Giraffe Ocean View Hotel yapata hadhi ya nyota nne!!

Charles Becon (Mkurugenzi wa Giraffe View Hotel ) akipokea tuzo ya hadhi ya nyota nne toka kwaWaziri wa Utalii na Maliasili Mh. Shamsa Mwangunga
Mkurugenzi wa Giraffe Ocean View Hotel Charles Bekon akiwa na tuzo ya Nyota Nne mara baada ya kuipokea.
wakurugenzi na wakilishi wa mahotel mbalimbali yaliyopata hadhi ya Nyota za madaraja mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Mh. Shamsa Mwangunga.
Hatimaye Wizara ya Maliasili na Utalii imezipatia hadhi ya NYOTA hoteli za Tanzania ambapo 66 kati ya hotel 99 zilizokuwa kwenye kinyang'anyiro zimepata hadhi ya nyota kwenye ngazi mbalimbali.

Huku the Kilimanjaro Hotel Kempinski, Movenpick Royal Palm Hotel na Sea Cliff Hotel, wakiibuka na hadhi ya nyota 5 mahoteli mengine kumi yakiibuka na hadhi ya nyota nne (Four Star) nayo ni Golden Tulip Hotel, New Africa Hotel and Casino, Paradise City Hotel, Protea Hotel and Serviced Apartments, Southern Sun Dar es Salaam, Saadani Safari Lodge, White sand Hotel, Giraffe Ocean View, Hotel Harbour View Apartments na Kinasi Mafia Hotel.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Mkurugenzi wa Giraffe Ocean View Hotel Dr. Charles Bekon amesema kuwa hayo ni mafanikio ya kujivunia kwani Hotel yao ina muda mfupi na hasa ukizingatia ushindani mkubwa wa biashara ambapo sekta ya Mahotel hasa ya kitalii imekamatwa na wageni.

Hata hivyo Dr. Bekon ametoa shukrani za dhati kwa watanzania wote wanaowaunga mkoni na kusisitiza kuwa pamoja na kupokea wageni wengi toka nje bado soko la ndani ni kubwa na linamchango wa kutosha.
Kwa upande wake Mheshimiwa Mwangunga alisema zilitumika 250milion shilingi za kitanzania kufanikisha zoezi hili huku wizara yake ikichangia Millioni 85 na Wizara ya biashara kupitia kitengo cha Tanzania Trade Integration Project wao wamechangia Million 176/-.

Kwa habari zaidi ya tukio hilo bofya hapa
http://www.dailynews.co.tz/home/?n=10968&cat=home

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment