Msanii wa maigizo na filamu mwenye asili ya kitanzania Alma Eno, ameng'ara na kutikisa ulimwengu wa Theatre mjini London kwenye onyesho la mchezo uitwao BEAK STREET ulioandikwa na mwandishi maarufu Greg Freeman, na kuongozwa na Ken McClymont.
BEAK STREET ni mchezo wa kijangili ulio kwenye ulimwengu wa Mapaka.
BEAK STREET ni mchezo wa kijangili ulio kwenye ulimwengu wa Mapaka.
Mchezo huo umekuwa ukionyeshwa kwenye kitongoji cha West End mjini London, ambacho ni maarufu kwa majumba ya maigizo,sinema na starehe. Beak Street imeonyeshwa kwa wiki 24 sasa katika majumba ya Tabard Theatre na Theatre Delicatessen (Sekunde 30 kutoka Selfridges)
Alma Eno anacheza silka mbili kwenye igizo hili; kwanza anacheza paka teja ambaye anaweza kuuza mtu yeyote kwa maziwa ya unga.
Vilevile anacheza silka ya Chorus ambayo anakuwa nafsi ya jangili Beak. Onyesho lake limesifiwa sana na wahakiki na sasa amefanikiwa kuingia mkataba wa kuigiza kwenye mchezo mpya wa Zip Postcode Wars ambao unaendeshwa na gwiji Ray Shell.
Alma ambaye ni mwigizaji wa kulipwa, alipata shahada yake ya sanaa na maigizo kutoka chuo maarufu cha Mountview Academy of Theatre and Art. Chuo hiki kina sifkia kwa kutoa waigizaji maarufu wa kimataifa kama Amanda Holden,Nick Moran, Ayub Khan Din mwandishi wa mchezo na sinema ya East is East and director Edward Hall.
Da Eno pia ameshawahi kucheza kwenye kipindi cha televisheni ITV hapa Uingereza kiitwacho Collision. Vilevile yuko kwenye filamu ya British Art iitwayo Boggie Woogie.
0 comments:
Post a Comment