Mke wa Rais Mama Salama Kikwete akisikiliza maelezo ya Mkurugenzi wa Pride Tanzania Bw. Rashid Malima wakati akimkabidhi zawadi zake mara baada ya kutembelea banda hilo leo kwenye maonyesho ya 34 ya biashara ya kimataifa yanayofanyika barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, Mama Salma amewataka wanawake hao kuboresha bidhaa zao hasa katika zoezi zima la umaliziaji (Finishing) baada ya kuzitengeneza ili ziwe na viwango vya kimataifa na kuwafanya wapate soko katika nchi za nje kama vile soko la Afrika Mashariki ambalo ndiyo kwanza limefunguliwa, kushoto ni Meneja Mkuu wa Pride Tanzania B. Shimimana Ntuyabaliwe
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia kikapu kilichofumwa na Zaida Issa mmoja wa watejam wa Pride Tanzania wakati alipotembelea banda la Pride Tanzania leo katika maonyesho ya 34 ya biashara ya kimataifa yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyererebarabara ya kilwa jijini Dar es salaam.
Meneja Mkuu wa Pride Tanzania Bi Shimimana Ntuyabaliwe akimkabidhi zawadi ya ngoma na kigoda Balozi wa Marekani Nchini Bw. A.E Lenhardt mara baada ya kutembelea banda lao katikati ni Mkurugenzi wa Pride Tanzania Rashid Malima.
Balozi wa Marekani nchini Bw. A.E Lenhardt akiangalia bidhaa kutoka kwa akina mama wajasiriamali mbalimbali ambao ni wateja wa Pride Tanzania wakati alipotembelea kwenye banda hilo leo katika maonyesho ya biashara ya 34 kwenye viwanja vya mwalimu J.K Nyerere barabara ya kirwa jijini Dar es salaam, katikati ni Mkurugenzi wa Pride Tanzania Bw. Rashid Malima.
0 comments:
Post a Comment