Mkuu wa wilaya ya TEMEKE CHIKU NGALAWA amewataka viongozi wa michezo nchini kuwa na mipango endelevu ambayo itasaidia kukuza michezo badala ya kuleta migogoro.
Ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya viongozi mbali mbali wa michezo yaliyoandaliwa na kamati ya OLIMPIKI TANZANIA (TOC) ambapo amesema bila kuwa na uongozi wenye mipango na mikakati michezo itaendelea kubakia nyuma.
Kwa upande wake katibu mkuu wa TOC , FILBERT BAYI amesema kuwa kamati yake imeona mapungufu mengi katika vyama vya michezo nchini, hivyo imeamua kutoa mafunzo hayo ili kuweza kusaidia baadhi ya viongozi kujua nini maana ya utawala katika michezo
Vyama vitano vya michezo hapa nchini viongozi wanashiriki katika mafunzo hayo ambayo yanaendeshwa na mkufunzi kutoka kamati ya Olimpiki Tanzania HENRY TANDAU. Habari na picha kwa hisani ya
0 comments:
Post a Comment