REDDS MISS ILALA KUSHANGWEKA BILICANAS KESHO!!


Warembo wanaotarajiwa kushiriki kinyang’anyiro cha kumtafuta Redds Miss Ilala 2010 watajimwaga kwenye ukumbi wa Club Bilicanas kwenye usiku wa Mwafrika siku ya jumatano usiku.

Wakiwa Bilicanas Warembo watatambulishwa kwa watu wa Dar es Salaam wanaotembelea Club hiyo iliyoko katikati ya Jiji la Dar es salaam. Tunatarajia kuwa kutakuwepo na fursa kwa Patrons wa Club hiyo kuchagua Miss Popularity Ilala baada ya warembo kujitambulisha na kutembea kidogo kwenye sehemu ya kuchezea muziki.

Vigezo vya kumchagua Miss Popularity Ilala vitakuwa ni kupendeza kwa mavazi ya usiku huo, kujitambulisha vizuri na kushangiliwa kwa sana na mashabiki na watu watakaokuwa kwenye Club.
Mazoezi ya Warembo wa Redds Miss Ilala yanaendelea vizuri na tambo za yupi atashinda zimeendelea kuitikisa kambi. Warembo wanaweka mikakati ya ushindi hata wakati mwingine wanaweka vikao vya namna ya kukabiliana na washindani wao wakubwa.

Kwa hali inavyoendelea imebidi wandaaji tuwaongezee shughuli za kufanya ili kuwakosesha muda wa kupumzika ambao wanautumia kwa kuwekeana vikao na bifu za kimashindano.

Hivi sasa tumeongeza nguvu kwenye kambi yao iliyoko Lamada Hotel Apartment kwa kuweka walinzi ( Body Guards) na kuwafanya Wasimamizi wao watatu ( Leila Bhanji, Sylivia Shally na Torry Oscar) wawe makini zaidi na kukaa nao muda mrefu.
Asubuhi Jumatano warembo watafanya shughuli za kijamii kwa kudhaminiwa na kampuni ya Aurora Security na kuonyesha mifano au kujifunza namna msichana wa Kitanzania anavyostahili kujitunza na kuwa mfano kwa jamii maana hawa wasichana ndio hawa hawa ambao watakuja kuwa Mama wa Familia na nguzo za ustawi wa Taifa kimaadili.
Shindano la Redds Miss Ilala 2010 litafanyika siku ya Jumamosi 26 juni katika ukumbi wa Ubungo Plaza kuanzia saa mbili usiku. Viingilio katika shindano hili vimetajwa kuwa Shs 100,000/= kwa Watu Mashuhuri ambao watapata chakula cha jioni na kuangalia mechi ya robo fainali ya kwanza ya kombe la Dunia. Viingilio vingine ni Business Class Tshs 50,000/= kwa watu ambao watataka kukaa mahari palipotulia na kuangalia mashindao ya warembo bila kukosa mechi ya Kombe la Dunia. Pia kutakuwepo na kiingilio cha daraja la Economy ambapo watu watalipa Tshs 10,000/= tu.

Shindano la Redds Miss Ilala 2010 limedhaminiwa na Premium Redds Original, Vodacom Tanzania, Aurora Security, Muzasha Tours and Safaris, Fabak fashion, Chanel Ten, Magic FM, Sofia Production, Habari Leo, Fullshangwe.blogspot na Issamichuzi blogspot, SYSCORP Group, Valye Spring, Clouds FM, Lamada Hotel Apartment na CXC Africa.
Warembo 18 wanatarajiwa kupanda jukwaani siku ya jumamosi.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment