Jamal Zuberi na Mwirabi Sise
MAELEZO Dodoma.
Jumla ya wagonjwa 654,982 waliandikishwa na kupatia huduma bure ya za ushauri nasaha pampja na kupima virusi vya Ukimwi katika vituo 909 nchi nzima.
Idadi hiyo imetolewa a Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dokta Aisha Kigoda akijibu swali la Mhe. Emmanuel Luhahula Mbunge wa Bukombe aliyetaka kujua idadi ya vituop vya ushauri nasaha na upi,aji wa Virusi vya Ukimwi kwa hiari nchini.

Mhe. Kigoda amesema, jumla ya wagonjwa 337,854 walikuwa wameanzishiwa dawa za kupunguza makali ya UKIMWI katika kipindi hicho ambapo na kati yao 4,375 wanatoka katika wilaya ya Bukombe mkoani Shinyanga.
Waziri huyo amesema, Wizara yake inaendelea na mpango maalum wa kutoa huduma ya upimaji wa hiari na kupanua wigo wa huduma hiyo
“Baadhi ya maeneo tunaendesha huduma ya upimaji wa nyumba kwa nyumba ambao pia hufanyika kwa hiari baada ya kutolewa kwa ushauri nasaha,” alifafanua zaidi.
Aidha Naibu Waziri huyo amewataka wabunge kuwa jasiri katika kupiga vita dhidi ya Ukimwi kwa kuwahimiza wapiga kura wao majimboni matumizi ya kondom kama kinga ya ugonjwa huo.

0 comments:
Post a Comment