Jamal Zuberi na Mwirabi Sise – MAELEZO Dodoma
SERIKALI inakamilisha mchakato wa kubadilisha sheria ya leseni za biashara ili kuwawezesha wafanyabiashara wenye mtaji mdogo wa kuanzia shilingi milioni 20 kusajili bure biashara zao.
Hayo yamesemwa leo Bungeni na Mhe. Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko Bi. Mary Nagu, akijibu hoja za wabunge waliochangia hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali.
Mhe. Nagu alisema kuwa mpango wa majaribio kuhusiana na utaratibu huo tayari umekwishaanza katika Halmahsauri 16 za Tanzania Bara zikiwemo Tanga, Bukoba, Arusha na Monduli.
Waziri huyo amesema sanjari na usajili huo wa bure, serikali inakusudia kuboresha elimu ya biashara ili iweze kuwafikia Watanzania.
Amesema kuwa, tayari Shirika la Viwanda Vidovidogo (SIDO) limeanza kutoa elimu hiyo na imeonekana ni mkombozi kwa wafanyabiashara wadogowadogo ambao wwaliokuwa wakiendesha biashara zao bila kuwa na elimu ya ujasilia mali.
Hadi sasa vyuo mbalimbali vikiwemo vya Biashara (CBE) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam vimeingiza somo la ujasiriamali kwenye mitaala yao ili kuwawezesha wanafunzi wao kupambana na changamoto ya uchumi katika kuingia kwenye soko la pamoja la uchumi la Afrika Mashariki.

0 comments:
Post a Comment