MKURUGENZI WA HABARI NA ELIMU KWA UMMA WA BUNGE AZUNGUMZA NA FULLSHANGWE!!



Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tazania kwa mara nyingine limeshiriki katika maonyesho ya 34 ya biashara ya kimataifa yanaoenelea kwenye viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere ambapo mwaka huu kumeongezeka mambo kadhaa yanayoonyeshwa katika banda la bunge kama anavyelezea Bw. JosseyMwakasyuka Mkurugenzi wa Habari Elimu kwa umma na uhusiano wa kimataifa.

Anasema mwaka huu ni mwaka wa tatu kwa ofisi hiyo ya bunge kushiriki kwenye maonyesho hayo ya biashara ambapo mwanzo kabisa kushiriki ilikuwa mwaka 2008 na mara ya pili ilikuwa mkwa 2009 na mwaka huu ndiyo mara ya tatu.

Jossey anasema lengo kubwa la kushiriki maonyesho haya ni kulipeleka bunge kwa wananchi kwa kuwa mara nyingi utamaduni tuliouzoea wananchi wanakwenda bungeni na kusikiliza mambo mbalimbali yanayoendelea bungeni hapo.

Hivyo tuliona tupanue wigo kwa wananchi kwa kuja katika maonyesho haya ili kuwaeleza mambo mbalimbali ya bunge na kuwaelezea kazi zake kwani tunaamini kwamba kupitia maonyesho haya tutawafikia wananchi wengi zaidi na malengo yetu ya kuwaelimisha watu kuhusu kazi za bunge yatakuwa yanatimia.

Anasema mwaka huu wameongeza nayaraka mbalimbali, majoho ya makatibu wa bunge na Spika wa bunge, lakini pia wameongeza upeo wa kutoa maelezo yao kwa kuwa mwaka huu ni wa uchaguzi mkuu wa rais wabunge na madiwani.

Amemalizia kwa kutoa wito kwa wananchi kuwa mwaka huu ni wa uchaguzi wananchi wajitokeze kwa wingi na kuchagua wawakilishi wazuri bungeni ili chombo hiki kuelekea kwenye bunge lenye nguvu na lenye kuelekeza kikamilifu utungaji wa sheria na kusimamia uhuru, usawa na umoja wa wananchi wa Tanzania.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment