BAYPORT YAZINDUA MPANGO WA BAYPORT UNIVERSITY SCHOLRSHIP KWA WATEJA WAKE!!

Meneja Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya Bayport Bw. Ngula Cheyo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo wakati kampuni hiyo ilipozindua rasmi mpango wake wa (Bayport University Scholarship) ambao utasomesha wanafuzi wawili kwa kuwalipia gharama zote za chuo mara watakapopatikana katika mchakato wa kutafuta washindi unaotarajiwa kuanza leo Julai 12 na kumalizika Agosti 31 mwaka huu nchini kote ukihusisha wateja wake ambao ni watumishi wa serikali .

Bw. Ngula Cheyo amesema Fomu zinapatikana katika matawi yao yote mikoani na wilayani na wanafuzi au wazazi wao ambao ni watumishi wa Serikali watachukua fomu watazijaza na kuzirudisha kwenye matawi hayo kabla ya hiyo Agosti 31.

Katika fomu hizo kuna kipengele cha kuandika Insha ambacho ni kigezo muhimu katika kupata washindi wawili watakaobahatika kupata ufadhili huo na hii itategemea uwezo wa mwanafunzi katika kuandika Insha yake awe mwanamke au mwanaume wote wana nafasi sawa katika shindano hili, katika picha kulia ni Mica Mavoa Meneja Mwendeshaji Mkazi wa Bayport.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Bayport Bw. Ngula Cheyo na Meneja Mwendeshaji Mkazi wa Kampuni hiyo Mica Mavoa wakizindua rasmi mpango wa Bayport University Scholrship ambao ni kwa ajili ya kusomesha wanafuzi wawili wa vyuo vikuu watakaoshinda katika shindano hilo ambalo linahusisha uandikaji wa Insha.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment