSANGI WAMEREMETA!!

Bibi harusi mLaghtness Msangi akimvisha pete ya ndoa mume wake Sunday Peruda Mwinuka wakati ndoa yao ilipofungwa leo kwenye kanisa la KKKT Azania Front jijini Dar es salaam na kufuatiwa na sherehe ya kukata na shoka iliyofanyika kwenye ukumbi wa Future Resort Mbezi Tangi Bovu kwa Komba, FULLSHANGWE tunawatakia maisha mema ya ndoa yao na mungu awabariki na kuwazidishia ili waweze kumtumikia vyema mungu wao.

Mzee Bernald Mwinuka kulia na mke wake mama Mwinuka pamoja na kaka yake na bwana harusi Raymond Mwinuka wakiwa kanisani huku wakifuatilia mahubiri ya mchungaji aliyekuwa akiendesha ibada hiyo takatifu ya ndoa ya Peruda na Laghtness leo mchana.
Mama yake na Bibi harusi Mama Msangi wa kwanza kulia akiwa akiwa na ndugu wenginee kanisani wakati wa ibada ya ndoa kwenye kanisa la Azania Front jijini Dar es salaam.
Bwana harusi na Bibi harusi wakiingia katika kanisa la kilutheri la Azania Front ili kufunga ndoa yao leo.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment