Dar es Salaam, June 22, 2010: Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom imeanzisha huduma ya kutuma ujumbe mfupi bure kupitia Cheka SMS.
Ikiwa na wateja zaidi ya milioni nane, huduma hii mpya itawawezesha wateja wa Vodacom kuwasiliana zaidi kwa gharama nafuu na kuwafikia watu wengi.
Huduma hii mpya pia inamruhusu mteja kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwenda mtandao wowote hapa nchini na sio Vodacom peke yake.
Mkurugenzi wa Mahusuanio ya Jamii, Bi Mwamvita Makamba amesema kuwa kupitia huduma hii mteja anaweza kupata kwa wakati mmoja fursa ya kutuma ujumbe ufupi 25 bure na dakika 25 za bure za muda wa maongeze kwa shilingi 1000.
Ameongeza kuwa mteja pia anaweza kupata fursa ya kutuma ujumbe mfupi 15 bure na dakika kupata dakika 10 za bure za maongezi kwa shilingi 400 tu.
Huduma hii mpya pia inatoa fursa ya kutuma ujumbe mfupi wa maneno mara tano kwa kujisajili kwa shilingi mia moja. Amesema kuwa huduma zote zinapatikana kwa masaa 24 baada ya mteja kujisajili.
Ili kujisajili alisema kwa mteja wa shilingi 1000 anapaswa kupiga *147*1000#, wa shilingi 400 napaswa kupiga *147*400# na wa shilingi mia 100 anapaswa kupiga *147*100# wa siku nzima.
Pamoja na uzinduzi wa huduma hii mpya huduma ya Cheka Time ya muda wa maongeze bure bado inaendelea ambapo mteja anapata dakika 15 za bure kwa kujisajili kwa shilingi 200 na dakika 60 bure kwa kujisajili kwa shilingi 500.
Mteja ambaye anajisajili kwa shilingi 2000 anazawadiwa dakika 100 za maongeze bure na ambaye atajisajili kwa shilingi 5000 atazawadiwa dakika 300 za bure.
Bi Makamba amesema kuwa Vodacom Tanzania itaendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake ili kuweza kukidhi mahitaji yao ya mawasiliano.
0 comments:
Post a Comment