LIFE MINISTRY YAANDAA KONGAMANO LA WASOMI WA VYUO VIKUU!!

Mkurugenzi wa Life Ministry na Mratibu wa kongamano la Change Your Destiny Conference akiongea na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati alipozungumzia maandalizi ya kongamano hilo linalotarajiwa kufanyika kuanzia Julai 26 mpaka Agosti 1 mwaka huu katika Chuo Kikuu Cha Dar es salaam eneo la Mabibo na kushirikisha vyuo zaidi ya 150 ndani na nje ya Tanzania.



Kongamano hilo limepewa jina la Change Your Desitny Conference. litazungumzia Mwaongozo wa vijana wanaomaliza vyuo vikuu, Imani na Maendeleo, maandalizi ya kujiunga na vyuo vikuu, Uongozi unaoleta mabadiliko, Masuala yanayosumbua vijana kama Utoaji mimba, Ushoga,Matumizi ya Madawa ya Kulevya na kadhalika.



Mambo mengine ni Jinsi ya kufanya vyema kitaaluma Maandalizi ya Ndoa, Uzalendo, Jinsi ya Kudhibiti muda wako chuoni na kazi, HIV-AIDS na Uadilifu, ambapo Mh. Jaji Mkuu Agustino Ramadhan atazungumza na Vijana kwa mtazamo wa Ubaba na Uongozi ili kuwaandaa vijana wetu kwa ajili ya Uongozi, Katika picha kushoto ni Hebron Mwakagenda Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment