MFANYAKAZI AUNGUA KIWANDANI

Bw Mtolo Muminu akiwa katika Hospitali ya Dar Group.
MFANYAKAZI wa kiwanda cha kutengeza vioo vya Aluminium kilichopo Vingunguti barabara ya Nyerere cha Jijini Dar es Salaam, Bw. Mtolo Muminu, 32, akiwa amelazwa katika Hospitali ya Dar Group baada ya kuungua vibaya sehemu kadhaa za mwili wake hususani sehemu za makalio. Leo ni siku ya 18 akiwa hospitalini hapo ambapo alipelekwa baada ya kulipukiwa na mtambo wa kuyeyushia vyuma. Akihojiwa hospitalini hapo Mumimu alilalamikia utaratibu wa baadhi ya makampuni kutokuwa na vifaa vya kazi na vya kujisaidia wakati wa matatizo.
Habari kwa hisani ya .http://www.globalpublishers.

You liked this post? Subscribe via RSS feed and get daily updates.

0 comments:

Post a Comment