Mkutano wa wahariri kuhusu Bima ya afya mjini Morogoro!!

Mkurugenzi wa NHIF Bwn Emanuel Humba akifafanua jambo juu ya mafanikio ya Mfuko sanjari na kuwashukuru wanahabari kwa kuwa chachu ya mafanikio hayo wakati wa mkutano wa sita wa wahariri waandamizi mjini morogoro unaoandaliwa kila mwaka na Mfuko huo kwa kuwakutanisha wanahabari kutoka kila kona yaTanzania.
Kutoka kulia Bw. H.I Mdee Mkurugenzi wa uanachama na shughuli za kanda, kati mkurugenzi wa kanda ya kati Bw. C. Mapunda na mshiriki mwalikwa mkuu wa kitengo cha masoko kutoka bohari ya madawa (MSD) Bw..Haule wakifuatilia kwa makini hotuba ya mkurugenzi mkuu

Kamati ya ufundi ya mfuko haikuwa nyuma katika kuchukua dondoo muhimu kutoka kwa wawasilisha mada kwenye mkutano wa sita wa wahariri na waandishi waandamizimbele ni afisa uhusiano mwandamizi wa NHIF Bwn L.singu,nyuma aliyesimama afisa itifaki Bw. Msifu Chenjela na anayechukua dondoo ni afisa uhusiano na itifaki Bwn Paul Marenga.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment