Ridhawan akabidhiwa mikoba ya kusaka wadhamini wa JK
*Kikwete asema sababu za kumpa jukumu ni rahisi kumpata
*Awaomba madereva kutokwenda kasi wakati wa kuomba wadhamini
MTOTO wa Rais Jakaya Kikwete , Ridhiwani Kikwete amekabidhiwa mikoba ya kutembeza fomu za kusaka wadhamini katika mikoa 10 nchini akishirikiana na baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Baraza la Kuu la Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) na wanafunzi wachache kutoka Vyuo Vikuu nchini.
Kwa mujibu wa chama hicho ni kwamba Ridhiwani ndio atakuwa mwenyekiti wa kamati hiyo akishikiana na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Beno Malisa ambao watawaongoza vijana wngine 32 kuzunguka katika mikoa hiyo ambayo imegwanywa katika kanda nane ikiwemo Kanda A ya Dar es Salaam ambayo kiongozi wake ni ridhiwani pia.
Tukio la Ridhiwani kukabidhiwa fomu za kuomba wadhamini lilifanyika Mjini Dodoma jana mchana, baada ya rais kukamilisha tukio la kuchukua fomu asubuhi ambalo lilifanyika Makao Makuu ya CCM na kasha kufuatiwa na kukutana na wadhamini 250 wa Mkoa wa Dodoma.
Akizungumza mbele ya Rais Kikwete , Katibu Mkuu wa UVCCM, Maltin Shigela alisema vijana hao ambao viongozi wa jumuiya, makada na wanachama makini watazunguka katika maeneo hayo ambpo kila mkoa wanatakiwa kupata wadhimini 250 na hiyo inatokana na kwamba mgombea wao kutokana na majukumu kuwa mengi hivyo hataweza kutafuta wadhimini yeye mwenyewe.
Alisema katika mgawanyo huo wa kanda kila kila itakuwa na vijana wane ambao watashirikiana kuhakikisha wanalifanikisha suala hilo kwa wakati lakini pia kwa umakini mkubwa.Wakiwa huko maeneo ya mikoani watapata ushirikiano mzuri kutoka kwa wanachama.
“Katika kutafua wadhamini, chama kimeamua kutoa jukumu la kufanya kazi hiyo kwa vijana wetu wachama nkutoka jumuiya yetu lakini pia tunao wasomi kutoka vyuo vikuu vyote nchini ambapo walipatikana kwa utaratibu maalumu.Mwanzoni walikuwa 90 lakini tumeamua hao 32 ndio watafanya kazi hiyo,”alisema Shigela.
Kwa mujibu wa taratibu za chama Rais Kikwete aliamua kukabidhi fomu hizo kwa Ridhani ikiwa ndio ishara ya kuanza safari ya kwenda huko mikoani kwa ajili ya kutafuta wadhamini hao.
Rais Kikwete akizungumzia sababu za kuamua kumpa fomu Ridhiwani ili ashirikiane na vijana wenzake, alisema sababu kubwa inatokana na kwamba akimpa Ridhiwani itakuwa rahisi kuwasiliana naye na atakapomuhitaji itakuwa rahisi kumpata tofauti na mtu mwingine.
Alisema kazi ya kuomba wadhamini ni kubwa na inahitaji muda wa kutosha na kwa muda alionao sasa na majukumu yaliyopo mbele yake ndio maana ameamua kuomba vijana hao wasomi kuifanya kazi hiyo ambapo anaamini itafanyikla vizuri kwa sababu vyuo vimefungwa.
0 comments:
Post a Comment