Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa TBC Tido Muhando akizungumza na mashabiki na wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi wa matangazo ya kombe la Dunia kwa kituo hicho ambacho ndiyo pekee kitakuwa kikirusha matangazo hayo moja kwa moja kutoka nchini Afrika Kusini.
Tido amesema michezo yote 62 itaonyeshwa moja kwa moja kupitia TBC2 lakini kwa wale ambao tayari wameshaunganishiwa King'amuzi kutoka StarTime ambapo karibu kila siku kutakuwa na michezo takriban mitatu hivi.
Ameongeza kwamba kwa upande wa TBC1 pia michezo hiyo itaonyeshwa lakini akasema kwakuwa katika kipindi hiki kutakua ni vipindi vya kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma na bunge hili ni muhimu kwakuwa ni la Bajeti wakati mwingine michezo itakua haionyeshi hivyo watu wanaweza kutumia TBC2 kuangalia michezo hiyo vizuri bila usumbufu.
Wanne Star akifanya vitu vyake jukwaani jana.
Mmoja wa washindi walioshinda safari ya kukwea pipa kwenda kushuhudia fainali hizo zinazoanza Juni 11 nchini Afrika Kusini akipokea mfano wa viza yake kutoka kwa mgeni rasmi Waziri wa habari utamaduni na Michezo Joel Bendera.
Mashabiki mbalimbali waliojitokeza katika uzinduzi huo.
Kundi la TMK Family likiongozwa na Mh. Tema likikamua jukwaani.
Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Tido Muhando wa pili kutoka kulia akizungumza na Pendaeli Omary Mhariri wa Michezo kushoto na Asumpta Masoi Mhariri Mkuu TBC katika kuweka sawa mikakati wakati wa uzinduzi wa matangazo ya kombe la dunia uliofanyika jana kwenye uwanja wa Taifa.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Joel Bendera kushoto akisikiliza mazungumzo kati ya Mkurugenzi wa shirika la utangazaji Tanzania TBC na Mwenyekiti wa Klabu ya Simba wakati wa uzinduzi rasmi wa matangazo ya Kombe la Dunia jana kwenye uwanja wa Taifa.
0 comments:
Post a Comment